Mm bado napenda kuelimishwa kwa wale wanaoijua shule hii watueleze vzr ukweli wa sakata hili.Naamini kuna watu wanaoijua ukweli hasa wazazi waseme nao sababu ndio wahanga wakubwa wa sakata hili.Hicho ndio kiini chenyewe.
Watu wengi Arusha wanajua kisa kilianzia siku Magufuli alipokuja Arusha kwenye kampeni na waendeshaji wa shule ya St. Jude wakagoma kuswaga wanafunzi wake kwenda Sheikh Amri Abeid kuongeza idadi ya wahudhuriaji kwenye mkutano wa CCM.
Wamiliki wa shule waliweka wazi kuwa, shule yao haina itikadi yoyote ya vyama vya siasa, uongozi wa shule haukuwa na mamlaka ya kuwahusisha kwa lazima wanafunzi wake kwenye itikadi za vyama na mwisho uongozi wa shule hauwezi kuhahakisha usalama wa wanafunzi wake kwenda uwanjani.
Yote kwa yote, chuki ya serikali ya Magu dhidi ya ukanda wa Kaskazini ni kubwa mnoo, St. Jude huenda ni miongoni mwa taasisi za Elimu zilizokuwa zinawindwa kuangamizwa kwa muda mrefu sana, maana ni miongoni mwa taasisi za mtaji wa kimaendeleo ya kijamii kwa kizazi cha watoto na vijana waliopo kanda ya Kaskazini.