Kinachokosekana kwenye filamu zetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kinachokosekana kwenye filamu zetu

Discussion in 'Entertainment' started by NasDaz, Aug 10, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]Hapa najaribu kuchambua kinachokosekana na kile tunachozani kinakosekana kwenye filamu zetu! Uchambuzi wangu ni mawazo binafsi kwavile mimi si mtaalamu katika tasnia husika ingawaje nina uzoefu usio haba katika utunzi wa stori(sio za filamu). Kutokana na hilo, uchambuzi wangu hautakuwa wa kitaalamu bali kutokana na vile ninavyoona mimi![/FONT]
  [FONT=&quot]WAIGIZAJI: [/FONT][FONT=&quot]Wapenzi wengi wa filamu za kibongo wanalalamika kwamba waigizaji wetu wanashindwa kuvaa uhalisia! Kwa maana nyingine, mwigizaji anaweza kuigiza analia huku uso wake umebeba tabasamu la chati! Hata nami nakubaliana katika hili, kwani kuna wakati panaweza kuwa na tukio la utekaji huku mtekwaji nae akionesha dalili zote za kukaa tayari kwa kutekwa! (NIMESOMEKA?)[/FONT]
  [FONT=&quot]STORY:[/FONT][FONT=&quot] Pamoja na yote hayo, binafsi naona tatizo kuu lililopo kwenye filamu zetu ni stori mbovu! Stori mbovu haiwezi kutoa filamu mzuri hata kama wachezaji wa filamu hiyo watakuwa magwiji wa filamu kutoka Hollywood(inaandikwaje vile?!) au wale wa Bollywood! Stori zetu ni mbovu kv utungaji wa stori unahitaji kipaji zaidi kuliko vinginevyo! I guess unaweza kum-train mtu kuwa mwigizaji na akawa mwigizaji bora kabisa lakini huwezi kum-train mtu kuwa mtunzi na akawa mtunzi mzuri! Uigizaji unahitaji CREATIVITY and/or TALENT lakini utunzi wa stori bora unahitaji TALENT + CREATIVITY + INSPIRATION! Unaweza kuwa na wazo (idea) bomba lakini [/FONT]
  [FONT=&quot]MSUKO WA MATUKIO: [/FONT][FONT=&quot]Ubovu wa stori yoyote ile unatokana na msuko mbovu wa matukio! Msuko wa matukio unahitaji creativity as well as inspiration. More often than not, creativity and inspiration ni gift from god.Pamoja na yote hayo, unapotunga stori yoyote inayohitaji msuko mzuri wa matukio meditation ni muhimu! Katika utunzi, inafika wakati mtu unakwama huna kitu cha kuandika. Mtunzi bora ataacha kuandika na ku-meditate ili apate kitu bora cha kuendelezea stori yake! Watunzi wetu wengi wa filamu hawana hicho kitu na matokeo yake kuishia kutunga stori zilizokosa msuko mzuri wa matukio! Msuko wa matukio ndio unamfanya mwangiliaji wa filamu(au msomaji wa stori) apate hamu ya kuendelea mbele zaidi ili kujua kitakachotokea.[/FONT]
  [FONT=&quot]CLIMAX ZONE: [/FONT][FONT=&quot]Stori iliyokosa msuko mzuri wa matukio inakosa Climax Zone! Climax zone ni ile sehemu ambayo msisimuko wa filamu/hadithi umefikia peak kiasi kwamba mtu hawezi kuwa tayari kuacha kuangalia filamu/kusoma hadithi anapofikia kwenye climax! Ingekuwa kwenye tendo la ndoa, Climax Zone ni pale mtu anapokuwa tayari kupiga bao![/FONT]
  [FONT=&quot]USHAURI: [/FONT][FONT=&quot]W[/FONT][FONT=&quot]atengenezaji wa filamu lazima wakubali kwamba si kila mtu anaweza kutunga stori kama wafanyavyo sasa! Kutunga stori kunahitaji kipaji na time! Unaweza kum-train mtu kucheza filamu na akafanya vizuri lakini huwezi kum-train mtu au wewe mwenyewe kutunga stori mzuri ikiwa kipaji cha utunzi hakuna. Stori iliyopwaya inaleta filamu mbovu hata kama waigizaji ni wazuri. Stori iliyosukwa vizuri inazalisha filamu itakayovutia kutazamwa na hata wasiojua lugha iliyotumika kwenye filamu husika. Ni bora watengenezaji wa filamu watafute watu wenye uwezo wa kutunga stori kuliko kulazimisha kuifanya kazi hiyo wao wenyewe kwani endapo yatakosekana niliyoyainisha hapo juu; filamu itapwaya.[/FONT]
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Jana nilimkuta mtu anaangalia filamu ya Ki Nigeria "Cain and Abel" nikaona yote uliyotaja hapo juu na mengine zaidi. Labda hii filamu haikuwa representative , lakini mimi nikaona wana matatizo yale yale tuliyonayo. Now I am not excusing our film industry, just pointing this out.

