Kimondo cha Mbozi ni kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
KIMONDO CHA MBOZI
1605687773920.png

Kimondo cha Mbozi ni kimondo ambacho kilianguka kutoka anga-nje karibu na mji wa Vwawa. Kinakadiriwa kuwa na uzito wa takribani tani 16, kilianguka katika kilima cha Mlenje, wilayani Mbozi katika mkoa wa Songwe, Tanzania. Kipindi hicho Songwe ikiwa ni moja ya wilaya ya Mbeya.

Kipo kati ya vimondo vizito 10 vinavyojulikana duniani. Kina urefu wa mita 3.3, upana wa mita 1.63 na kimo cha mita 1.22.

Kina maumbile maalum tofauti na vimondo vingine vinavyopatikana ulimwenguni kwa kuwa hiki ni hasa cha chuma. Chuma ni 90.45%, nikeli 8.69%, sulfuri 0.01% na fosfori 0.11% ya masi yake. Ndani yake vipande vidogo vya silikati vinapatikana.

Wenyeji wa eneo walijua kimondo hiki tangu muda mrefu; kilielezwa kisayansi mara ya kwanza mwaka 1930 na wakati ule hapakuwa na dalili za kasoko; kwahiyo inawezekana ya kwamba ama kilifika kwenye uso wa Dunia kwa pembe butu sana na kuvingirika hadi kukaa au muda wa kugonga uso wa dunia ni mrefu sana hadi dalili zote za kasoko asilia zilipotea tayari kutokana na mmomonyoko.
 
... tani 16 za chuma si haba! Kwanini kisiuzwe serikali ya mkoa ikapata mapato? Kama chuma chakavu mtaani tunauza kg sh. 500 tani 16 x 1000 x 500 = 8,000,000/= hiyo.
 
... tani 16 za chuma si haba! Kwanini kisiuzwe serikali ya mkoa ikapata mapato? Kama chuma chakavu mtaani tunauza kg sh. 500 tani 16 x 1000 x 500 = 8,000,000/= hiyo.
Sasa hiyo milioni nane itafanya shughuli gani kubwa itakaonekana kizazi hadi kizazi? Halafu hiyo milioni 8 inaweza kupatikana kwa wataliii wanaoingia pale kwa mwaka mmoja, hebu ongeza bei
 
... tani 16 za chuma si haba! Kwanini kisiuzwe serikali ya mkoa ikapata mapato? Kama chuma chakavu mtaani tunauza kg sh. 500 tani 16 x 1000 x 500 = 8,000,000/= hiyo.
Huenda wanapata zaidi kutokana na utalii.
 
Back
Top Bottom