Kina Kaka: Kati ya hivi viwili.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kina Kaka: Kati ya hivi viwili....

Discussion in 'Entertainment' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 20, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 20, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kati ya Hivi viwili, wewe ungekula kipi?

  Swali hili nalipanga, lawahusu kina kaka,
  Nalipanga kwa kutunga, kwa beti za uhakika,
  Ni miye gwiji malenga, wa kijiji nimefika,
  Vitumbua na sambusa, wewe ungekula kipi?

  Ni kisa kimenikuta, miye nikatatizika,
  Siku chache zilopita, Jenifa kanialika,
  Kwa haraka kama ndata, gia nikazichomeka,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  “Karibu mtu wa shamba”, bibiye akatamka,
  Mkono kama kwa kamba, kizingiti nikaruka,
  Sebule yenye kutamba, kapanga ikapangika,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Kaaga kwenda jikoni, na nyuma akageuka,
  Nkajikuta taabani, dada kweli kaumbika,
  Nikanguruma tumboni, na njaa ikanishika,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Moyo ukaenda mbio, akili zikaniruka,
  Nikatafuta pambio, kuituliza mizuka,
  Nikasema leo ndiyo, ujanja umenitoka,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Karudi kajiandaa, kanga moja kafunika,
  Nikabaki kushangaa, ni nini anachopika,
  Nikatamani chang’aa, mifukoni nikashika,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Twende chemba wa kijiji, vitafunwa nimeweka,
  Si vya chai wala uji, nikazidi weweseka,
  Na ushamba wa kijiji, ute ukanidondoka,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Chagua chako kimoja, ukile mpaka kuchoka,
  Dada akatoa hoja, meza akaiandika,
  Nikila hicho kimoja, kingine kitaondoka,
  Vitumbua na sambusa, wewe ungekula kipi?

  Vitumbua ni viwili, sambusa moja kaweka,
  Vyote havina shubili, ni vitamu vya hakika,
  Hanipi vyote viwili, kimoja ametamka,
  Vitumbua na sambusa, wewe ungekula kipi?

  Kwa ufundi wa maneno, hoja nikazitamka,
  Napenda vyote vinono, kwani miye navitaka,
  Kanijibu kwa mguno, kimoja akakishika,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Hamu yote ikatoka, ya njaa iliyoshika,
  Viwili vyote nataka, msimamo kaushika,
  Nikasema naondoka, naenda kwake Jessika,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  Siku chache zimepita, bado nimeghadhibika,
  Alileta ya kuleta, na masharti ya kushika,
  Kama njaa inaita, vyakula vyote nataka,
  Vitumbua na Sambusa, wewe ungekula kipi?

  M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Shamba)
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Jun 21, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kimoja kati ya vile vitumbua viwili!
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 21, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  jibu zuri... Kuhani.... kitakutosha?
   
 4. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #4
  Jun 21, 2008
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kijiji nami nakuja, nnaingia uwanjani
  nakuja na kiunguja, na lahaja za kipwani
  tamaliza yako haja, inokupa mtihani


  ikiwa mpenda chumvi, sambusa itakufaa
  huchapuzwa tangawizi, nyama kusaga murua
  pia pili pili mbuzi, na ndimu ilokolea

  amini takula sana, binti tamwita tena
  ule huku ukipuma, na kutaja lake jina
  ukae ukisimama, kwa raha utazoona

  ikiwa mtu wa sukari, kitumbua ni chaguo
  utakula kwa fahari, tena bila gugumio
  chukua na tahadhari, usije toka umio

  kijiji leo yatosha, haya niliokujuvya
  usikae ukikesha, domo mate kulirovya
  chukua kilichokukosha, si vyema kudovya dovya
   
 5. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #5
  Jun 21, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Kitumbua kizuri kisianguke tu
   
 6. Mswahilina

  Mswahilina Senior Member

  #6
  Jun 21, 2008
  Joined: Apr 7, 2008
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji, mie ningesusa kama wewe maana vyote ninavitaka.
   
 7. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #7
  Jun 21, 2008
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mzee Mwanakijiji, Hii Sambusa ni ile ya Nyama au ya Viazi?
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Jun 21, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  well,.. ina nyamanyama na mafuta mafuta...
   
Loading...