Kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba kuna madhara yoyote?

Darlis2016

Member
Nov 3, 2016
81
25
Habari wakuu, naomba kuelemishwa. Kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba? Mke wangu umri wake wa mimba ni wiki 37+6 na kimo cha mimba ni 40. Na hii ni mimba ya pili kwake. Naomba msaada wenu wataalamu.
 
Habari za leo wakuu,

Naomba msaada kueleweshwa, je kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba? Mke wangu ni mjamzito na leo kapima umri mimba ni week 37+6 na kimo cha mimba ni 40.

Hii kwake ni mimba ya pili namaanisha tunatarajia mtoto wa pili. Je, kuna madhara kwenye huo utofauti. Tafadhali naomba msaada wenu kwenye hili.

Asante sana.
 
Kwahiyo difference hakuna shida. kimo cha mimba kinaruhusiwa kutofautiana kwa wiki mbili (plus or minus 2weeks) na hiyo 37+6 is almost 38 which is normal, endelea kulea mimba.
 
Mmejisahahu tu ila hilo swali mlitakiwa muulize hapo hapo mlipopewa majibu
Ni kweli ,maana Mimi nipo safari mbali kidogo na wife lakini wife kauliza akaambiwa kwamba huenda ana mapacha hivo akapige ultra sound ,yaani ni kama huyo nesi kamfanya apanik.
 
Hakuna kiashirio cha tatizo kama tofauti ya umri wa mimba na kimo cha mimba ni chini ya 5.

Umri wa mimba huhesabiwa kwa wiki na siku. Kimo cha mimba hupimwa kwa sentimeta za urefu/kimo.

Kukiwa na tofauti zaidi ya 5 inaonyesha aidha mtoto tumboni ni mkubwa au zaidi ya mmoja au mtoto ni mdogo kuliko umri wa mimba.

Mfano GA (umri wa mimba) 30 FH (kimo cha mimba) 18 hapa mtoto mdogo /hakui vizuri tumboni

GA 30 FH 38 mtoto ni mkubwa au kuna maji mengi tumboni au mtoto zaidi ya mmoja
 
Wilbert1974,
Asante mkuu, kwahiyo Mimi kulingana na suala langu wife anaangukia kwenye kipengele cha pili GA 30 FH 38 ina maana yeye haijazidi 5 maana ni GA 37+6 (38) na FH ni 40?? Samahani naomba tena ufafanuzi kidogo mkuu.
 
Asante mkuu, kwahiyo Mimi kulingana na suala langu wife anaangukia kwenye kipengele cha pili GA 30 FH 38 ina maana yeye haijazidi 5 maana ni GA 37+6 (38) na FH ni 40?? Samahani naomba tena ufafanuzi kidogo mkuu.
Tuko pamoja kiongozi
40-38=2 hapo ni ukuaji na maendeleo ya kawaida kwa ujauzito.

Angalizo ulinganifu wa FH & GH unaweza usiwe sahihi kwa baadhi ya jamii...
Wafupi au warefu sana.
 
Tuko pamoja kiongozi
40-38=2 hapo ni ukuaji na maendeleo ya kawaida kwa ujauzito.

Angalizo ulinganifu wa FH & GH unaweza usiwe sahihi kwa baadhi ya jamii...
Wafupi au warefu sana.
Asante sana mkuu, nimekuelewa vizuri sana,

Kitu ambacho kingine ameambiwa ni kwamba mtoto anatakiwa awe ameshashuka kwenye nyonga lakini hadi sasa hajashuka kwenye nyonga ,je na hili lipo sawa mkuu?
 
Ilinitokea,nilipomuuliza Dr.alisema nina maji Mengi au nimebeba mimba ya mapacha. Mwisho nilijifungua mapacha.
 
Habari wakuu ,
Naomba kuelemishwa , kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba?
Mke wangu umri wake wa mimba ni wiki 37+6 na kimo cha mimba ni 40.
Na hii ni mimba ya pili kwake.
Naomba msaada wenu wataalamu.
Huyo mtaalamu aliyewapa majibu alitoa comment gani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom