Kinachoendelea Uingereza ni dhahiri Mwl Nyerere ataendelea kuishi

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
"Kufanya dhambi ya ubaguzi ni sawasawa kabisa na kula nyama ya mtu,ukishakula nyama ya mtu utaendelea kuila tu".

Haya ni maneno ya mwalimu aliyoyatoa akiwaasa watanzania kutokujaribu kuuvunja muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Mwalimu aliendelea kusema "Nje ya muungano hakuna Zanzibar, nje ya muungano kuna wanzibari na wanzibara, kuna wapemba na kuna waunguja, ile dhambi ya ubaguzi haiishii hapo".

Sasa tunaona Uingereza mara tu baada ya kuamua kujitenga kutoka kwenye jumuiya ya umoja wa Ulaya tayari Scotland nao wanampango wakujitenga kutoka Uingereza warudi kwenye jumuiya ya Ulaya.

Hapa tunaona ile dhambi ya ubaguzi aliyotuasa mwalimu kwamba ni kweli haiishii hapo badala yake wanaendelea kugawanyika vipande vipande.

RIP JK Nyerere.


New up to date
Zaidi ya saini milioni mbili za raia wa uingereza zakusanywa kuhitaji kura zilizopigwa kufanya maazi ya kujitoa EU zirudiwe.
Inabaki palepale wao kwa wao wanaendelea kuvurugana wakiendelea kutafunwa na dhambi ya ubaguzi.
Source BBC.

New up to date
Zaidi ya nusu ya mawaziri wa leba kujiuzuru Uingereza.Ikumbukwe hiki ndicho chama kilichokua kikipiga kampeni ya uingereza kujitoa EU.
Source BBC

New up to date
Scotland inapanga kuizuia uingereza kujitoa EU kupitia bunge na kwamujibu wa katiba uingereza itahitaji baraka za Scotland ili kujitoa EU.
source BBC.
 
Ukweli ni kuwa European Union ilishaanza kuwa tatizo la nyongeza badala ya suluhu ya matatizo ya wanachama.

Changamoto za usalama, ugaidi, masherti kwenye bajeti , ulipaji wa kusuasua wa madeni ya wanachama, suluhu za kuchelewa, redtape na nyingine nyingi zitawatoa wanachama wengi zaidi kwenye EU.

Zanzibar imegeuka koloni la Tanganyika na linaendeshwa kimabavu.

Muungano huu pia umekuwa tatizo la nyongeza tena tatizo mtambuka!

Kama ilivyo sasa kwa EU inayofikiria maboresho ya kisera na kimuundo, ndivyo ilivyopaswa kuwa kwa huu muungano wetu.

Tukiendelea kutembea huku tumesinzia,hakuna mwisho mzuri.
 
Nimeipenda Comments ya Waziri wa fedha wa Italia, Pier Carlo Padoan amesema kwamba, Jumuiya ya Ulaya ilikuwa inatengeza zaidi matatizo kuliko kusolve matatatizo.

Hivyo, anaona kama Jumuiya hiyo inatakiwa kuendelea kuwa na nguvu inatakiwa mfumo wote ubadilike na utengenezwe upya. Lakini kwa hali ilivyo sasa wananchi wa nchi nyingi za Ulata nao watahamasika kufanya kama wa UK walivyofanya.
 
Tizama south Sudan nao baada yakujitenga na kaskazini.Kaskazini ilibaki salama lakini south wakajikuta si wamoja tena,Wakajikuta kuna kabila la Dinka na kabila Nuer na hapo mpaka leo bado hakujatulia wanaendelea kubaguana.
Mwl ataendelea kuishi.
 
Nimeipenda Comments ya Waziri wa fedha wa Italia, Pier Carlo Padoan amesema kwamba, Jumuiya ya Ulaya ilikuwa inatengeza zaidi matatizo kuliko kusolve matatatizo. Hivyo, anaona kama Jumuiya hiyo inatakiwa kuendelea kuwa na nguvu inatakiwa mfumo wote ubadilike na utengenezwe upya. Lakini kwa hali ilivyo sasa wananchi wa nchi nyingi za Ulata nao watahamasika kufanya kama wa England walivyofanya.

Sio England ni UK bana.
 
Tatizo mnapofanya ubaguzi mnasahau kipo kilichowaunganisha kuwafanya mjione "sisi" na wengine "wao" . Mkishajigawa "wao" watabaki salama kwavile hawakuzalisha zao la "usisi" lakini wale waliojiona "sisi" wakibaki peke yao ile dhana ya "usisi" haifi, wataanza kuangaliana na kugundua hata "sisi" si wamoja kwasababu lukuki! RIP JK Nyerere!
 
