Kinachoendelea nchini na uwezekano wa rais Magufuli kuchukiwa na wana CCM wenzake

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Mjadala wa hama hama unaendelea na kuacha masuali mengi, tunashuhudia kutupiana maneno kwa BAADHI YA MAKADA WA CCM wanavyotofautiana kuhusu namna wapinzani wanavyopata nafasi ndani ya CCM na serikalini. Upande wa pili wapinzani wanalalamika kuhusu hujuma za kidemokrasia na kisiasa.

Wadadisi wanahoji hili wimbi la kuhama, baadhi ya ccm wanapongeza kwamba ni kukubalika kwa rais lakini katikati ya safari wanaibuka CCM wengine wanaanza kuonesha wasiwasi.
Jambo moja muhimu hapa ni nini kinahofiwa hasa na hawa wanaoonesha wasi wasi ? majibu yako mengi yakiwemo na tishio la kupotea matumaini ya kupata nafasi na kuvurugwa kwa itikadi za chama na mengine mengi.

Hata hivyo hofu hii ya wana CCM imezidisha zile penyenye kwamba inawezekana Rais Magufuli ana ajenda zake nyuma ya pazia. Mnasaba na hili wimbi la kuhama wapinzani kuna minongono mingi kama ifuatavyo.

1. Pengine rais amegunduwa kitisho ndani ya CCM kwa hivyo anaandaa CCM mpya inayotokana na wapinzani ili kuja kukimkingia kifua na kumlinda kutokana na maamuzi aliyoyafanya na atakayokuja kuyafanya huko mbele ambapo yumkini hayatakuja kuwafurahisha MAKADA wenzake hasa wafia chama na wahafidhina.

Maeneo haya yanahusika

i. Mabadiliko ya katiba kwenye maeneo mbali mbali
ii. Muungano na makando kando yake
iii. Suala la Zanzibar
iii. Mabadiliko ndani ya CCM n.k

2. Pili pengine kuna jambo la dharura linamtesa kuhusu maamuzi, inawezekana FALSAFA ZAKE na misimamo yake inakwazwa na anahitaji kundi lengine liweze kumsadia.

Katika hali zote hizo na nyengine si bure kuwa, kuwe na wimbi hili la kuhama hama kwa hoja zile zile tena kwa wakati mahsusi.

Kwani kuna umuhimu gani wa kisiasa kwa sasa CCM na serikali kuweka nguvu kubwa kwa hii hama hama ? Majibu hayaendani na uhalisia hasa ikizingatiwa hizi gharama za chaguzi na ukimya wa serikali.

Ikifika hali hiyo LAZIMA CCM WATACHUKIA TU, na watamchukia Rais Magufuli.

Mantiki na sayansi ya siasa inabashiri huu si upepo wa kawaida na yawezekana muda si mrefu tutapata jibu.



Kishada
 
Huyu jamaa anachukiwa na almost watu wote including wana CCM wenyewe

Kumbuka tafiti zilizofanywa na Twaweza zilibainisha kuwa umaarufu wa Magufuli.unashuka kwa kasi kubwa sana
 
Ujinga ni hawa wanaoamia CCM kudhani kwamba watakua na uhakika wa nafasi zao uchaguzi ujao, aminini nawaambia hakuna mtu atakayerudi kugombea kati ya hawa wanaoamia sasa hivi, kutakua na siasa za ubaguzi mkubwa ndani ya chama kuliko wakati mwingine wowote, mfano mtu anaachaje kumuunga mkono Jerry Slaa akamuunge mkono Mwita??
 
Kama kusemwa ni sumu Kwa kweli mngeshamwangaza Mhe rais wetu! Haki haipendwi na watu kumbe hujiingiza kwenye vyama vya siasa Kwa masrahi mapana ya kwao tu na si vinginevyo



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ujinga ni hawa wanaoamia CCM kudhani kwamba watakua na uhakika wa nafasi zao uchaguzi ujao, aminini nawaambia hakuna mtu atakayerudi kugombea kati ya hawa wanaoamia sasa hivi, kutakua na siasa za ubaguzi mkubwa ndani ya chama kuliko wakati mwingine wowote, mfano mtu anaachaje kumuunga mkono Jerry Slaa akamuunge mkono Mwita??
Hao ccm ukawa mwisho wao 2020 watakatwa wasiamini,wataharibiwa potepote na kurudi nyuma hawawezi yuko wapi tambwe hiza,kaburu,yule muuza mayai Mkurya wa dar alijui hilo kakalia kutukana mamba tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii hii miccm isiyokuwa na akili?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo hapo
tapatalk_1534827679228.jpeg
FB_IMG_1534819537108.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Attachments

  • FB_IMG_1534819537108.jpg
    FB_IMG_1534819537108.jpg
    22.1 KB · Views: 12
Back
Top Bottom