Kinachoisumbua Tanzania ni upinzani hewa

Upinzani hewa ni matusi kwa wale wote wanakosoa au kushauri njia sahihi za kulijenga taifa letu.
Bila upinzani Magufuri asingekuwa raisi.Kauli ya raisi hapa kazi tu imetokana na madai ya upinzani juu ya serikali za CCM kwa muda mrefu.
 
Kama wewe kaka ake itakuwa kaka poa yaani unajua dadaako alikuwa anapata vitu adimu Na sasa anavikosa, enyi kizazi cha mwendo Kasi wekeni ABS.
Anakera kila mara anatafuta njia za kum provoke Sa8 na kuna thread humu kuwa alikuwa mchepuko na akatoswa, hivyo inaonyesha alikuwa anapata vitu adimu ndio maana hamsahau na kila wakati lazima amu attack
 
Wasira alitabiri chadema itakufa tena akiwa waziri wa serikali lakini wapi ..... yupo wapi sasa ..... sembuse wewe kitasa tu
 
Lazima tukiri tu katika siasa za vyama vingi tulifika pazuri lakini kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita tumerudi nyuma miaka 24. Kazi kuu ya upinzani si kuombea nchi mabaya au kufurahia majanga bali ni kukosoa serikali kwa hoja na mantiki.

Kwa Tanzania sasa hatuna upinzani bali tuna kundi la 'wachawi', walioyaunga mkono miaka iliyopita sasa hawayataki. Hawataki kuona maboresho katika miundombinu,nishati,udhibiti wa rushwa nk. Kuna tatizo la msingi hapa na kama lisipofanyiwa kazi basi hakutakuwa na tija ya kuwa na upinzani, wananchi kila kukicha wanakata tama na upinzani. Kada maarufu wa upinzani amesisitiza kuwa reli haina umuhimu, mwingine leo ameandika kiwanda cha Dangote ni hatari kwa uchumi wa Tanzania,Mwingine hataki kuona Tanzania ikinunua ndege, hawapendi kuona mamboresho kwenye sekta ya elimu wamesusa hata kuchangia kwa hali na mali wao wanasubiri kukosoa.

Tatizo hili limezidi kuwa sugu na kusababisha baadhi ya vijana kuacha kutumikia serikali katika Nyanja mbalimbali na kuamua kuwa omba omba kwa wanasiasa kwa kigezo cha 'ukamanda'.Kunahitajika msaada hapa wasiachwe waangamie hawa.

Kinachoisumbua Tanzania kwa miaka zaidi 50 ni UJINGA, MARADHI na UMASKINI. You have to get the facts right...usituhangaishe na matatizo hewa huku ukiacha matatizo ya kiukweli..
 
Back
Top Bottom