Kina nani wanaomtumia mzee akilimali ndani ya yanga ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kina nani wanaomtumia mzee akilimali ndani ya yanga ?

Discussion in 'Sports' started by Innobrown, Jun 20, 2012.

 1. I

  Innobrown Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 36
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  pasua kichwa.JPG

  Hi Mr. Shaffih, JUzi usiku nilikuwa nasikiliza kipindi chenu cha Michezo Sports Extra na Sports Bar, vilivyorushwa kwa wakati mmoja kupitia Clouds Fm na Clouds Tv. Nilisikiliza kipande ambacho kuna Mzee Anayeitwa Akilimali, ambaye hujiita katibu wa Baraza la Wazee Wa Yanga. Sina uhakika na hiyo nafasi kwenye Katiba ya Yanga kama ipo.

  Amekuwa akitumika sana, nashukuiru kwa kulitambuahilo jana. Waandishi mmempa sana airtime ya kutosha huyu Mzee mpaka imekuwa kero. Amekuwa Msemaji Mkuu wa Yanga kinyume na utaratibu. Wakati wachezaji wetu wamempiga refa Mechi ya Yanga na Azam alilumbana na TFF na kuongea mambo ya ajabu.

  Kwenye birthday ya Yanga aliwasifia akina Nchunga na akawageuka baadaye. Jana tu Anasema uchaguzi wa Yanga ukiisha atamfukuza Mwanachama Abedi Falcon uanachama kisa ameweka pingamizi kwa
  wagombea kuhusu uchaguzi. Kwani hajui ni haki ya mwanachama kuweka pingamizi? alisema ana milioni 750 za usajili, azitoe wapi?

  Mzee yule na wenzake wasioitakia Yanga Mema ndio hao wamewaponza wachezaji wetu wa Yanga leo hii wamekosa fursa muhimu ya kutumikia timu ya Taifa kutokana na kuwatumia mechi zetu za mwisho wacheze maigizo ili kumkomoa Nchunga. Kiko Wapi leo? Menyekiti hayupo Yanga na Yanga itaendelea kuwepo. Timu yetu ilipoteza muelekeo mwishoni mwa ligi kwa hujuma za hao wazee dhidi ya Uongozi halali.

  Leo wachezaji wanasajiliwa na watu binafsi kwa gharama kubwa, kwa akili ya kawaida wanayanga wanachekelea tu bila kutafakari. Mchezaji anasajiliwa kwa Milioni 30 na Mshahara M 1 kwa chanzo gani cha mapato klabuni? hao wanaowatumia akina Akilimali wakigombana na viongozi halali si ndio wanagoma kutoa mishahara, na kupigwa zile tano?

  Tuna safari ndefu Kaka. Nahitimisha na kusema yule Mzeee alikuwa anatumika tangu mwanzo wa mgogoro wa Yanga, na ameendelea kuwa Msemaji Mkuu, Sekretarieti ya Yanga inamuchia, Nyie waandishi wa Michezo mnampa nafasi bila sababu. Ni bora mmemgundua. Mimi ni Mshabiki wa Yanga wa Kawaida, huyo Mzee hana Mamlaka ya kunivua ushabiki ndio maana nimefunguka.

  Mr. Faraja Emmanuel Mkazi wa Kurasini.

  0717 079727

  :sad:
   
 2. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Huyu Mzee kwakweli ana matatizo lkn Shaffih Dauda na yeye ana matatizo makubwa.
   
 3. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #3
  Jun 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Mnashangaa nn? Mbona hata shafi anatumiwa na rage!
   
Loading...