Kina Warioba, Mwinyi, Kimiti na Vijana wa zamani wakae kimya sasa; tunalipia hatia yao

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982


Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba

Kama kuna kitu kimeanza kunigusa pabaya katika fikra zangu ni kauli za mara kwa mara za wale wanaotajwa kuwa ni “viongozi wa zamani” wa taifa letu ambao hutoa kauli mbalimbali za kujaribu kuonesha kuwa nchi imefika pabaya. Kauli za hivi karibuni za aliyekuwa Waziri Mkuu Bw. Joseph Warioba na zile za aliyewahi kuwa Waziri na Mkuu wa Mkoa kwa muda mrefu na Mdhamini wa CCM Bw. Paul Kimiti zinanifanya nianze kuona kuwa kama taifa tunaanza kuchezewa akili na wale ambao waliwahi kuwa viongozi.


Lakini vile vile kauli za aliyekuwa Rais wa Tanzania Mzee Ally Hassan Mwinyi kuhusu masuala ya madawa ya kulevya na viongozi wa dini nazo zinanifanya niamini kabisa kuwa viongozi wetu hawa wa zamani wanaishi katika ulimwengu wa wale wanaokana. Yaani, wale ambao hawajakaa chini na kuangalia ni kwa jinsi gani maamuzi yao wao wenyewe ndio yamelifikisha taifa letu leo hii.


Wazee hawa wanapozungumza japo inaonekana kana kwamba ni katika “uzalendo” ukweli ni kwamba wanajaribu kujitenga na matendo na misimamo yao wakati walipokuwa madarakani. Ndugu zangu, leo hii tunalipia hatia yao. Wanayo hatia na wakati umefika waanze kukiri hatia hiyo na kuliomba taifa letu msamaha na wawajibike kwa kuanza kukaa kimya.

SOMA ZAIDI HAPA:
 

Nyambala

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
4,467
1,164
Mkuu nimeiosoma hiyo makala it's a good one. Kinachonisikitisha zaidi kama ulivyojaribu ku-highlight ni namna hawa wazee wanaposhindwa kueleza kinagaubaga chanzo cha matatizo haya. And no one seem to be close into taking responsibility kwa yanayotokea. Kiukweli hawa wazee nao ni sehemu ya janga. Nadhani imefika muda sasa wa aidha tukae kimya au tuchukue hatua.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,339
38,982
Mkuu nimeiosoma hiyo makala it's a good one. Kinachonisikitisha zaidi kama ulivyojaribu ku-highlight ni namna hawa wazee wanaposhindwa kueleza kinagaubaga chanzo cha matatizo haya. And no one seem to be close into taking responsibility kwa yanayotokea. Kiukweli hawa wazee nao ni sehemu ya janga. Nadhani imefika muda sasa wa aidha tukae kimya au tuchukue hatua.

Nitakupa mfano - wakati wote wa kampeni Igunga na pamoja na tuhuma zote za uvunjwaji wa haki na taratibu mbalimbali Warioba hakusema kitu chochote. Of course yawezekana hakutaka kusema kwa sababu ingeonekana ana influence uchaguzi. Gharama ya ukimya wake tumeona katika mivutano mbalimbali iliyotokea na hata madai ya watu kupoteza maisha. Hakuwa na ujasiri wa kuikemea serikali wala kukinyoshea kidole chama chake. Baada ya uchaguzi ndio anatoka na kutuambia ati hali ilikuwa mbaya.

Lakini cha kuudhi zaidi ni kuwa yeye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu na ndiye aliyeongoza tume ya kuangalia hali ya corruption nchini. Leo ni nani kati ya wale waliotajwa mle ambaye hana nafasi ya maana au haendelei na shughuli zake kama kawaida. Ripoti ya Warioba ilishangiliwa sana lakini mtu mwenyewe aliyeiagiza naye mwenyewe anasimama akidaiwa kuhusika na ufisadi na hujawahi kumsikia Warioba akizungumzia hilo!
 

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,520
859
huyu mzee ni miongoni mwa viongozi wastaafu wa nchi hii ambao ni wanafiki. ONDOA HISA ZAKO VODACOM AMA JIONDOE UJUMBE WA BODI YA TTCL. wewe ndiye unayeiua TTCL KWA MASLAHI YA VODACOM UKUSHIRIKIANA NA BAADHI YA WATENDAJI WA TTCL , NYIE MGELIKUA CHINA TUNGELIKUWA TUMEISHA WASAHAU.
 

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
279
warioba kazi yake ni kukitetea chama na pia ni mmoja wa watu wenye kundi kwa kulenga uchaguzi wa 2015
 

timbilimu

JF-Expert Member
Sep 2, 2010
4,840
1,490
Ni kweli hawa wazee wanataka kuonyesha mambo yameharibika siku hizi,jambo ambalo siyo kweli. Wao ndiyo walijenga huu mfumo ambao umelipeleka taifa katika maangamizi. Wanapaswa watuombe msamaha,wakubali kwamba nao ni sehemu ya mfumo huu kwasababu wengi wao bado wako katika vikao vya maamuzi ndani ya chama chao. Wakati wakiwa serikalini wameshiriki kutunga na kusimamia sheria kandamizi ambazo leo watawala wanajiona maboss badala ya watumishi. Kumekua na kilio cha muda mrefu kuhusu Tume huru ya uchaguzi,wizi na uchakachuaji wa kura,muda wote huo hawa wazee wamekaa kimya,maana aliyekua ananufaika ni wao na chama chao. Sasa wanaona mambo yamekua mabaya eti wanajidai kutushauri vijana kudumisha amani!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom