Yaliyojiri Ikulu: Mazungumzo kati ya Viongozi wa dini nchini na Rais Magufuli

Mkuu sasa kama hujawahi kusikia dhehebu lake/analoliongoza haina maana halipo!
Ana dhehebu na ni mchungaji!
Uliza watu wa Iringa ndo wanajua!
Msgwa ni kiongozi wa dini au dhehebu lipi? Kwa maelezo tuliopewa, walioalikwa siyo kila mchungaji/padre/katekista/shehe nk. Waliitwa viongozi wanaoongoza dini au madhehebu yao. Wengi waliofika ni viongozi wenyewe wenye huduma zao kama vile akina Kakobe, Mwingira, Gwajima, nk, au wawakilishi waliotumwa na viongozi wanaoongoza madhehebu mfano Bakwata, RC, KKKT, nk.

Mchungaji Msigwa sijawahi kuisikia huduma yake inayojitegemea. Labda swahi hili lingemhusu mama Lwakatare ambaye ni mbunge na ana huduma yake anayoiongoza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni jana tu viongozi wa dini walikutana na Rais ikulu, kwa mwaliko wa Rais. Viongozi hawa wa dini wanaishi na watanzania, kwa fikra za watu wengi, ni kuwa viongozi hawa wa dini wanayajua matatizo ya waumini wao kwa undani.

Waumini wengi walitarajia kuwa matatizo na madhira yao mengi yangelifikia sikio la Mh. Rais kwa kupitia wao. Nina imani Mh. Rais aliwaalika viongozi akiwa na dhamira ya kusikia mapungufu yaliyopo kwenye utawala wake ili aweze kuyafanyia kazi.

Waumini wengi walivunjika moyo pale ambapo viongozi wao wengi wa dinia walipoonekana kuitumia nafasi waliyopewa, kuacha kutoa maoni kuhusiana na matatizo ya waumini wao, na zaidi wakaitumia nafasi hiyo kutafuta recognition kwa Rais.

Wengine wakatumia nafasi hiyo kuelezea jinsi wao walivyo muhimu katika uongozi wa nchi.

Baadhi walienda mbali zaidi na kutamka kuwa Rais alikuwa amechelewa mno kuwaalila, alitakiwa awaalike wakati alipochukua madaraka ili wapange kwa pamoja namna ya kuongoza nchi!

Kwa maoni yangu, mahusiano ya viongozi wa dini kwa serikali yanaishia kwenye kushauri na kuonya. Na pia ni jambo jema kukiwepo mahusiano mazuri kati ya serikali na taasisi za dini lakini siyo kutengeneza urafiki wa kuongoza nchi.

Viongozi wa dini wana majukwaa yao mahekaluni, misikitini na makanisani ambako wanaweza kuwahubiria waumini wao, wakiwemo watawala na watumishi wa serikali. Huko wanaweza kuonya, wanaweza kukemea, wanaweza kushauri, na kusiwepo wa kuwaingilia. Kualikwa na Rais kwaajili kusikia maoni yao, ni matakwa ya Rais, na siyo wajibu.

Viongozi wa dini wasitafute urafiki na watawala wala wasitafute kuwa sehemu ya watawala. Kama watakuwa marafiki wa watawala au watajiingiza kwenye serikali, watapoteza ihalali wao wa kukemea, kushauri na kuonya.

Zaidi ya kutafuta recognition, viongozi wa dini walitumia muda wao mwingi kupongeza juhudi na mambo mema anayofanya Rais. Kupongeza siyo jambo baya kama kuna jambo jema linafanywa. Lakini kupongeza tu bila kushauri kwenye kasoro, hasa zile kubwa, nadhani hata Rais mwenyewe hatakuwa amefaidika chochote toka kwenye hekima ya hawa viongozi wa dini maana siamini kama Rais aliwaalika kwa nia ya kumpongeza.

Kinachoshangaza zaidi, ni viongozi hawa hawa wa dini, ndio wanaotoa kasoro nyingi za utawala wa Mh. Rais Magufuli wakiwa mbali naye. Ni hawa hawa ndio wanaoandika nyaraka kali kali dhidi ya serikali na watawala. Lakini baada ya kuitwa wanachoweza kutamka ni pongezi tu! Tunachojiuliza, yale malalamiko kwenye nyaraka ilikuwa ni tuhuma za uwongo au chuki ya kitotambulika kuwa na wao ni muhimu? Au wanashindwa kunena KWELI kwa sababu ya woga mbele ya mtawala? Au viongpzi hawa ni wanafiki, wanatamka uale wanayodhani aliywewaalika atapenda kusikia? Au pengine yawezekana yale malalamiko ya kwenye nyaraka yalikwishafanyiwa kazi yote?

Kama viongozi wa dini ni waoga, ni nani atakuwa jasiri?

Kama viongozi wa dini ni wanafiki, wanawafundisha nini waumini wao? Rais atawaheshimu vipi viongozi wanafiki?

Au viongozi wa dini wanawashutumu watawala kwa vile watawala hawataki kuonesha kuwa viongozi wa dini ni muhimu sana katika kuongoza nchi?

Au viongozi wa dini hawakujua Rais alikuwa amewaitia nini, pamoja na ukweli kuwa aliwaeleza mwanzoni mwa mkutano wao?

Viongozi wa dini tumewasikia. Tutawadharau kama baada ya kutoka ikulu ndimi zenu zikanena tofauti na tulovyowasikia mkinena mlipokuwa mbele ya Mh Rais.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza kuodherasha madhila na matatizo mbali mbali ambayo waumini dini mbali mbali wanayo ?
Hebu yataje........

...kwa mfano ujasiri gani walikosa !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
next time hata Mwingira hatoalikwa, anataka wanaomsifia tu.
Alilalamikia wachungaji wake kuwekwa ndani mara kwa mara na maDC. Mwingira ana tuhuma za kupora ardhi wa wanakijiji na kuhodhi eneo kubwa sana. Ameweka askari/walinzi ambao mara kwa mara hujichukulia sheria mkononi.
Yupo Askofu kwenye kikao hicho hicho ana amini kuna Wachungaji/viongozi wa dini wanastahiki kuwekwa ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafundisheni watu kumjua mungu ,kuacha dhambi, kuheshimu mamlaka na mamlaka kuheshimu waajiri wao (wananchi) bila kichola.
Huko kwenye nyumba zenu za ibada mjue kunawafuasi wasimba pamoja na Yanga na wengine wapita njia tu hawana upande wowote.

Viongozi wetu wa dini tunaomba sana mseme mapungufu ya wanasiasa kwa usawa bila kuigopa au kupendelea.

Msithubutu kuvaa jezi ya upande wowote wkt mnachezesha mechi ngumu kabisa ya Yanga na Simba bakini Neutral kwa maslahi mapana ya taifa letu

Dini zinamchango mkubwa sana katika kuleta amani au vurugu ktk taifa.

Mtuache na AMANI YETU
Mungu awape moyo wa busara watumishi wa mungu mbarikiwe sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom