Kimya cha SMZ na kuzuliwa kwa mizigo Kutoka Zanzibar yakiwemo magari yalio rundikana Bandar ya Dar.

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
[h=1][/h]Written by Hassan10 // 01/07/2011 // Habari // No comments

Written by Hassan10 // 01/07/2011 // Habari // No comments
Hivi sasa takribani unaingia mwezi mizigo yote kutoka Zanzibar yakiwemo
magari alfu na kitu imekwama katika Bandar ya Dar-es-laam kisa na
sababu hazijulikani bali ya wafanya Biashara wakiaha kwa ulipaji wa kila
siku storege na bado kuendelea mizigo yao kubaki.
Wafanya biashara wamefika sehemu mbalimbali ili kuliza sababu
zilizosababisha mizigo yao kukwama haliyakuwa wamesha lipa malipo yote
ya ushuru lakini bado mizigo yao ipo na kinachoendelea hivi sasa
nikulipia storege kwa kila siku na kupigwa danedane kutoruhusiwa
kutolewa mizigo hio.
Jee Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshukuwa hatua gani kuwasaidia
Wafanya biashara hao wa Zanzibar? na jee hio ni kukomolewa wafanya
biashara wenye asili ya Zanzibar kupeleka mizigo yao Tanzania Bara?.
Kipindi cha nyuma walikuwa wanasema system ya uchuru wa Bandari Tanzania
Bara umebadilika kwa hio mpaka wapate tarifa ndio waweze kui-release
mizigo yote, lakini chakuchangaza nikuwa tayari watu wengi wamesha lipia
malipo yote na bado still inaingia mwezi tena mizigo ipo na wanaendelea
kulipo storege kwa kila siku.
Kuna wafanya biashara wameshaanza kupiga kelele na kusema biashara zao
zinazidi kushuka samani kutokana na vitu vyao kubakia hapo na wengine
wako tayari kurudisha mizigo yao iliko toka Zanzibar, swali nikuwa jee
hii ni agenda ya kukomolewa wafanya biashara wenye asili ya Zanzibar
wanao bitisha mizigo yao kwa kutumia Bandari ya Zanzibar na kama ni
hivyo Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeshukuwa hatua gani ili
kuwasaidia wafanya biashara wao ambao mizigo yao inazidi kusota ktk
Bandari ya Dar?.
Uchumi wa Zanzibar unategemea sana Bandari lakini uchumi wa Tanzania
Bara una chanal nyingi kuliko Zanzibar, Sasa kama hii ni kukomowana au
kuitia adabu Zanzibar kutokana na kiwango chake kidogo cha uchuru
wabandari, Hii sikuuwa Biashara na Wafanya biashara wa Zanzibar?.
Haiwezekani kiwango cha mishahara Zanzibar na kiwango cha uchumi cha
Wzanzibar kikalingana na Tanzania Bara, hivyo basi kama hii ni adabu kwa
wafanya Biashara wa Zanzibar, kwa hio vile vile ni adabu kwa Serekali
ya SMZ kuanguka kiuchumi kutokana na wafanya biashara wake wa ndani.
kurundikana kwa mizigo ya wafanya biashara kutoka Zanzibar ktk Bandari ya Dar
 
Back
Top Bottom