Kina dada wenye tatizo la hemoroid (kutokwa na nyama sehem ya haja kubwa) kuna fursa la sponsorship

Mung Chris

JF-Expert Member
Sep 12, 2017
3,367
3,778
Kuna kina dada ambao wamejikuta wana tatizo la hemoroid (kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa) hivyo kuwa wasiri sana na kutokuwa wawazi ili wapewe msaada.

Miongoni mwao wapo ambao walipatwa na tatizo hilo tu baada ya kujifungua na wengine katika mazingira ya kawaida.

Sasa naendesha kampeni hii ili kuwasaidia, nitawalipia matibabu na wenyewe watachangia kidogo sana ili kuonyesha wana utayari wa kujituma mpaka wapone maana wengine wakisikia unawalipia wanazembea kuhudhuria tiba mwisho wa siku najikuta nimepoteza hela.

Walio na tatizo hili watalipiwa matibabu ambapo nimeshafanya mazungumzo na madaktari bingwa wa kutibu na kuna uhakika wa wenyewe kutibiwa. Nimeingia mkataba na ma daktari na hospitali ambazo watatibiwa.

Mwenye tatizo aje inbox nitamuunganisha na hospitali ambayo nimesaini mkataba atahojiwa na daktari na hivyo kukubaliana lini akatibiwe.

Karibuni. (nisipotoa kidogo kwa ninachopata kwa walio na matatizo Mwenyezi Mungu hata nielewa, lazima nitoe sadaka).

UPDATES:
HADI SAA 5 ASUBUHI LEO HII NILIKUWA NIMESHAPOKEA PM ZA KINA DADA 7 NA WOTE NIMEWAELEKEZA KWA MADAKTARI NA MUDA HUU NIMEPATA UPDATES KWA MADAKTARI KUWA WAMESHAWAPANGIA RATIBA YA TIBA KWA 5 WENGINE NAONA BADO WANATAFUTA VOCHA YA KUWAPIGIA MA DAKTARI. Mwenyezi Mungu awaponye.
 
Kuna kina dada ambao wamejikuta wana tatizo la hemoroid (kutokwa na kinyama sehem ya haja kubwa) hivyo kuwa wasiri sana na kutokuwa wawazi ili wapewe msaada. Miongoni mwao wapo ambao walipatwa na tatizo hilo tu baada ya kujifungua na wengine katika mazingira ya kawaida. Sasa naendesha kampeni hii ili kuwasaidia, nitawalipia matibabu na wenyewe watachangia kidogo sana ili kuonyesha wana utayari wa kujituma mpaka wapone maana wengine wakisikia unawalipia wanazembea kuhudhuria tiba mwisho wa siku najikuta nimepoteza hela.

Walio na tatizo hili watalipiwa matibabu ambapo nimeshafanya mazungumzo na madaktari bingwa wa kutibu na kuna uhakika wa wenyewe kutibiwa. Nimeingia mkataba na ma daktari na hospitali ambazo watatibiwa.

Mwenye tatizo aje inbox nitamuunganisha na hospitali ambayo nimesaini mkataba atahojiwa na daktari na hivyo kukubaliana lini akatibiwe.

Karibuni. (nisipotoa kidogo kwa ninachopata kwa walio na matatizo Mwenyezi Mungu hata nielewa, lazima nitoe sadaka).
Mkuu nikupongeze kwa kuonyesha kujali. Ni kweli wanawake, hasa huku Afrika, kuna wengi wanasumbuliwa na magonjwa ya ambayo hawajui pa kuanzia au huona aibu kwenda hospital kuelezea. Ningekushauri ungeeleza zaidi unawalenga wanawake wa maeneo gani (kwani Bongo ni kubwa) na wao watachangia asilimia ngapi ya matibabu (ili mtu ajipe kama ataweza. Elfu thelathini inaweza kuwa ndogo sana kwako ila kwa mwingine ni kubwa sana).
 
Mung Chris, umefanya jambo jema japo natamani kujua ni kwa nini wanawake tu! Hii issue inawatesa hata wanaume. Lakini pia ni vizuri ukawasaidia wale ambao hawana uwezo wa matibabu.
 
Vipi wanaume wenye kinyama sehemu za haja kubwa unawasaidia na wenyewe?
Hapana kwa wanaume hawana aibu huwa wanaongea wanawake wana aibu sana ni baada ya kuwasikia kama wangapi hivi ambao wanawakatalia waume zao na kusema hawataki kufanya tendo kwa sababu tatizo likichachamaa wanakuwa wanapoteza munkari na hawatamani kabisa.
 
