Kina Konki Masta na Piere ni zao la nguvu ya mitandao!

matumbo

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
7,225
3,944
Siku hizi habari zipo mkononi, watu wanahitaji content za kusoma kila muda, nani wa kuwalisha habari?. Maisha ni magumu watu wanahitaji zaidi habari za kuwapunguzia stress za maisha, binadamu anapenda furaha. Kwa hiyo uwezi kuzuia watu maarufu mitandaoni dizain ya Piere Liquid au Konki Masta sababu mitaa inawaitaji.

Anaesema nchi yetu ina tatizo sababu ya kuwa na kina Piere basi either yupo gizani au anataka kushindana na wakati.

Ukienda nje ya nchi kuna watu walioibuka mitandaoni na kuwa maarufu wakatumia umaarufu wao kutengeneza maisha yao. Tazama binti kama Kylie Jenner leo ni millionea akiwa na miaka 23 tu. Ametokea family ya Kardashians waliopata umaarufu kwa sex tape ya Kim.

Kuna fundi makenika anaitwa Just Sul leo anaishi Dubai baada ya kupata umaarufu wa mitandaoni na alikuwa fundi wa kawaida tu nchini Zambia, akapost video akitumia lafudhi ya kihindi sasa hivi ana hela chafu.

Salt bae mgahawa wake unakadiliwa kufikia thamani ya 1.5 billion. Kina Messi wanafunga safari wakatafune nyama aliyochoma.
Point yangu ni kwamba hatuwezi kuzuia watu maarufu mitandaoni, hila tunaweza kuwasaidia wakatengeneza maisha mazuri kwao na kwa jamii zetu kupitia umaarufu wao.
 
Back
Top Bottom