Kina Kikwete wakutana na vurugu Ivory Coast | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kina Kikwete wakutana na vurugu Ivory Coast

Discussion in 'International Forum' started by Rutashubanyuma, Feb 24, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Kina Kikwete wakutana na vurugu Ivory Coast


  Na Mwandishi Maalumu

  WAKATI vurugu zililipuka juzi mitaani nchini Ivory Coast kushinikiza kiongozi aliyeng'ang'ania madarakani, Bw. Laurent Gbagbo aachie ngazi, Rais Jakaya Kikwete na
  viongozi wenzake wa Afrika wanaotafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa katika nchi ya Afrika Magharibi ya Ivory Coast juzi walikutana kwa zaidi ya saa tatu na mmoja wa mahasimu hao waliojitangaza marais wa nchi hiyo.

  Katika jiji la Abidjan, wafuasi wa Bw. Alassane Ouattara aliyetangazwa na Tume ya Uchaguzi kama mshindi waliingia mitaani kupinga mpinzani wake, kitendo kilichosababisha vifo vya askari watatu.

  Wanajeshi wanaomuunga mkono Bw. Gbagbo walisema wamechokozwa kwa kuwa wafuasi wa Bw. Ouattara walikuwa na silaha, hivyo tangu asubuhi kulikuwa na kurushiana risasi na wananchi waliojazana mitaani.

  Rais Kikwete na viongozi hao wa nchi za Mauritania, Chad na Afrika Kusini walikutana na kufanya mazungumzo na Bw. Gbagbo, mmoja wa wanasiasa ambao wamejitangaza kuwa Rais wa Ivory Coast kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Novemba 28, mwaka jana.

  Kwa muda mwingi wa mkutano huo katika Ikulu ya Ivory Coast mjini Abidjan, viongozi hao walimsikiliza Bw. Gbagbo na kumuuliza maswali katika hatua hiyo ya kwanza ya kazi ya ujumbe wa viongozi hao ambao ni kuwasililiza na kuwauliza maswali wadau wote katika mzozo huo, ambao umeiacha Ivory Coast ikiwa na marais wawili, serikali mbili na uwezekano mkubwa kuwapo makundi mawili ya watu wenye silaha na waliko tayari kuzitumia kuwania madaraka ya kuongoza nchi hiyo.

  Katika mkutano huo, Bw. Gbagbo alidai kuwa yeye ndiye Rais halali wa Ivory Coast kwa sababu alishinda raundi ya pili ya upigaji kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana nchini humo.

  Viongozi hao wako Ivory Coast kutekeleza azimio la Umoja wa Afrika (AU) ambao katika Mkutano wa Wakuu wa nchi za AU mwezi uliopita mjini Addis Ababa, Ethiopia, uliteua kundi la nchi sita za Afrika chini ya uenyekiti wa nchi ya Mauritania kutafuta suluhisho la amani katika Ivory Coast.

  Nchi zinazounda kundi hilo chini ya uenyekiti wa Mauritania ni Tanzania, Afrika Kusini, Chad, Burkina Faso, Equatorial Guinea ambayo ndiyo mwenyekiti wa sasa wa AU pamoja na Nigeria ambayo ndiyo Mwenyekiti wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

  Nchi hizo zilifanya kikao cha kwanza Jumapili ya wiki hii mjini Nouakchott, Mauritania kabla ya kusafiri kwa kuja mjini Abidjan kukutana na pande zote zinazovutana katika mzozo huo wa kisiasa wa nchi hiyo ya Ivory Coast.

  Kutwa nzima ya jana, viongozi hao walikuwa wamepanga kukutana na makundi ya watu na taasisi mbalimbali za wadau wa suala hilo la Ivory Coast.

  Miongoni mwa watakaokutana na marais hao leo ni pamoja na Bw. Alassane Quattara, ambaye kama alivyo Gbagbo, amejitangaza kuwa Rais wa Ivory Coast kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu huo wa mwaka jana na pia naye ameunda serikali yake.

  Makundi mengine yanayokutana na viongozi hao leo ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Ivory Coast, Bw. Choi; wajumbe wa Baraza la Katiba la Ivory Coast, wajumbe wa Jeshi la Ivory Coast, wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast kwa upande wa Bw. Gbagbo, Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Serikali ya Bw. Quattara, na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast kwa upande wa Bw. Quattara.

  Katika raundi ya pili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimtangaza Bw. Quattara kuwa mshindi.
  Lakini Baraza la Katiba ya nchi hiyo lilibadilisha matokeo kwa kutangaza Gbagbo kuwa mshindi baada ya kufuta matokeo ya kura katika majimbo saba ya wilaya 13 za eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ambako ndiyo ngome ya Bw. Quattara.

  Hatua hiyo ya Baraza la Katiba ilimpunguzia Bw. Quattara kura 600,000, sawa na asilimia 12 ya kura zote zilizopigwa.

  [​IMG]


  2 Maoni:

  [​IMG]
  Anonymous said... Hivi Jakaya anafikiria nini? Kwake hali ni mbaya Ivory Coast anafuata nini?
  February 23, 2011 11:43 PM [​IMG] [​IMG]
  Anonymous said... anatimiza ile kauli ya kujenga kwa mwenzio wakati kwako kunabomoka, aibu tupu kikwete na serikali yako ya kikomedy hv ndounaongoza nchi au unaigiza unahata haya kumetokea janga la mabomu tuna msiba unang'ng'na kwenda huko ilihali migogoro huku inakuandama why usimtume hata makamu wako ili tuamini unatupenda japo kidogo sjawahi kuona baba anawaachia msiba wanae afu yeye anakwenda kupatanisha familia za watu
  February 24, 2011 12:24 AM
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  JK aungana na marais watano kutafuta suluhu Ivory Coast Send to a friend Wednesday, 23 February 2011 20:46

  Mwandishi Wetu
  RAIS Jakaya Kikwete na viongozi wengine wa Afrika wanaotafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast ,wamekutana kwa zaidi ya saa tatu na mmoja wa viongozi wawili waliojitangaza urais nchi hiyo.

  Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais ilisema wengine walioungana na Rais Kikwete katika kutafuta suluhisho la mgogoro huo, ni wa nchi za Mauritania, Chad na Afrika Kusini.

  Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wapatanishi hao walikutana na kuzungumza na Laurent Gbagbo, mmoja wa wanasiasa aliyejitangaza kuwa Rais wa Ivory Coast, kufuatia uchaguzi mkuu wa Novemba 18 mwaka jana.

  Katika mkutano huo uliofanyika katika Ikulu ya Ivory Coast mjini Abidjan, viongozi hao walitumia muda mrefu kumsikiliza Gbagbo na baadaye kumuuliza maswali .

  Mazungumzo hayo ni ya hatua kwanza kwa ujumbe wa viongozi hao katika kushughulikia mzozo huo ulioiacha Ivory Coast ikiwa na marais wawili, serikali mbili na uwezekano mkubwa kuwapo kwa makundi mawili ya watu wenye silaha na waliko tayari kuzitumia katika kuuwania madaraka ya kuiongoza nchi hiyo.

  Katika mkutano huo, Gbagbo aliwahakikishia viongozi hao kuwa yeye ndiye rais halali wa Ivory Coast kwa madai kuwa alishinda katika duru ya pili ya upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo.

  Viongozi hao wako Ivory Coast kutekeleza azimio la Umoja wa Afrika (AU) ambao uliteua kundi la nchi sita za Afrika, chini ya uenyekiti wa Mauritania, ili kutafuta suluhisho la amani nchini Ivory Coast.

  Nchi zinazounda kundi hilo ni Tanzania, Afrika Kusini, Chad, Burkina Faso, Equatorial Guinea na Nigeria ambayo ni Mwenyekiti wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS).

  Nchi hizo zilifanya kikao cha kwanza Jumapili ya wiki hii mjini Nouakchott, Mauritania kabla ya wajumbe hawajasafiri kwenda mjini Abidjan kukutana na pande zinazovutana katika mzozo huo.

  Pamoja na kukutana na Gbagbo viongozi hao pia walikutana na Alassane Quattara, ambaye Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast, ilimtangaza kuwa rais halali wa nchi hiyo.

  Quattara ameunda serikali yake kama alivyofanya Gbagbo.

  Makundi mengine yaliyokutana na viongozi hao ni Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika Ivory Coast, wajumbe wa Baraza la Katiba la Ivory Coast, wajumbe wa Jeshi la Ivory Coast, wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast kwa upande wa Gbagbo, Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Serikali ya Quattara, na wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Ivory Coast kwa upande wa Quattara.

  Mikutano mingi inafanyika kwenye Hoteli ya Pullman ambako viongozi wa Afrika,wamefikia.

  Mikutano inayomhusu Quattara itafanyika katika Hoteli ya Golf, mjini Abidjan, ambako kiongozi huyo amejichimbia pamoja na serikali yake.

  Katika raundi ya pili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana, Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimtangaza Quattara kuwa mshindi.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 421,163
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Jk yeye mwenyewe ni mwizi wa kura sasa atamwambia nini Gbagbo??????????????????
   
Loading...