Huwezi kutaka kuwasaidia watu kwa kutumia ID feki
Kama una nia nzuri ungefukua akaunti kwa jina lako,maalum kwa shughuli hii,yaani unataka watu wakwambie siri zao wakati wewe una fake id?
Hayo ni majina yangu, wewe hunijui ndo maana unaongea hivyo. kwani akija inbox si atanifahamu maana namuelekeza.
 
Mung Chris, umefanya jambo jema japo natamani kujua ni kwa nini wanawake tu! Hii issue inawatesa hata wanaume. Lakini pia ni vizuri ukawasaidia wale ambao hawana uwezo wa matibabu.
Ujue mwanamke ana aibu sana kujieleza kuhusu hili gonjwa utakaa naye miaka hata 5 na usijue ila utasikia naumwa ana lala tu na ukiuliza ugonjwa atakwambia mwingine sasa wanaumwa kimya kimya. tiba ya huu gonjwa ni ghali kidogo, acha tuwasaidie kwanza hawa mama zetu maana wanatulea wanatuhudumia. kwa mwanaume mwenye tatizo hili aje inbox ntampa gharama kama nilivyoelezwa.
 
UPDATES:

HADI SAA 5 ASUBUHI LEO HII NILIKUWA NIMESHA POKEA PM ZA KINA DADA 7 NA WOTE NIMEWAELEKEZA KWA MADAKTARI NA MUDA HUU NIMEPATA UPDATES KWA MADAKTARI KUWA WAMESHAWAPANGIA RATIBA YA TIBA KWA 5 WENGINE NAONA BADO WANATAFUTA VOCHA YA KUWAPIGIA MA DAKTARI. Mwenyezi Mungu awaponye.
 
Ujue mwanamke ana aibu sana kujieleza kuhusu hili gonjwa utakaa naye miaka hata 5 na usijue ila utasikia naumwa ana lala tu na ukiuliza ugonjwa atakwambia mwingine sasa wanaumwa kimya kimya. tiba ya huu gonjwa ni ghali kidogo, acha tuwasaidie kwanza hawa mama zetu maana wanatulea wanatuhudumia. kwa mwanaume mwenye tatizo hili aje inbox ntampa gharama kama nilivyoelezwa.
Mungu na akubariki.

Nadhani haitadhuru ukiweka gharama hapa. Kuna wengine hawatakuja kwa sababu ya aibu. Na ikiwezekana hata hiyo hospitali uitaje.

Umenifungua macho lakini " ukiona mama watoto wako hataki dog style inawezekana anaogopa utaona hako kanyama"
 
Kuna kina dada ambao wamejikuta wana tatizo la hemoroid (kutokwa na kinyama sehemu ya haja kubwa) hivyo kuwa wasiri sana na kutokuwa wawazi ili wapewe msaada.

Miongoni mwao wapo ambao walipatwa na tatizo hilo tu baada ya kujifungua na wengine katika mazingira ya kawaida.

Sasa naendesha kampeni hii ili kuwasaidia, nitawalipia matibabu na wenyewe watachangia kidogo sana ili kuonyesha wana utayari wa kujituma mpaka wapone maana wengine wakisikia unawalipia wanazembea kuhudhuria tiba mwisho wa siku najikuta nimepoteza hela.

Walio na tatizo hili watalipiwa matibabu ambapo nimeshafanya mazungumzo na madaktari bingwa wa kutibu na kuna uhakika wa wenyewe kutibiwa. Nimeingia mkataba na ma daktari na hospitali ambazo watatibiwa.

Mwenye tatizo aje inbox nitamuunganisha na hospitali ambayo nimesaini mkataba atahojiwa na daktari na hivyo kukubaliana lini akatibiwe.

Karibuni. (nisipotoa kidogo kwa ninachopata kwa walio na matatizo Mwenyezi Mungu hata nielewa, lazima nitoe sadaka).

UPDATES:

HADI SASA NIMESHA POKEA PM ZA KINA DADA 7 NA WOTE NIMEWAELEKEZA KWA MADAKTARI NA MUDA HUU NIMEPATA UPDATES KWA MADAKTARI KUWA WAMESHAWAPANGIA RATIBA YA TIBA KWA 5 WENGINE NAONA BADO WANATAFUTA VOCHA YA KUWAPIGIA MA DAKTARI. Mwenyezi Mungu awaponye.

How much do you sponsor them? wakikuzidi si mbaya ukishirikiana nasi pengine twaweza kuweka mkono hapo! HONGERA SANA KWA KUWASAIDI DADA NA MAMA ZETU!
 
