Kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba kuna madhara yoyote?

Darlis2016

Member
Joined
Nov 3, 2016
Messages
73
Points
95

Darlis2016

Member
Joined Nov 3, 2016
73 95
Habari wakuu, naomba kuelemishwa. Kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba? Mke wangu umri wake wa mimba ni wiki 37+6 na kimo cha mimba ni 40. Na hii ni mimba ya pili kwake. Naomba msaada wenu wataalamu.
 

Darlis2016

Member
Joined
Nov 3, 2016
Messages
73
Points
95

Darlis2016

Member
Joined Nov 3, 2016
73 95
Habari za leo wakuu,

Naomba msaada kueleweshwa, je kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba? Mke wangu ni mjamzito na leo kapima umri mimba ni week 37+6 na kimo cha mimba ni 40.

Hii kwake ni mimba ya pili namaanisha tunatarajia mtoto wa pili. Je, kuna madhara kwenye huo utofauti. Tafadhali naomba msaada wenu kwenye hili.

Asante sana.
 

Wilbert1974

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Messages
1,627
Points
1,225

Wilbert1974

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2011
1,627 1,225
Hakuna kiashirio cha tatizo kama tofauti ya umri wa mimba na kimo cha mimba ni chini ya 5.

Umri wa mimba huhesabiwa kwa wiki na siku. Kimo cha mimba hupimwa kwa sentimeta za urefu/kimo.

Kukiwa na tofauti zaidi ya 5 inaonyesha aidha mtoto tumboni ni mkubwa au zaidi ya mmoja au mtoto ni mdogo kuliko umri wa mimba.

Mfano GA (umri wa mimba) 30 FH (kimo cha mimba) 18 hapa mtoto mdogo /hakui vizuri tumboni

GA 30 FH 38 mtoto ni mkubwa au kuna maji mengi tumboni au mtoto zaidi ya mmoja
 

Wilbert1974

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2011
Messages
1,627
Points
1,225

Wilbert1974

JF-Expert Member
Joined Feb 10, 2011
1,627 1,225
Asante mkuu, kwahiyo Mimi kulingana na suala langu wife anaangukia kwenye kipengele cha pili GA 30 FH 38 ina maana yeye haijazidi 5 maana ni GA 37+6 (38) na FH ni 40?? Samahani naomba tena ufafanuzi kidogo mkuu.
Tuko pamoja kiongozi
40-38=2 hapo ni ukuaji na maendeleo ya kawaida kwa ujauzito.

Angalizo ulinganifu wa FH & GH unaweza usiwe sahihi kwa baadhi ya jamii...
Wafupi au warefu sana.
 

Darlis2016

Member
Joined
Nov 3, 2016
Messages
73
Points
95

Darlis2016

Member
Joined Nov 3, 2016
73 95
Tuko pamoja kiongozi
40-38=2 hapo ni ukuaji na maendeleo ya kawaida kwa ujauzito.

Angalizo ulinganifu wa FH & GH unaweza usiwe sahihi kwa baadhi ya jamii...
Wafupi au warefu sana.
Asante sana mkuu, nimekuelewa vizuri sana,

Kitu ambacho kingine ameambiwa ni kwamba mtoto anatakiwa awe ameshashuka kwenye nyonga lakini hadi sasa hajashuka kwenye nyonga ,je na hili lipo sawa mkuu?
 

Chrisvern

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Messages
2,172
Points
2,000

Chrisvern

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2011
2,172 2,000
Habari wakuu ,
Naomba kuelemishwa , kuna madhara yoyote kimo cha mimba kuwa tofauti na umri wa mimba?
Mke wangu umri wake wa mimba ni wiki 37+6 na kimo cha mimba ni 40.
Na hii ni mimba ya pili kwake.
Naomba msaada wenu wataalamu.
Huyo mtaalamu aliyewapa majibu alitoa comment gani?
 

Forum statistics

Threads 1,366,664
Members 521,539
Posts 33,375,024
Top