  Mimi nilijiuliza mbona movie mbovu kama hii inauzika ? Je sisi Waafrika tunategemea standards tofauti za acting kutoka kwa wacheza filamu wetu? Je tunaotegemea realistic acting kama ya Hollywood tunakuwa hatuitendei haki industry yetu ya sinema ? Je kuna watu wamechoka the realistic fights of Hollywood na wanataka a soft and fake looking fighting (to use just one common example) such as seen on Bongo / Nigerian movies ? Are we being critics irrespective of the culture in question and imposing Hollywood standards where we don't even have a Hollywood type audience ?

  Nawakubali wa Afrika Kusini katika sinema, wako karibu kabisa kama si sawa na the best of Hollywood. Nafikiri tunahitaji kusomea zaidi uigizaji, vifaa vya kisasa zaidi, kuanza kuonyesha filamu zetu katika majumba ya sinema na kutokubali vitu sub-standard. Sasa kuhusu sub-standard ni nini katika nyanja ambayo haina standards za kisayansi, hili ndilo swali interesting.
   
 3. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,974
  Likes Received: 21,138
  Trophy Points: 280
  MR KIGOSI anawajibu wote wanaokosoa movie zao na anatoa sababu kadhaa kwa nini mnaona mnachokiona kwenye movie zake:  WARAKA KWA MASHABIKI WANGU


  [​IMG] Kwanza kabisa ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa mashabiki wangu wote Kwa kuweza kunipa sapoti kubwa kwa kuzikubali kazi zangu nawashukuru sana kwa hilo. Kwani bila nyinyi nisingekuwa hapa ila ningependa kutoa ufafanuzi juu ya ili swala ambalo kila mara huwa Napata malalamiko juu ya utoaji sinema kwa haraka na kusema kuwa tuwaige Hollywood kwa kutoa sinema moja kwa mwaka, Ila ningependa kuwakumbusha kitu kimoja kuwa kuna tofauti kubwa kati ya Hollywood na Tollywood. Sisi tunacheza African story maisha yanayoizunguka jamii tofauti na Hollywood wanacheza sinema zinazotumia teknolojia kubwa sana na zenye kufikirika, pia mkumbuke kuwa tunachokipata ni kidogo kuliko kazi tunazozifanya tangu tuingie kwenye kiwanda cha filam ni miaka kumi tu. Tulipotoka ni mbali sana hivyo mashabiki tupeni muda wa kuendelea kufanya vitu vikubwa na si lawama za kila siku na kutukatisha tamaa. Hatukatahi kukoselewa, Ninaposema naingia kufanya shooting siyo kwamba ndio sinema inatoka laaa, ni kuweza kufanya kazi taratibu ili tupate ubora tunaohuitaji. Soko la filam Tanzania bado ni gumu sana hatuwezi kulinganisha na wenzetu kwa mfano, Denzel Washington akitoa sinema moja anatengeneza sio chini ya dola million kumi na na nane mpaka ishirini na tano. Sawa na na kama bilioni 30 za Tanzania, Tom cruise analipwa dola milioni sitini sawa na kama bilioni sabini za Kitanzania huyu ana haki ya kukaa mwaka mzima bila kutengeneza sinema. Mimi sifikii hata robo ya malipo hayo nikikaa mwaka mzima bila kutengeneza sinema nitakula nini? Wakati asilimia 50 ya Watanzania wananunua kazi feki. Jamani siri ya mtungi haijuae ni kata, Samahani kama nitakuwa nimemkwaza mtu ila nimejaribu kuweka jambo ili wazi ili mashabiki wangu waelewe japo kidogo. Mungu awabariki sana......
   
