Kinachoendelea Kenya kumbe Ulimboka ilikuwa sawa kushambuliwa

Mkuu kuna kazi zingine unajulishwa kabla hujaanza kazi tangu ukiwa chuo kwamba hutakiwi kugoma kwa sababu zinahusu roho za watu. Mfano Polisi wote wakigoma sibitakuwa balaa ujambazi, kubakana, kuchomeana nyumba moto, na kuuwana? Au askari wa jeshi la ulinzi JWTZ(TPDF) wakaamua kugoma wakati Malawi wanaingiza jeshi lao kutushambulia itakuwaje? Je huu mfano wa JWTZ hauoni kama unafanana na madaktri wanaogoma huku hospitalini kukiwa na wagonjwa kibao maisha yao yanategemea hao daktari.

Ingekuwa wanagoma kwa vile hawalipwi mshahara kabisa kwa muda wa miezi miwili ningewaunga mkono kwa vile wataishi vipi? Lakini kwa madai yale no justification ya kuvunja kiapo chao cha kutogoma.
JWTZ wenyewe walishawahi kugoma sembuse madaktari?kwako wewe uliona madai ya kijinga kwao waliyaona ya msingi,,wewe unadhani kama waliyokubaliana yangefanyika wangegoma?
 
ndio gharama za mapinduzi,,wapo wataokufa,wataokuwa walemavu n.k maisha lazima yaendelee..tujiulize wamefikiaje huko?sababu ni zipi?
You look to be smart lady.....I wish ningekuwa na make mwenye uwezo kama huu....
 
ndio gharama za mapinduzi,,wapo wataokufa,wataokuwa walemavu n.k maisha lazima yaendelee..tujiulize wamefikiaje huko?sababu ni zipi?

Mapinduzi ya kudai nyongeza ya 300%? Kama daktari hajali uhai kuna haja ya kuendelea kuwa nao?
 
Sio usalama tu, hata TCRA waliripoti hili mahala husika, huyu anaweze kua shahidi mzuri. Anataka kutuambia kua serikali huteza na kuumiza raia wake. Naweza kua miongoni mwa watakaoenda kushinikiza huyu mleta mada akamatwe.
Ndugu jukwaa hili ni la mawazo huria.
Unapoanza kuleta hoja za tuhuma za kimahakama hapa unapotea njia.
Ninadhani wewe kunahabari unazifahamu zaidi ya mtoa mada, ambazo unauhakika kuwa zinaukweli,basi ziweke wazi kumpinga na hoja zake ili ukweli uweke wazi wewe unayefahamu.
Hivi haujawahi kusikia serikali mbalimbali zinavikundi vya kimafia kudhibiti wapinzani wake?
Mfano Kenya, akina Tom Mboya na Dk.Owuko waliuawa na nani? Ninekutolea mfano huo utulize akili zako kutafakari mambo.
Sababu serikali kama haihusiki moja kwa moja, ni lini ilisema imekamata watesi wa Ulimboka na kuwafungulia mashitaka?
Usipende kutishia nyau pahala panapotakiwa tafakuri jadidi na pana.
Tishatoto yako hiyo inafanana sana na kumtolea lugha ya kitisho mtu kwa kumuuliza "hivi haunijui mimi ni nani?" Unani wako unatakiwa uutambulishe kwa uchambuzi wa mambo, hapo jf itaku-like na siyo kutaka kubabaisha watu humu.
Tuhuma ikiishatolewa na upande unaotuhumiwa ukakaa kimya, maana yake ni kukubaliana na tuhuma hizo.
 
mimi sioni kosa hapo...shule ya medicine mizinguo af mtu anakuja kucheza na elimu za watu....yaani wanasiasa wajinga sana...
 
Mtoa mada usikurupuke kusema madaktar wanalipwa fedha nyingi ,kwa nchi zetu licha ya fan hii kuwa ngumu na hatarishi kwa watoa Huduma still serikali nyingi za Africa zimekuwa zikiwalipa wanasiasa fedha nyingi kwa kupayuka tu majukwaan wakati wanawapuuza medical practitioners ,unaweza ukagoogle most paid jobs in US or Europe uone tofauti ya mishahara ya madaktar na fani nyingine kisha ulete mrejesho hapa sio kulaumu tu Madaktari wabinafsi wakati wanafanya kazi zenye risks kwa maisha yao na kuokoa maisha ya wananchi
 
