Kinachokuvutia wewe kwenye mahusiano ni muonekano wa mtu au tabia ya mtu?

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,269
40,054
Kumekuwa na tabia ya kubaguana katika kutafuta wapenzi; wapo wanaosema wanataka wapenzi wao mara wawe weusi, weupe, warefu, wanene, wenye chura, macho goroli, kiuno nyugwi, aliyejazia kifua n.k

Bila kujua huyo muhusika hakuomba kuzaliwa jinsi alivyo, sasa hii tabia ya kukosoa uumbaji kwa kujitangazia sifa zako za kumtaka umpendaye, hujui hunapingana na uumbaji?

Na hii inapelekea watu wengi kuwa singo mpaka uzeeni. Wengine wanaenda mbali mpaka kufanya upasuaji au maboresho ya maumbile yao. Sasa wewe kinachokuvutia ni muonekano au tabia ya mtu?
 
Tabia.

Kwasabubu hakuna kibonge asie penda kulakula.
I mean tabia ya mtu ndio hutoa na muonekano wake.
Kuna dada mmoja kibonge huwa ananifurahisha sana eti kanunua vifaa vya mazoezi na mipango mingi ya mazoezi lakini ukitazama kula yake yaani hata afanye mazoezi miaka buku hatakaa apungue yaani hali chakula kingi lakini anakulakula kila dakika yaani ni kulakula wa dunia nyingine
 
Japokuwa tabia ni muhimu zaidi ila kuna mionekano mingine ni kazi kuivumilia🐒
IMG_20211012_204516.jpg
 
Back
Top Bottom