Kinachofaa kwa Vyama vya Siasa kwa Ushindi 2020 Muungano wa Mabadiliko ya Fikra(MUMAFI)

Civilian Coin

JF-Expert Member
Dec 2, 2012
2,305
4,334
Kinachofaa kwa Vyama vya Siasa vya Upinzani-Tanzania.

MUUNGANO wa MABADILIKO ya FIKIRA (MUMAFI).

Don Nalimison, Mwanamziki, Mtetezi wa Haki za Binadamu na Mshauri wa Maswala ya Kiusalama Duniani leo nakuja kuunda Umoja utakaowapa Ushindi wa Kishindo Uchaguzi Mkuu 2020 kwa vya Kisiasa hasa Upinzani.

NINI KIFANYIKE?
Kwa miaka mingi Wapinzani wamesota Sana kuitafuta Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(SJMT) na ile Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) ili kuweza kuiongoza kwa ufanisi bila mafanikio.February Mwaka 2013 kupitia gazeti la FAHAMU nilitoa Makala maalum katika Mfumo wa mahojiano na kupendekeza kuachiana majimbo na kuwa na mgombea mmoja, nashukuru lilitekelezwa pale Wapinzani walipo kuja na Umoja wa Katiba Mpya (UKAWA) na kufanya Yale niliyoyawaza kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Sasa hatuko kipindi Cha Kusaka Katiba mpya, Bali ni kipindi Cha kuwajenga Wanachi Kifikra ili wajitambue wasiwe wanaburuzwa buruzwa tu Kama mang'ombe. Ni kipindi ambacho jamii ya Tanzania inatakiwa kuwa na Fikra ya kuchagua kilicho Bora zaidi yaani MUMAFI. Ni kipindi Sasa Cha kuunda Muungano mpya utakao wabadilisha Fikra WANANCHI na Muungano huo uitwe "MUUNGANO wa MABADILIKO ya FIKRA kwa kifupi MUMAFI.

MUMAFI iwe ndio DIRA ya kushika DOLA na kuiweka mikononi mwa Wanasiasa Safi wasio na Roho mbaya na wenye nia ya kweli ya kuijenga Nchi Kiuchumi na Kifikra. MUMAFI iwe ndio ngao ya Taifa na Ukombozi kwa WANANCHI waliotelekezwa na Chama kilichogandamana kwa muda mrefu.

MTAPATAJE USHINDI?

Mgombea wa URAIS awe mmoja anayekubalika na Vyama vyote bila chuki Wala ugomvi. Mfano:
1.CHADEMA awe Tundu Lisu.
2.CUF awe Ibrahim Lipumba.
3.ACT awe Bernard Membe
4.Vyama vidogo vigawiwe majimbo na kata kulingana na mchango wao utakavyo kuwa.

Katika Vyama vitatu vyenye nguvu mmoja asimame kuwakilisha MUMAFI na wote mkubaliane bila kinyongo.Hii NI kwa BARA na kwa Zanzibar abaki Yule Yule Maalim Seif Sharif kutokana na historia yàke ya Kisiasa Visiwani Zanzibar na asiwekewe kinyongo. Kwa kufanya hivi Ushindi upo uchi kabisa yaani ni kuweka tu na kuchukua Serikali zote mbili.

MUMAFI itawapa mafanikio Upinzani ya kushika hatamu bila pingamizi na mjikite zaidi katika kuelimisha ukweli Nchi ilivyo na inavyotakiwa kuendeshwa, Kama unavyojua kuendesha Nchi sio kuwatisha watu na kuwateka na kuwafanyia unyama halafu mnasema mnatetea wanyonge kwa mgongo wa Barabara na majengo ya kuhadaa Umma. Mfanye siasa Takatifu zenye ubora wa Hadhi ya juu Sana. Msikubali KUONEWA kwenye Haki na mtimize wajibu. Mliheshimu Jeshi la POLISI na mfanye nalo kazi vizuri japo lipo mikononi mwa Chama kilicho madarakani. Ila muwe MAKINI Sana maana Jeshi la POLISI wakati mwingine hutumika Kisiasa kwa masilahi ya watawala wasiotaka kuachia ngazi.

MUMAFI ndio kioo Cha Watanzania wote wa Rika zote na ngazi zote bila kujali rangi Wala ukabila Wala dini wala kanda. Msisahau kumpa Ubunge Viti maalum mama yangu Mzazi Bi. Laurencia pale Wilayani Kahama kwa masilahi ya Mshauri wenu na Dada yangu Magreth Chagula msimuache bila Udiwani Viti maalum pale Mbezi Luis-DSM.

Ni hayo tu, nawatakia kutafakari Jambo hili kwa kina Sana.

DON NALIMISON
O'CLOCK MUSIC PRESS
+255 682 94 29 01.
E-mail: donnalimison70@gmail.com
27/07/2020.
 

Attachments

  • IMG_159586383064F.jpg
    IMG_159586383064F.jpg
    107.1 KB · Views: 1
Hebu tujaribu kutafakari vifupisho vingine vya kuupa muungano wa hivyo vyama duh Sasa MUMAFI inatofauti gani na MUMAVI
Kwa Hilo jina tu sioni ushindi hata agombee malaika.
 
Don epuka kuwa na ndimi mbili saivi we ni public figure kuwa na msimamo kwene mambo yako.

Ule mpango wako wa kutuachia nchi yetu na kujiunga kwa tramp umekufa au?.

Unatuchanganya wafuasi wako wachache tuliosalia.
 
Don epuka kuwa na ndimi mbili saivi we ni public figure kuwa na msimamo kwene mambo yako.

Ule mpango wako wa kutuachia nchi yetu na kujiunga kwa tramp umekufa au?.

Unatuchanganya wafuasi wako wachache tuliosalia.

Ushauri hauna Nchi nilichofanya nikutoa Ushauri.
 
Sometime chaneli zinasoma muda mwingine kunguru wanatua kwenye antena inakua chenga tupu
 
Back
Top Bottom