 4. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Huyu bwana anaeleza kimsingi kile kile nilichokisema, kwamba tusiwafananishe na Hollywood, ila naona kama kuna umuhimu apandishe shule zaidi na kuweza kujieleza vizuri zaidi.

  Arguments zake weak, na anaonekana kama mtu asiyeweza kuwa inventive, anayependa mteremko na anayefanya kazi ili kupata kipato tu, na wala haumizi kichwa sana kutoa bidhaa bora. Kama angesema kwamba hii ndiyo style yetu ya Tanzania iko tofauti na Hollywood, na kuna watu kibao wanaipenda ningemuelewa, lakini kwa kukubali kwamba wanalipua lipua essentially, ili kusudi wapate kipato naona kaharibu.

  Msanii hata kama ni kweli unatafuta kipato tu, hutakiwi kusema hivyo, inaharibu perception ya purity ya kazi yako. Inaonekana kwamba wewe umekuwa msanii si kwa sababu una kipaji, bali labda huna uwezo wa kufanya kazi nyingine yenye kipato zaidi, au huna uwezo wa kufanya kazi nyingine period. Majuzi hapa LeBron James kaondoka Cleveland Cavaliers ambako ilikuwa aende kuongeza mkataba na kupata kipato kizuri zaidi ya hicho anachoenda kupata Miami, lakini LeBron kakubali kushusha kipato na kuingia katika controversy na hometown yake, kwa nini? Anatafuta ushindi, anatafuta championship ring, anatafuta glory ambayo kipato hakiwezi kununua,anajua akipata ushindi na hiyo glory kipato kitakuja tu. Anakubali kuangalia ufanisi wake kabla ya kipato. Mtu yeyote anayeangalia kipato kabla ya ufanisi wake ni mufilisi wa mawazo.

  Afadhali basic PR na decency anayo.Positive.


  Mnaiga mpaka jina halafu mnataka msilinganishwe ?

  Kwangu mimi kutoa sinema moja kwa mwaka wala si issue, unaweza kutoa sinema nyingi utakavyo ili mradi ziwe bora. Ningeweza kusema ni sawa kwa Hollywood mtu kutoa sinema moja kwa mwaka kwanza kwa sababu industry ni kubwa, actors wako wengi, movies zinatolewa na maelfu kwa maelfu ya actors, kwa hiyo hata kila actor mmoja mkubwa akitoa movie moja kwa mwaka majumba ya sinema yatakuwa hayakauki sinema. Leo hii mkitaka hawa wacheza filamu wetu watoe movie moja kwa mwaka, wakati industry yenyewe si kubwa tutaweza kuwa na movies za kutosha au tutarudia movies kumi mwaka mzima ? Unaweza kusema watoe movie moja kwa mwaka kama kuna industry kubwa, kama kuna distribution network kubwa, kama kuna publicity machinery ya kueleweka, kama kuna a paying audience etc.

  Kwa hiyo kwangu mimi hili la movie moja kwa mwaka si issue, hata kina Alfred Hitchcock walikuwa wanatoa movies kibao kwa mwaka, na bado mpaka kesho ni legends huko huko Hollywood.

  What is his point here? Kwamba Hollywood wana special effects na teknolojia kubwa sana? Distinction yake hajaiweka clear, kwanza kabisa kwa sababu si kweli kwamba Hollywood hawana sinema za maisha. Halafu zaidi ya hapo, kuna sinema za indie (independent films) ambazo hazitegemei Hollywood, zinatoka kwa budget ndogo tu lakini acting creative na realistic, stories kabambe na bila kutumia teknolojia kubwa sana watu wanazifurahia. Naweza kukupa majina ya movies kama "Uninvited Guest" ya Mekhi Phifer , kama hujaiona itafute Uninvited Guest - Wikipedia, the free encyclopedia