Mungu na akubariki.

Nadhani haitadhuru ukiweka gharama hapa. Kuna wengine hawatakuja kwa sababu ya aibu. Na ikiwezekana hata hiyo hospitali uitaje.

Umenifungua macho lakini " ukiona mama watoto wako hataki dog style inawezekana anaogopa utaona hako kanyama"
Makubaliano na hospitali tuli burgain bei na mganga mkuu kwa sababu ni msaada nikiweka bei inaweza ikatokea mtu akaenda kule akaanza kuwashutumu kuwa mbona kuna mtu aliweka JF kuwa mnatibu kwa bei hii na kwanini mimi mnanitajia bei hii bila ya kujua ni mkataba, sasa mgonjwa mwenyewe labda ataje hospitali alikopelekwa au kupangiwa maana nikisema watasema labda kwanini unataja tulipo wao wenyewe wakisoma hii reply kila mtu kwa muda wake aseme aliko na alikopangiwa.
 
Hayo ni majina yangu, wewe hunijui ndo maana unaongea hivyo. kwani akija inbox si atanifahamu maana namuelekeza.
Yanaweza kuwa Majina yako lakini bado hayafanyi account yako kuwa verified.

Chukulia Ushauri huo kwa namna chanya Kama una nia ya dhati kusaidia wahanga wa tatizo Hilo.

Kuwa na verified account maalum kwa Jambo Hilo andika post yenye details zako zote muhimu na namna unavyopatikana (anuani na namba za simu ni muhimu).

Ukifanya hivyo utakuwa umesaidia kufikiwa na wenye uhitaji bila hata kufahamu ID zao za humu, hiyo itaimarisha na kuendelea Kulinda faragha za wahusika.

Otherwise hongera kwa Moyo huo wakusaidia wenye uhitaji.
 
How much do you sponsor them? wakikuzidi si mbaya ukishirikiana nasi pengine twaweza kuweka mkono hapo! HONGERA SANA KWA KUWASAIDI DADA NA MAMA ZETU!
Ok kwanza siwezi weka mkataba wa hospitali na mimi maana hatuja kubaliana niweke public, ila niseme tu kwamba tiba za hospitali zinatofautiana maana zingine ni private hata hivyo hatujaenda kwenye hospitali kubwa private maana wao ni ghali sana, tiba ina range kuanzia sh 902,000-1,670,000 kwa mtu mmoja ila kuna hawa wa tiba zingine wenye aina ya dawa kama mnazoona pale foreplan clinic zinaitwa herbal clinic ambao wawili waliomba tusaini mkataba na endapo mtu hata pona tusiwalipe hawa walisema watatibu kwa sh 550,000. sasa bado tuna bargain pamoja na kuwa wanahakikisha kuwa watapona kwa 100%. tutakuwa na mazungumzo tena kesho jioni nikitoka kazini maana bado hatujaafikiana.
 
Sawa, this is good! and on the same note: Nakushauri tu, weka angalizo zuri la uwezo wa hao watu, vifaa na kazalika, Si unajua ndugu wa Tanzania tunavyopenda kubahatisha? Hao wauguzi wetu wasije kukuangusha ndugu! Nilitaka tu kujua average cost sio mkataba, ALL THE BEST!
 
Yanaweza kuwa Majina yako lakini bado hayafanyi account yako kuwa verified.

Chukulia Ushauri huo kwa namna chanya Kama una nia ya dhati kusaidia wahanga wa tatizo Hilo.

Kuwa na verified account maalum kwa Jambo Hilo andika post yenye details zako zote muhimu na namna unavyopatikana (anuani na namba za simu ni muhimu).

Ukifanya hivyo utakuwa umesaidia kufikiwa na wenye uhitaji bila hata kufahamu ID zao za humu, hiyo itaimarisha na kuendelea Kulinda faragha za wahusika.

Otherwise hongera kwa Moyo huo wakusaidia wenye uhitaji.
kwanza sifanyi biashara swala hili ni la muda tu kwakuwa kazini nimelipwa pesa flan hivi nikaona nijitose kwa hili sasa nikiweka contact zangu zote hata itakapoisha muda wake nitakuwa naipigiwa simu na kuwasiliana na mimi huku wakiwa wanafikiri kuwa hili zoezi ni endelevu. walio kuja inbox wanajua namba yangu ya simu maana ni wahusika zaidi, ndio simjibu mtu ambaye sio mhusika maana kuna maswali 6 namuuliza kabla sijamkabidhi kwa dactari amuhoji.
 
Back
Top Bottom