Napoleon the Great tried to unify Europe and he failed..he used his sweat and blood for unsuccessful. Huko alikolala ataanza kugeuka maana this would be his personal failure for those who like to emulate him. Ndio maana pale Brussels kuna 666
 
Nafikiri Waingereza wanaelewa zaidi kwa walichoamua kukifanya

gimmy's wa Mwakaleli sidhani km unajua vizuri wazungu wanafikiri kwa umbali gani mbele hadi ukaanza kunukuu tungo tata za mwalimu

Waingereza wameonyesha ukomavu wa democracy wa kuigwa na dunia nzima.

muungano wowote unatakiwa uwe wa hiyari hata vitabu vitakatifu viliwahi andika hivyo

Muungano wa kulazimisha pasipo barka za wananchi Mungu hawezi bariki.
 
Tatizo mnapofanya ubaguzi mnasahau kipo kilichowaunganisha kuwafanya mjione "sisi" na wengine "wao" . Mkishajigawa "wao" watabaki salama kwavile hawakuzalisha zao la "usisi" lakini wale waliojiona "sisi" wakibaki peke yao ile dhana ya "usisi" haifi, wataanza kuangaliana na kugundua hata "sisi" si wamoja kwasababu lukuki! RIP JK Nyerere!
Wapemba wanatakiwa kujifunza katika hili waache upuuzi wao.
 
Scotland 2014 walifanya referendum ya au kubaki UK au kuwa huru.
Matokeo ya kubaki yalikuwa 55% na uongozi uliopigia kelele uhuru wa Scotland ukajiuzulu.
Naona wamepata sababu ya kurudi kwenye siasa sasa.
Ila baadae busara itawaambia zimwi likujualo halikuli likakwisha.
Changamoto zilizofanya UK akimbie EU bado zipo na zinafanya wanachama wengine wajitafakari.
Scotland akijipima mwenyewe kurudi EU atazitafakari upya changamoto hizi. Na list itaongezeka kwasababu hatakuwa kwenye mgongo wa UK.
Scotland imefungamana zaidi kila nyanja na UK kuliko EU. Kilichowafanya wasione ukubwa wa changamoto ni sababu zilikuwa zinapita kwenye shockabsorber [ UK] kabla ya kuwafikia.
Na sasa wanaweza kuwa na knee jerk reaction kwasababu wanaona biashara zao, assets zao na savings zimepoteza thamani kwa pound kushuka thamani.
Ila hili lilitegemewa, ni shock ya muda mfupi na mambo yatakaa sawa.
 
Nafikiri Waingereza wanaelewa zaidi kwa walichoamua kukifanya

gimmy's wa Mwakaleli sidhani km unajua vizuri wazungu wanafikiri kwa umbali gani mbele hadi ukaanza kunukuu tungo tata za mwalimu

Waingereza wameonyesha ukomavu wa democracy wa kuigwa na dunia nzima.

muungano wowote unatakiwa uwe wa hiyari hata vitabu vitakatifu viliwahi andika hivyo

Muungano wa kulazimisha pasipo barka za wananchi Mungu hawezi bariki.
Sasa unataka kusema muungano wa Tanganyika na Zanziber hauna Baraka?
 
"Kufanya dhambi ya ubaguzi ni sawasawa kabisa na kula nyama ya mtu,ukishakula nyama ya mtu utaendelea kuila tu".

Haya ni maneno ya mwalimu aliyoyatoa akiwaasa watanzania kutokujaribu kuuvunja muungano wa Tanganyika na Zanziba.

Mwalimu aliendelea kusema"Nje ya muungano hakuna zanzibar,nje ya muungano kuna wanzibari na wanzibara,kuna wapemba na kuna waunguja,ile dhambi ya ubaguzi haiishii hapo".

Sasa tunaona Uingereza mara tu baada ya kuamua kujitenga kutoka kwenye jumuiya ya umoja wa ulaya tayari Scotland nao wanampango wakujitenga kutoka Uingereza warudi kwenye juiya ya ulaya.

Hapa tunaona Ile dhambi ya ubaguzi aliyotuasa mwalimu kwamba ni kweli haiishii hapo badala yake wanaendelea kugawanyika vipande vipande.

RIP JK Nyerere.
Wacha wagawanyike tu, hawana faida na sisi, kwanza wao wametugawanya sana waafrika na hawataki tuwe na umoja.
 
Back
Top Bottom