Kinachoigharimu Tanzania ni kukosekana kwa watunga sera wanaoelewa 'Public Policy'

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Ni sahihi pia kusema Tanzania kuna 'Public Policy Crisis'. Ntatumia neno Sera nikimaanisha 'Public Policy'.

Sera ni nini? Sera unaweza kusema ni sheria au miongozo ambayo inawekwa ili kutatua changamoto ambazo zipo kwenye jamii. Maana yake ni kwamba, ukiona kuna sera ambazo hazitatui changamoto za wananchi wa nchi yako, solution huwa ni kuzibadilisha, kuziboresha, au kuzifuta kabisa.

Kwa maana nyingine ni kwamba, sera ni lazima ilenge haswa 'welfare' ya wananchi kwa kuangalia 'cost and benefit' ya sera husika.

Miaka ya hivi karibuni, hususani miaka mitatu iliyopita kumekuwa na maneno sana kuhusu, issue ya kodi kuwa sio fair kwa watanzania. Wananchi na baadhi ya wanasiasa ambao wanaelewa madhara ya kodi kuwa 'Unfair' kwenye uchumi, wameongea sana, lakini mpaka sasa hakuna chochote ambacho kinafanyika. Ni kama vile tatizo linazidi kuwa kali siku hadi siku.

Upande mngine wa serikali, wao wameamua kwamba kodi ni lazima ipatikane ili miradi ya maendeleo itekelezwe, lakini wanashindwa kujua kwamba, hata kama hii miradi ikikamilika yote, kama hakutakuwa na sekta binafsi imara ya wamwekezaji wa ndani, hii miradi yote itakuwa 'Underutilised'.

Ni kama vile kusema, kama hamna wafanyabashara, hiyo reli itasafirisha kitu gani? Ikiwa kwa mfano, mfumo wa kinyonyaji wa kodi utaondoa nusu ya wafanyabiashara ambayo ikapelekea kupungua kwa matumizi ya reli ambayo imetumia mabilioni, hapo itakuwa taifa limepata hasara au faida?

Ndo maana nnasema, Tanzania kuna Crisis ya Public Policy, ni kama vile mambo yanafanyika kutimiza lengo moja tu na kuleta madhara upande mwingine kitu ambacho hakitakiwi kabisa unapo design Public Policy.

Kuna tatizo pia kubwa kuwaachia wabunge ambao wengine sio wasomi kuwa ndo wawe watunga sera. Nadhani ikiwa nchi hii tunataka kuibadilisha, itatubidi tuunde mfumo mpya wa kutunga na kusimamia sera za nchi.
 
Back
Top Bottom