  "Uninvited Guest" ni movie ambayo hata wasanii wa Tanzania ambao wanasema hawana teknolojia kubwa wanaweza kuitengeneza vizuri, hamna mlipuko mkubwa (maybe a gunshot or two if I remember correctly) hakuna car chase, hakuna pyrotechnics yoyote.Hata Tanzania mtu anaweza kutafuta nyumba nzuri Mbezi Beach akashoot movie kama hii, karibu movie nzima watu wako ndani lakini hata huwezi ku mind hilo kwa sababu plot line ni ya kusisimua kichizi, movie nzima karibu wako ndani but yet the movie is fast moving (unlike our movies where a 40 seconds scene can be stretched to 5 minutes). Kwa hiyo hili swala la teknolojia mimi silioni.Teknolojia si lazima katika kutengeneza movie nzuri.Kuna movie nyingi tu zimetengenezwa kwa kutumia creativity zaidi kuliko teknolojia. "Citizen Kane" arguably the best American movies ever made according to cinematographers, movie buffs and officionados, was filmed with more cinematographic creativity than technology. It is not about what you don't have, it is about what you can do with what you have. When given lemons, don't complain that others have oranges and therefore fare much better than you, when given lemons, make lemonade.

  I understand you gotta eat and all, I am not trying to knock you, lakini don't be too soft on yourself. Hata kama ni katika PR tu. Denzel huyo huyo mnayemsema ni big star sijawahi kumsikia anakuwa soft on himself, kila akiulizwa anakwambia anafanya kazi kama punda ma kubeba mizigo, he is ever hungry.Miaka kumi hiyo hiyo unayosema midogo Alexander The Great alipiga na kuhusuru kutoka Macedonia, Dameski, kapita Hindu Kush, Uajemi mpaka India huko. Sie tunashindwa kutengeneza film industry ya maana ? Hamna anayekukatisha tamaa, wewe mwenyewe inabidi ujielimishe zaidi kuhusu haya mambo, uwe na njaa ya kufanya vizuri zaidi sio ukionekana Dar tu, watu wanakupa offer kwenye vibaa unajiona star na kila anyekukosoa anakukatisha tamaa, inawezekana wewe ndiye unayekatisha tamaa wapenda filamu za bongo kwa kukubali kushindwa kirahisi hivi.


  Inaonekana hata kiswahili kinampiga chenga, huyu ndiye muigizaji wa sinema hajui kuandika "hatukatai". Halafu akikosolewa anasema anakatishwa tamaa.

  Sasa unajichanganya hapa, mwanzo umesema Tanzania hatuwezi kutoa movie moja kwa mwaka kwa sababu si Hollywood, nikafikiri mna kasi nzuri, hapa tena unasma mnatoa sinema taratibu ili kutafuta ubora, kipi ni sawa ? Na kama mnatoa movie taratibu ili mtoe na ubora ubora wenyewe uko wapi? Ndizo hizi movies zinazolalamikiwa kuwa na ubora hafifu au kuna nyingine?

  Eti "mimi sifikii hata robo", more like sifikii hata "robo ya robo ya robo ya robo"

  Labda soko la filamu zenu ni gumu kwa sababu hamna creativity, na kama mngekuwa na creativity mngepata soko si Tanzania tu, bali duniani kote. Mimi naangalia movies za Kichina, hazina teknolojia kubwa, hazina umagharibi wa Hollywood, hawaongei hata Kiingereza - Kiingereza unaona kwenye subtitles, there you have it, I watch Chinese movies with subtitles- lakini ni filamu nzuri sana kwa sababu zina sanaa ya hali ya juu, zina stories very interesting kuhusu tamaduni na historia zao, na mtu unaangalia unaona hawa ni serious actors, mara nyingine unaona hata hao Hollywood wanatamba kwa sababu ya marketing na cultural imperialism ya Marekani, but most of the blockbuster are really nothing much than sex and violence, almost everything is formulaic and predictable kama ushamuona will Smith katika "Independence Day" basi "Men in Black" na "I am Legend" ni variation zake tu, big bad aliens, big bad explosions, and big bad Willie, same story, different days. Kwa hiyo hata hiyo Hollywood si Rosetta Stone ya success vile vile.Kuna watu kibao hata huku Marekani watataka kuona filamu za Kitanzania zinazoeleza maisha ya watanzania, kuanzia wa mjini mpaka wa vijijini. Lakini hata hili nalo linatushinda, tukubali.

