Don san tan
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 562
- 433
Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu , na hatimaye kuweka uongozi mikononi mwa Waafrika , ambao ndio wengi visiwani humo (230,000 hivi).
Tarehe 12 Januari 1964 asubuhi na mapema, mwanachama wa ASP John
Okello ( 1937 - 1971 ?) kutoka Uganda aliongoza wanamapinduzi 600–800 wa kisiwa kikuu cha Unguja kushinda polisi wa nchi na kuteka silaha zao. Halafu walielekea Zanzibar Town walipompindua Sultani Jamshid bin Abdullah na serikali yake.
Kiongozi wa ASP Abeid Karume ,asiyekuwa na msimamo mkali akawa rais wa kwanza wa nchi.
Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania.
Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.
Karibuni kuweka Updates za kuhusu kinachojiri kisiwani humo, leo ikiwa ni Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, Sherehe ambazo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Rais Dr. Ally Mohamed Shein.
Nawatakia kumbukumbu njema katika Sherehe hizo za mapinduzi ikiwa leo ni tar 12/1/2017.