'Kina mama wengi Moshi wana saratani ya matiti';SIO KITOCHI KWELI!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Kina mama wengi Moshi wana saratani ya matiti';SIO KITOCHI KWELI!!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Feb 22, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  'Kina mama wengi Moshi wana saratani ya matiti'James Lanka, Moshi

  MKOA wa Kilimanjaro umeelezwa kuwa miongoni mwa mikoa yenye kinamama wengi wenye matatizo ya saratani ya matiti na shingo ya uzazi.

  Hayo yalibainika baada ya tafiti mbalimbali kufanywa na chama cha madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) katika mkoa huo.

  Taarifa hiyo, ilitolewa juzi na Mwenyekiti wa MEWATA mkoani Kilimanjaro Dk Zaitun Bokhary kwa Mkuu wa mkoa huo, Monica Mbega wakati wa ufunguzi rasmi wa ofisi ya chama hicho, uliofanyika kwenye hospitali ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

  Alitoa mfano wa utafiti wa matatizo ya aina hiyo unaoendelea katika hospitali ya rufaa ya KCMC kwamba kati ya mwaka 2008/2009, utafiti umeonyesha kuwa kati ya wanawake 134 wenye uvimbe katika matiti, 74 kati yao walibainika kuwa na saratani ya matiti.

  "Mpaka sasa wananwake wengi wa Mkoa wa Kilimanjaro hawajafanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi, hivyo basi wanawake madaktari wa mkoa huo, wamedhamiria kujenga uwezo wa kuwafikia kinamama wengi zaidi," alifafanua Dk Bokhary.

  Akizungumza katika hafla fupi ya Ufunguzi wa ofisi hiyo, Mwakilishi wa MEWATA kutoka makao makuu ya Chama hicho jijini Dar-es-Salaam, Dk Martha Mkony alisema mafanikio ya MEWATA yamechangiwa kwa kiasi kikubwa na moyo wa kujitolea wa wanachama wake.

  "Takwimu zinaonyesha kuwa daktari mmoja anahudumia takribani wananchi 25,000, lakini pamoja na majukumu makubwa waliyonayo, bado madaktari hawa wanawake wameamua kujitolea zaidi kuwasadia kinamama. vijana na watoto ambao ni tegemeo kubwa sana katika maendeleo ya taifa," alifafanua Dk Mkony.

  Akizunguimza na Mwananchi baada ya ufunguzi huo, mmoja ya wanachama wa MEWATA mkoani hapa, Dk Wahida Shangali, alisema licha ya tawi la MEWATA Mkoa wa Kilimanjaro kundwa mwishoni mwaka jana, tayari wamefanikiwa kupima saratani ya matiti kwa kinamama 87 wa kijiji cha Uru-Shimbwe.

  "Kuwa na ofisi katika hospitali ya Mawenzi, tunatarajia kupata wanachama wengi zaidi kutoka katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro na itatuwia rahisi zaidi kuwafanyia uchunguzi wa saratani ya matiti na shingo ya kizazi ikiwezekana kuwafikia kinamama wote wa Mkoa wa Kilimanjaro," alifafanua Dk Shangali.

  Akizungumza katika ufunguzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega aliwapongeza madaktari wanawake kufungua ofisi ya katika mkoa huo.

  Alitoa wito kwa wananchi na taasisi mbalimbali kuiunga mkono MEWATA wa hali na mali na bosi huyo wa mkoa alichangia Sh 500,000. Mkoa wa Kilimanjaro ni mkoa wa kwanza kuwa na Tawi la MEWATA kati ya mikoa yote 26 ya Tanzania kuacha Jiji la Dar es Salaam.
   
 2. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,986
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Sio "KITOCHI aka MBEGE" kama unavyodai bali mimi nadhani ina uhusiano na madawa ya kupulizia kahawa...
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  ahsante sana
  kuanzia leo nakupa DK ya heshima ya JF FRM NOW

  DK T..........BARIIIDIIIII
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,231
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Weye unatafuta ugomvi na watu hapa weye.

  Lakini kama ni kweli kwamba akina mama wengi toka Kilimanjaro wanaugua Kansa, ni ukweli kuwa baadhi ya magonjwa hujikita zaidi maeneo fulani fulani ya nchi kutokana na factors kama occupational activities, altitude, weather etc.
  Sidhani kama ni Mbege, aka kitochi!
  Mbona kwenu kuna Chimpumu mingi sana, kwanini watu hawaugui TB?
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  yaaaalllaaah yamekuwa hayo
  ngoja niede kwa jukwaa la wakubwa!!!kumradhi wana vitochi
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,141
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Inawezekana kabisa kuwa hivyo kwa sababu madawa mengi ya kilimo ambayo tumekuwa tukiyatumia huwa kwanza hatutafiti kujua athari zake za muda mfupi na mrefu na pengine remedy zake hivyo inawezekana kabisa mkuu.
   
 7. k

  kishumundu New Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 4, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ENHE!!!
  Hivi yawezekana kweli Niliwahi kuelezwa kuwa hapo zamani za kale,Waliishi nyumba moja na wanyama,km ngombe mbuzi kuku bata nk.Nyumba zenyewe full suit mlango tu ventilation vipi?kama vile haitoshi mzee akifurahi tu ndafu chini. mama mafuta ya ndafu mpaka liamba.Kila wiki lazima mafuta ya ngombe yachemshwe.YANASHAURRRRRRRRRRRIWA? Matunda yenyewe ndizi mbivu na lazima ziliwe na watoto wazee mh!!Kahawa ya kunywa ilikuwa fresh lakini iliyonyunyiziwa sumu na akina mama.Sumu yenyewe haileti SARATANI? Mwisho mapenzi yao yalikuwa saangapi? Baba akitoka kwenye kitochi huyoooo bandani kwake.
   
 8. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 18,355
  Likes Received: 3,132
  Trophy Points: 280
  Habari ilikuwa ni ya muhimu,ila kitochi ni upotoshaji,uungepeleka kule kwene hoja mchanganyiko coz sijui kitochi na siasa wapi na wapi....Maoni yako hayana mshiko na haya reflect great thinking.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...