  Kwa hiyo habari ya teknolojia si kweli, habari ya soko si kweli kwa maana soko si Tanzania tu ni dunia nzima, huwezi kulaumu soko wakati hujatoa bidhaa nzuri. Ndiyo maana watu wanataka mtoe bidhaa ya kueleweka, kisha hata kama ni kazi ya kuwatafutia soko by word of mouth tutawafanyia tu,mbona tuna rafiki zetu wa mataifa mbalimbali ambao wanaopenda kuijua Tanzania na wangependa kusoma vitabu vya waandishi wa Kitanzania na kuona filamu za Tanzania? Lakini sasa hivi mimi siwezi kumpendekezea mgeni filamu ya Tanzania hata kama naweza kuipata kwa sababu itakuwa ni kujichoresha tu.
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Kiranga, watu hupenda pia kuona uhalisia wa mazingira yao, kwahiyo sinema za nyumbani zina ladha yake kama zilivyo za kigeni.
  We are not imposing Hollywood standard! but the standard should be meet for clarity and quality. Kama muigizaji yupo kijijini Tanzania ni unrealistic kuwa na Lexus,lakini baiskeli iwepo. Mfano angalia video ya Prof Jay nikusaidiaje nadhani, ameenda kuoa kijijini na unapata real life ya tz. Hapa nina maana std na quality are uncompromised being in Tollywood, Bolly,Noll etc.
  Tatizo! waigizaji wetu hawataki ushauri na ni waoga wa kutumia gharama, matatizo yote ni kwasbabu hakuna Well informed Directors au Producers. kama ubora ni hafifu utauza hapa tz tu, ubora ukiwa mzuri utauza EA na sikumoja Africa etc. Ubinafsi wa waigizaji, fikiri hivi kanumba ameshindwa kuwaona wataalam wa lugha wamsaidie ku edit sinema zake. Wapo kibao na wangefanya kazi hiyo bure, lakini too much know!
   
 6. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Mazee,

  Maswali na maswala yako yote nayaelewa, in fact nimesema hivyo hivyo kwa mapana na marefu (na kuongezea mengine) katika post yangu iliyoifuatia hiyo kama umeisoma.
   
 7. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Watamzania vipaji vipo, kinachokosekana ni shule, walipaswa waigizaji, waongozaji na waandaaji wa hizi filam kukitumia kile chuo cha Bagamoyo ili waweze kutoa filam nzuri zenye kueleweka na kupata waigizaji wenye kujuwa nini wanafanya.

  Angalia filam kama Tsotsi au Gods Must be Crazy I & II hazina hizo technolojia wanazodai. Kinachotakiwa tu ni mtitiririko mzuri wa riwaya na uigizaji mahili pamoja na waongozaji waliokwenda shule basi. Mbona zile filam za Yomba yomba na Muhogo mchungu zilikuwa nzuri na zinatizamika mwanzo mpaka mwisho.
   
 8. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Nao waache kuiga Wanigeria. Hata hivo vivazi na hasa vya akina dada ndio havieleweki kabisa.

  Hebu angalia filam za Ghana, ijapokuwa na wao wanaiga baadhi ya stories kutoka Nigeria, lakini huwa wanazibadilisha, na kwa kweli wakina dada wanavaa kiafrika kabisa.
   
 9. RRONDO

  RRONDO JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 25,974
  Likes Received: 21,138
  Trophy Points: 280
  hawa waigizaji/waongozaji/watungaji wa sinema za kibongo washafika mwisho wa upeo wao.......mengi mnayoyaona hawa watu pamoja na army ya fans wao hawayaoni.........wale wenye upeo/elimu wa fani hii waingie wawasaidie hawa watu wafike NEXT LEVEL.....nina imani kuna opportunity ya kutengeneza senti kwenye hii fani kwahio wenye uwezo waingie kwenye fani......
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Well said, tatizo ni wabishi na hawaambiliki! Wapo watu kama akina NasDa, kiranga etc hata kama si wataalam wa kukobea lakini wana upeo i.e next level. Shida ni hawa mastaa kwanza hawajui kutumia resource, hawajui ku connect na potential [ of course wana connect na akina aunt so n so...]. na hawajui ku solicit information, lakini ni wabishi sana. Labda pa kuanzia ni kubadilisha mtazamo wa fikra zao kwanza.
   