Huo nao ni ujuha wa kiakili. Unawalaumu madakitari wanaodai malipo ya mishahara unasahau kuna wabunge ambalo wakikaa tu kwa Siku moja wanalipwa hela inayolingana na mishahara wa Dr na hawakatwi kodi. Acheni ujinga
 
Mkuu kuna kazi zingine unajulishwa kabla hujaanza kazi tangu ukiwa chuo kwamba hutakiwi kugoma kwa sababu zinahusu roho za watu. Mfano Polisi wote wakigoma sibitakuwa balaa ujambazi, kubakana, kuchomeana nyumba moto, na kuuwana? Au askari wa jeshi la ulinzi JWTZ(TPDF) wakaamua kugoma wakati Malawi wanaingiza jeshi lao kutushambulia itakuwaje? Je huu mfano wa JWTZ hauoni kama unafanana na madaktri wanaogoma huku hospitalini kukiwa na wagonjwa kibao maisha yao yanategemea hao daktari.
Unafahamu risk zilizopo kazini? Unafahamu kuwa serikali imeshindwa kuzitimiza? Kama Dr anashindwa kupata chanjo ya Hepatitis B atakuwa na moyo wa kazi
 
Walioamrisha Dr Ulimboka ateswe hawana Amani ndani ya mioyo yao na hawapo madarakani tena wamebaki na vidonda maisha yao yote na laana ipo juu yao hivi Pinda nani anakumbuka hat kama aliwahi kuishi karibu na ikulu maana alisema enough is enough, Kikwete hata siha ya mwili ukimwangalia kama amekula ndimu bado Msangi pale Mwanza yatamrudi tuu endelea kufurahia kuuwa watu wanaosema ukweli lakini mwisho wake ni kichapo toka kwa mwenyezi Mungu
 
Na yule aliyekuwa anaongoza Mgomo ili Watanzania wafe ndiyo leo Katibu Mkuu wa Chadema eti naye anataka kuwa Raisi wa nchi hii, nchi ambayo alikuwa tayari kuwauwa Wananchi wake kwa kuhimiza mgomo ili tu kuishinikiza Serikali!
Ni kweli kabisa huyu ndiye alikuwa kati ya viongozi wakuu wa huo mgomo. Ulimboka alikodiwa tu na hawa viongozi. Ulimboka wala hakuwa mwajiriwa wa serikali. Yeye alikuwa na NGO yake ambayo alikuwa anaendelea na kazi zake kama kawaida wakati wa huo mgomo ambao kwake hata ungefanikiwa haukuwa na masilahi yo yote kwenye NGO yake. Wakina Mashinji walikuwa wajanja sana, walimkodi Ulimboka ili awape cover up na walifanikiwa. Maelfu ya watanzania masikini walikufa. Ulimboka aliwapa taabu sana serikali, akibadilisha madai mara kwa mara hadi yalipomfika hayo yaliyomfika kutoka kwa ndugu waliopoteza wapendwa wao.
 
JWTZ wenyewe walishawahi kugoma sembuse madaktari?kwako wewe uliona madai ya kijinga kwao waliyaona ya msingi,,wewe unadhani kama waliyokubaliana yangefanyika wangegoma?
Mkuu nikumbushe lini JWTZ waligoma wakati nchi inashambuliwa na adui? Hapa hoja ya msingi sio kwamba madai ya madaktari hayakuwa ya msingi bali kugoma wakati watu wanakufa wodini. Madai yao yalikuwa ya msingi lakini kiapo/maadili ya kazi yao inakataza kugoma.
 
Huo nao ni ujuha wa kiakili. Unawalaumu madakitari wanaodai malipo ya mishahara unasahau kuna wabunge ambalo wakikaa tu kwa Siku moja wanalipwa hela inayolingana na mishahara wa Dr na hawakatwi kodi. Acheni ujinga
Mbunge akigoma hakuna anaekufa wala kupata ulemavu lakini kada za kazi kama askari, dokta, na wauguzi wakigoma kuna athari kubwa sana.
 
Unafahamu risk zilizopo kazini? Unafahamu kuwa serikali imeshindwa kuzitimiza? Kama Dr anashindwa kupata chanjo ya Hepatitis B atakuwa na moyo wa kazi
Kazi nyingi tu zina risky lakini kuna watu wamejitoa kuokoa maisha ya watu wakati kuna upungufu wa vifaa salama vya kazi. Sio sahihi kudhania ni daktari pekee ndio hufanya kazi mazingira hatarishi.
 
Back
Top Bottom