Kina mama hivi mbona sherehe zetu zinazidi kuongezeka kwa kasi!!!!!kulikoni

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
Lini tutajifunza ku-cut Cost yaani kila kukicha mambo yanazidi kuwa mambo...
Hizi zote ni sherehe zetu kila siku zinaongezeka
sijui mie najifunza ubahiri au?

1.Hinna party:confused2:
2.Bridal shower:confused2:
3.Kitchen party:confused2:
4.Send off party hapa sawa
5.Wedding party hapa sawa
6. Baby shower party:confused2:
7.
8.
9.
10.
 
Ukiona hivyo fungu linaongezeka kila kukicha mama!! loh na kweli siku hizi hadi ukisikia flani ana shughuli unaanza kumkwepa maana zikianza kuongozana kadi za mchango utachoka!!
 
Lini tutajifunza ku-cut Cost yaani kila kukicha mambo yanazidi kuwa mambo...
Hizi zote ni sherehe zetu kila siku zinaongezeka
sijui mie najifunza ubahiri au?

1.Hinna party:confused2:
2.Bridal shower:confused2:
3.Kitchen party:confused2:
4.Send off party hapa sawa
5.Wedding party hapa sawa
6. Baby shower party:confused2:
7.8.
9.
10.

Chai ya maharusi pamoja na wazazi na marafiki wa karibu
 
Mimi nafikiri kilichoongezeka hapo ni bridal shower. heena party iko tokea enzi za mabibi kwa ndugu zetu waislamu.
baby shower ni sanduku la mtoto aka beseni kwa ndugu zetu wa ukanda wa pwani. sema tatizo lilipo sasa ni kwa nini kila shughuli watu tunachangichwa? zamani mambo ya michango yalikuwa hakuna shughuli zilikuwa zinafanywa kifamilia.
 
kwa kweli mambo mengine yanakera sana. utakuta mtu hana uwezo kabisa lakini anang'ang'ania kufanya sherehe kibao na hapo anategemea michango hadi nguo atakazovaa. mimi kwa kweli huwa nasikitika sana na haya masherehe. mtu yupo tayari kukopa mamilioni sababu ya sherehe na wakati mwanae anasoma shule hata haieleweki kisa hana hela. hivi kama usipofanya bridal shower, kitchen party ya bar, nk huolewi? tena mimi namiss sana zile kitchen party za zamani. nakumbuka dada yangu alipokuwa anaolewa siku chache kabla ya harusi mama aliwaita wamama kama 10 hivi, wakakaa chumbani na bibi harusi wanaongea naye. siku hizi tunaongea na mabibi harusi bar.
inabidi tubadilike jamani. nadhani FL1 itabidi tuunganishe nguvu tuanze kususia michango ya masherehe yasiyo na maana. yanatumalizia hela jamani
 
Back
Top Bottom