 11. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakumbuke wanapoanza kufanikiwa kidogo. watenge visenti vichache kwenda Chuo cha sanaa bagamoyo. Nikimuona Mrisho Mpoto kwenye music yake na kwenye filamu chache alizoshirkishwa unaona tofauti kubwakati yake na waigizaji wengine. Wasanii wasibweteke na vipaji
  Chuo cha sanaa bagamoyo wana training hata za muda mfupi. Lakini nadhani ukiwapa ushauri huu wanaweza kuona umewadharau.

  Kuna wataalam pia wa sanaa/performing arts kwenye vyuo kama UDSM. sijui kama wakitayaraisha filamu japo wanawapa wataalam waangalie kuproof view na kutooa ushauri. Sidhani kuna kufunzi UDSM akiombwa kutazama kazi ya msanii na kutoa ushauri wake wa haraka haaka atadai hela hhata akidai haziwezi kuwa nyingi.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Mtazamaji umenikumbusha Chuo cha Sanaa Bagamoyo. Hivi wana course za Kiswahili pale? Of course hawa wasanii wetu wanaweza kufaidi, lakini - excuse my digression- kuna hata wageni wanaotaka kujifunza Kiswahili, kuna chuo chochote cha kuheshimika chenye kozi za Kiswahili ?
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kama kuna mtu alishaona ile filamu inayohusu mauaji ya albino ikimhusisha mwanamuziki keisha. Mtunzi wake nadhani ni prof mbogo. Niliipenda sana japo kuna wahusika wachache hawakuvaa uhusika vizuri. Kuna ile tamthilia ya hukumu ya tunu. The best of all. Stori nzuri, wahusika wazuri sana. Ukitazama igizo la simu ya mkononi, wahusika wake ni wakongwe na wanajua wafanyacho. Huwa napenda sana kutazama. Sijui kwa nini huu ubora hauko kwenye filamu. Kuna makanjanja wengi. Mtu akishakuwa na jina basi anataka kucheza filamu. Huyo ray asilete visingizio. Tatizo ni uigizaji mmbovu na stori mbovu zilizojaa mapenzi ya kitoto. Black Amerikan movies hazitumii teknolojia ya ajabu kiivyo na wala si za kufikirika kama asemavyo ray. Nimezitazama karibu zote. Zina watunzi wazuri ajabu. Wahusika wako more than natural... Nitaandika sana ila tu waigizaji wa bongo wajue wao ni bado. Wakiweza kunishawishi mimi kununua kazi zao basi watakuwa wamewashawishi wengi. Kizuri gharama wandugu. Nitaingia rasmi kwenye tasnia ya filamu kwa makusudi mawili hivi; kutunga simulizi na kuhakikisha uhalisia wa muigizaji.
   
 14. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu inaonekana tayari una ubongo unaoweza kuona mengi, ukiingia huko unaweza kuwafunisha mengi. Naweza kusema kwenye upande wa sound, mwanga na video quality-wamepiga hatua kubwa sana, inagwa nako kuna matatizo. Lakini content wise naweza kuwapa asilimia 10 kati ya 100. Kwanza wanazingatia mavazi zaidi kitu ambacho si muhimu kwenye TV, wanazingatia uzuri wa sura kitu ambacho ni cha wasoma habari kwenye televisheni, na kuonesha sehemu ambazo haziendani na mazingira ya filamu zenyenwe.

  Story zao ni za mapenzi tu as if watazamaji wao wote ni uneducated, ambao kwao kitu sophiscated ni mapenzi tu. Bado mpaka sasa naona kuwa kina Sumbi na Bocha, na Bishanga,Waridi na mwezao Aisha walikuwa far better that hawa jamaa. Wanaboa kweli, even worse wanaanza hata kuexport ujinga huu.
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  pia unayosema ni kweli. Wasanii wa kwenye maigizo wanaonekana kuwa juu kiuigizaji. Tatizo imekuwa kwamba filam wanacheza watu wenye majina na mvuto wakati maigizo ni wale wenzangu na mie ambao aidha walijisomea sanaa au hukesha na kushinda wakijifunza namna ya kuigiza lakini maisha yao yakiwa chini. Nimemsoma dada mmoja kwenye fema. Anaitwa maria sarungi. Yupo kwenye tasnia kwa muda mrefu. Anasema kinachokosekana kwenye hii tasnia ni hadithi nzuri ya hapa tz. Siku watakapoogopa gharama na kucheza filamu kitaaluma zaidi ndio wakati mapinduzi ya filamu yataanza bongo
   
 16. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #16
  Aug 14, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280
  Upo sahii mkuu, kinachokosekana sio hizo teknolojia kwani unaweza kuwa na teknolojioa bora kabisa lakini kama mtiririko ni mbovu bado filamu haiwezi kuwa ya kuvutia!
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Aug 14, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  tatizo kubwa ni mgawanyiko wa majukumu wa wana tasnia ya filamu.

  filamu inatungwa, script inaandikwa, inaigizwa, inakuwa edited, costume zinachaguliwa na mtu huyo huyo mmoja.

  wanahtaji kujua what they are good at and stick with it, mengine wawaachie waliokuwa wajuzi zaidi.
   
 18. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #18
  Aug 14, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0

  Mhhhhh swali gumu sina uhakika tusaidiane kutafuta majibu

  Kiranga Inaonekana training zao ni za kingereza tu. je unadhani inaweza kuwa kikwazo. Binafsi nadhani hatamsanii aliyepata D ya english form four bado anaweza. Nahisi wanaweza kuwa na pcatical training zaidi kuliko theory.
   
 19. A

  Anold JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,380
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Mimi nafikiri kosoro ambazo zimeelezwa, waigizaji wetu na waongazaji wa filamu wazichukue kama changamoto. Uigizaji ni fani na wale wote wanaojiingiza huko ni lazima wajue hivyo, Kuvaa uhusika kwenye filamu ni jambo la msingi na la muhimu kushinda inavyodhaniwa, kuvaa uhusika ni kuvaa uhalisia wa kitu au mtu au jambo n.k, bila kumudu hilo kinachofuata ni kichefuchefu, kwa mtu makini kama atabaini hiyo kasoro basi kama anaangalia filamu ujue ndiyo mwisho wake wa kuangalia au kufuatilia tamthilia hiyo. Ieleweke wazi kuwa watu wanapoeleza kasoro kama hizi isidhaniwe kuwa ni majungu, bali ichukuliwe kuwa ni changamoto ambayo inahitaji kufanyiwa kazi. Kuna idadi kubwa ya watu sasa hivi wamejitokeza na kuwa waigizaji au kuwa waongozaji wa filamu, sina uhakika kuwa kwa wingi wao huo wanasifa za kuwa waongozaji, mimi naamini wengi ni wapotoshaji na masilahi ni mbele daima.

  Suala la kuigiza uhalisia mimi naamini ni kitu kinachowezekana, fikiria mtu anaigiza nafasi ya kuwa kipofu lakini mara uone kafumbua macho, hivi hapo unaweza kusema ni ukosefu wa shule au kutokuwa makini?
  ushauri wangu kwa wale wote wanoigiza filamu n.k ni kuwa makini, wakielewa wazi kuwa kile wanachokifanya kinavuta hisia za watu, bila hivyo filamu zao zitakuwa ni kazi bure. Ni lazima wasanii wafanye kazi ya ziada kuhakikisha kuwa suala sio kushindana kutoa idadi ya filamu bali waelewe kuwa kazi ni kufanya waaminiwe na watanzania tena wa rika na kada zote. Utitiri wa filamu unaoingia sokoni kila kukicha ndiyo chanzo kikubwa kinachovuruga soko la filamu hapa nchini. Lazima na wakati umefika kwa wasanii wajue hata ikiwezekana waige kutoka kwa wasanii wengine waliopiga hatua kujua ni namna gani wamefikia hapo walipo, Kujaa ujuaji na dharau ni kukaribisha anguko la kisaanii. Wasanii wetu ni lazima wabadilike ili wapige hatua kinyume cha hapo filamu zao zitajaa madukani lakini hazitauzika kwa kiasi na idadi wanayotegemea, aidha ni lazima vyombo vinavyohusika katika kusimamia wasanii wawasaidie wasanii, hili ni pamoja na kulinda kazi zao lakini pia kuhakikisha kuwa Kazi wanazotoa wasanii zinakuwa na ubora unaohitajika hata kukubalika kimataifa achilia mbali hapa nchini. changamoto zilizotelewa kama kasoro wasanii wetu wazifanyie kazi badala ya kujaribu kujitetea maana utetezi wao hauwezi kuwaletea tija badala yake watajiangamiza wenyewe.
   
Loading...