Kinachoendelea sasa Tanzania na ukweli wake ni upi hasa?

Lord denning

JF-Expert Member
Jun 3, 2015
14,059
28,581
Amani iwe nanyi wadau,

Natumai wote mu wazima na mnaendelea vizuri tu na majukumu yenu. Baada ya kukaa kimya kwa muda kama kawaida yangu leo imenibidi nijitokeze na nitolee uchambuzi wangu kwa yanayoendelea saivi Tanzania.

Nchi ya Tanzania hivi karibuni imekuwa ikikumbwa na matukio kadhaa ambayo kama hulka ya watanzania wengi ilivyo ya kupapalikia mambo nadhani itawachukua muda mrefu sana kuelewa na hata kama wataelewa basi itakuwa too late.

Kwenye kichwa cha habari nimesema kinachoendelea sasa Tanzania na ukweli wake ni upi hasa? Hiki ni kichwa cha habari nilichokifikia baada ya kufanya tafakari ya kina na kwa faida ya kikazi hiki na kijacho ni lazima hili jambo nilieleze humu.

1. Suala la wabunge kutaka kutumia bunge katika kuiangusha serikali ya ndugu Magufuli.

Hili linaweza kuwa jambo geni machoni na masikioni pa wengi lakini huu ndo ukweli wenyewe. Hapa Tanzania kuna kipindi hasa mwaka 2008 ambapo ulianza kujengeka utamaduni mpya wa wabunge iwe kwa maslahi yao au kwa maslahi wanayojua wao kutaka kutumia platform ya bungeni kwa nia zao ovu za kuiangusha serikali. Ni katika kipindi hiki ambapo serikali ya ndugu Jakaya ilipata wakati mgumu sana kutokana na jambo kuu kuwa wabunge walitumia bunge vibaya katika kutekeleza maslahi yao binafsi dhidi ya seriakali na hatimaye siku ya mwisho waliweza hasa kuitikisa serikali ya kikwete. Kipindi hiki watu wenye ushawishi na watu wenye fedha waliweza kutumia ushawishi wao kwa kiwango kikubwa sana na hata kuwashughulikia wateule wa raisi kupitia wabunge na kwa ukweli waliweza kumzidi nguvu ndugu kikwete. Kikwete alipoteza wateule wake wazuri kama Khamis Kagasheki, Prof Sospeter Muhongo, Eliakim Maswi, David Jairo, Prof Anna Tibaijuka na wengineo wengi sana kwa sababu tu ya siasa za chuki, wivu na siasa za ubinafsi zilizokuwa zinaendeshwa ndani ya bunge. Kwa mtu mwenye akili Prof Muhongo hakutakiwa kuondoka kwa escrow scandal, kwa mtu mwenye akili Khamis Kagasheki wala hakutakiwa kuondoka kwenye operesheni tokomeza. Napenda kusema vilevile kuwa kwa mtu mwenye akili hata Edward Lowassa hakutakiwa kuondoka kwa Richmond scandal kwa kuwa hata leo hii hakuna ushahidi wowote kuwa Lowassa alikula hela na hata aliifilisi nchi kwenye issue ya Richmond. Haya yote yalikuwa ni matokeo ya bunge kutumika vibaya na hatimaye siku ya mwisho wabunge waliweza kuitetemesha na hata kukaribia kuiangusha serikali ya ndugu Jakaya. Kuna ushahidi kuwa wabunge walijitengenezea ukwasi wa kutisha kwa sababu tu ya kutumiwa na watu mbalimbali kwa mslahi yao kwenye kipindi hichi.

Tatizo limekuja kwa ndugu Magufuli kwa sababu huyu sio mgeni wa bunge, sio mgeni wa siasa chafu za wabunge na wala sio mgeni wa serikali kwa kuwa amehudumu kwenye nafasi ya juu kabisa kwa muda mrefu. Yeye anajua kuwa ni wabunge gani wanatetea maslahi mapana ya taifa najua ni vitu gani kwa namna gani huwa vinafanywa na wabunge na huwa vinafanywa kwa maslahi yapi hasa. Ndo mana kaamua kuwapuuza kwa sababu amejua nia yake ni kuiondolea focus serikali yake ili itoke kwenye reli na kuanza kushughulikia porojo za mitaani na umbea. Suala la wabunge kutaka kumpaka matope raisi kwa kupitia idara ya usalama wa taifa ni mfano mmoja wapo. Watanzania wengi wanabebwa na ngonjera hizi lakini hawajui ni kwa dhumuni gani zinafanyika. Hivi kwa akili za kawaida mtu anasema ana uthibitisho kuwa watu Fulani ni wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa alafu taifa linataka kumuamini bila kujiuliza atathibitisha kivipi? Uthibitisho kuwa Fulani ni ofisa wa idara ya usalama wa taifa unathibitishwa kwa kwanza kutoa namba yake ya kazini,siku alioajiliwa n ahata kitambuliso chake na faili namba yake. Kwa akili za kawaida ni nan9i anaweza kupata details nyeti kiasi hicho za taasisi ya kijasusi hapa duniani??? Ni hapa tu Tanzania ambapo mtu anasema ivo na watu bado wanamshangilia na kumuamini, nan do mana hapa raisi magufuli anaishia kuwadharau tu na kuwacheka.

2. Suala la Makonda na Magufuli.

Kwa kipindi sasa kumekuwa na jitihada za kumuangusha Magufuli kwa kumuhusisha na Makonda. Ni kweli makonda anaweza kuwa na udhaifu wa kawaida wa kibinadamu ila kuna upande mzuri wa makonda unaomfanya akubaliwe sana na Magufuli. Kwa wasiomuelewa Magufuli, yeye anapenda watu wenye uthubutu kwa kuwa hata yeye alipofikia pale alifika kutokana na kuwa na tabia ya uthubutu katika mambo ya msingi. Na ndo mana haishii kumpenda Makonda tu anampenda na kumkubali hadi Rc Gambon a hata DC wa Arumeru kwa kuwa tu nao wana tabia ya uthubutu kwenye mambo ya msingi. Magufuli ni mtu anayetaka matokeo chanya haraka na kwake haijalishi umechukua njia gani ila kama dhumuni lako ni kupata matokeo chanya haraka yeye atakuunga mkono. Paol Makonda ana tabia hii, ana uthubutu anajiamini na ana tabia pia ya kujaribu vitu ili tu apate matokeo ya haraka. Ndo mana imetokea kwa viongozi wenzake wengi kumchukia kudhaniu anapendwa na Magufuli kwa sababu ya kabila huku wakisahau kuwa hata Edward Hosea alikuwa msukuma na akatumbuliwa na hata Kitwanga alikuwa msukuma lakini pia alitumbuliwa. Magufuli haangalii kabila anaangalia uchapakazi wako tu.

3. Suala la utekaji.

Ni ukweli usiotia shaka kuwa hata siku moja idara ya usalama wa taifa haiwezi kuhusika na tukio lolote linaotokea sasa nah ii ni kwa sababu zifuatazo. Kwa kuanza na Ben Saanane na Roma kwa mtu mwenye akili hata akitoka usingizi hawezi hata siku moja kuamini hili kwa kuwa naamini hawa watu hawana umaarufu wa kufikia hata robo ya watanzania kwa iyo haitatokea wakawa threat kwa kiwango hata kuja kufikia kwenye attention ya idara hii nyeti. Ni watu wasiofikiri vizuri tu wanaoweza kuziamini ngonjera hizi na ndo mana hata raisi amelidharau.

Hitimisho

Kwenye hotuba yake raisi Magufuli alisema amejitoa sadaka na aliomba watu wamuombee. Kwa wengi walidhani ni maneno matupu tu yasio na maana ila alijua ni kwa nini alisema vile. Nchii hii ilikuwa na syndicate nzito zilizokuwa na mzizi kuanzia chini hadi juu. Syndicate hizi ziliitauna nchi na kuiharibu vibaya sana. Huyu Magufuli ksajitolea kudeal nazo na anadeal nazo kisawasawa ndo mana tunaona kelele hizi.

Mungu Ibariki Tanzania, Mungu mbariki Raisi Magufuli.
 
Back
Top Bottom