Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha 8, mkutano wa 3
Kipindi cha maswali na majibu
Swali: Seriakali ina mpago gani wa kuwabana waajiri wanaowatishia wafanyakazi kujiunga na vyama vya kutetea haki zao?Kipindi cha maswali na majibu
Majibu: Tayari sheria ipo na sheria inaruhusu wafanyakazi kujiunga na kikundi chochote cha wafanyakazi.
Aidha wizara inaendelea kutoa mafunzo kupitia warsha, vipindi vya redio na televisheni.
Pia sheria inaendelea kuwashughulikia waajiri wanaowabagua wafanyakazi.
Swali: Ongezeko la ombaomba, kwa nini serikali isiwawezeshe kwa kuwapa kipaumbele kwa zabuni mbalimbali?
Majibu: Serikali itaendelea kusimamia sheria ya watu wenye ulemavu kwa kuendelea kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu.
Watendaji wanawajibika kutoa kipumbele kwa watu wenye ulemavu.
Serikali kupitia Ilani ya chama cha Mapinduzi inaelekeza kutoa asilimia 30 ya tenda zote kwa watu wenye ulemavu.
Swali: Ni lini serikali itaanza kutoa posho kwa wenyeviti wa vijiji na mitaa ili iwe motisha kwao?
Majibu: Serikali inarudisha asilimia 20 ya mapato ya halmashauri kwa ajili ya kulipa posho za wenyeviti hao.
Kila halmashauri imetakiwa kuhakikisha inakusanya fedha za kutosha ili posho hizo ziweze kutosheleza.
Swali: Serikali ina mkakati upi kufanikisha mafunzo ya kompyuta ukizingatia changamoto ya vifaa na walimu.
Swali: Serikali inapeleka, umeme vijijini, inashirikiana na kampuni ya microsoft, inatoa mafunzo ya kompyuta kwenye vyuo vyote vya ualimu nchini.
Serikali inapanga kuwapa kipaumbele mkoa wa rukwa na mikoa yote ya pembezoni kwenye elimu hii ya kompyuta.
Swali: Serikali ina mpango gani wa kurejesha baadhi ya maeneo ya mashamba ya Mitaba?
Majibu: Wizara kushirikiana na ofisi ya Wilaya, hamashauri ya Kibaha, ofisi ya mkoa na wananchi wanashirikiana kumaliza mgogoro wa shamba hilo.
Aidha Wadau wametakiwa kutoa elimu kuacha kuvamia maeneo ya serikali na maeneo mengine.
Swali: Serikali haioni ni wakati sasa wa kurejesha mashamba yaliyobinafsishwa bila kuendelezwa hasa wilayani Korogwe?
Majibu: Serikali iko kwenye mchakato wa kukagua mashamba na kuwasilisha wizarani kwa ajili ya kubatilisha.
Taratibu za ubatilisha zikikamilika kwa kupata kibali cha rais, mashamba yatarejeshwa kwa wananchi.
Swali: Je ni lini serikali itatekeleza ahadi ya kumaliza tatizo la maji hasa katika Jimbo la ubungo?
Majibu: Serikali inatekeleza miradi yote ya maji inayoendelea jijini Dar es salaam, mradi wa Ruvu Chini na Ruvu juu umekamilika.
Mpaka sasa uzalishaji wa maji umefikia lita za ujazo milioni 390 kwa siku ukilinganisha na mahitaji ya lita za ujazo milioni 450 kwa siku. Miradi yote ikikamilika kutakuwa na uzalishaji wa lita za ujazo milioni 750 kwa siku ambayo yatatosheleza mpaka mwaka 2032.
Swali: Ni kwa nini usajili wa biashara ya mazao ya misitu hufanyika kila mwaka? Serikali haioni inawaongezea mzigo wafanyabisahara?
Majibu: Usajili wa kila mwaka husaidia kutekeleza mipango iliyowekwa kila mwaka.
Ni fursa ya kuchangia pato la taifa kupitia kuchangia kila mwaka.
Aidha uvunaji wa mazao ya misitu wa wilaya ya Manyoni ulizuiliwa kutokana na uharibifu.
Swali: Serikali inatoa tamko gani juu ya tangazo namba 28 la mpaka mpya wa bonde la Usangu na hifadhi ya Ruaha baada ya kushindikana?
Majibu: Serikali inaendelea kutekeleza tangazo namba 28 na bado inaendelea na fidia kwa wananchi.
Swali: Serikali inatoa kauli gani kuhusu kuwarudishia maeneo ya msitu wa hifadhi Sayata?
Majibu: Kubadilisha matumizi itasababisha uharibifu wa mazingira hasa mmomonyoko wa udongo na kufanya uchafuzi katika ziwa victoria. Serikali haina mpango wa kulirejesha kwa wananchi kwani litasababisha uharibifu wa mazingira na ziwa victoria.