Kinachoendelea kyerwa na karagwe ni ujinga uliopitiliza - uchaguzi serikali za mitaa

chitambikwa

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,937
1,195
Mabomu yanapigwa ngazi za Vitongoji – Kisa Pingamizi.
Jana watu Zaidi ya 500 wamewekewa Pingamizi Kijiji cha Murongo- Kyerwa na msimamizi wa uchaguzi eti si raia wa Tanzania. Wanachanchi wakaandama kutaka ufafanuzi, polisi wakaingilia kati kwa KUPIGA MABOMU 9 YA MACHOZI NA RISASI 2 ZA MOTO.
Watu 125 wamewekewa pingamizi kijiji cha Kihinda – Kyerwa, polisi wakaendelea na wembe ule ule.
Ieleweke kuwa katika kijiji cha Murongo Mgombea wa CHADEMA alishinda kura za maoni CCM, wakazichakachua akahamia CDM.

Viongozi wa CHADEMA wamepeleka matatizo hayo kwa Mkurugenzi wa wilaya ambaye aliamuru mara moja watu walejeshe kama wapiga kura halali lakini mtendaji wa kata amesema hatawarudisha watu hao. Kijiji cha Murongo kipo mpakani Mwa Tanzania na Uganda. Kwa sasa viongozi wa CHADEMA wapo ofisini kwa Mkurugenzi wakitaka Barua kutoka kwake ikitoa amri ya kuwarejesha mara moja wapiga kura hao.
Duru za siasa zianasema ukanda huu unagomabania sana na mafisadi kwani ndo njia ya kusafirisha kahawa za Magendo kwenda nchi ya jirani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom