Kimeumana Vanilla Njombe: Ni utapeli mtupu

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
15,369
2,000
Niliposikia tangazo kipinda cha PB asubuhi maeneo ya Korogwe naitafuta Bucha nikajichekea kimoyomoyo nikasema hivi kumbe wa TZ ni vilaza kiasi hiki? Yaani upewe shamba, miche, wakulimie wao we uje kuuza tu? halafu upate booonge la faida.

Haiingii akilini kwa mtu kwa kujua kusoma na kuandika tu halafu hana tamaa
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
6,209
2,000
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Soko la Hisa sio Guarantee ya Kupigwa..., Na huko maumivu yaweza kuwa maradufu...

Cha Muhimu do your homework and use your common sense..., Na hapo sio guanrantee ya kutokupoteza sababu unaweza ukaliwa legally (after all there are risks involved)

Moral of my Statement; Do Your Homework
 
CHECHEMLENDA

Senior Member
Sep 19, 2021
173
250
Mkuu ni kweli kilo moja 1M lkn shida ipo kwenye kukidhi izo grade za 1M maana Vanilla sio poa kuanzia kwenye pollination inaitaji artificial pia ikipata stress tuu inapelekea flowering abortion pia kwenye swala la kuvuna na utunzaji kwa sio rahisi maana ikipungua tuu grade sio rahisi lkn ukiweka jitiada kila kitu kinawezekana
Mhh. Hizi stress zipo mpaka kwenye vanilla!! Hata abortion!! Sasa mtawauwa watu
 
CHIEF MASALAKULANGWA

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
593
500
W
Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

📍Serikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

📍Kazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.
Wapi kwenye maelezo ya DC wa Njombe anaposema mambo ya UTAPELI au ni maneno yako unamlisha huyo DC kutokana na mentelity yako towards hao wawekezaji kwenye Vanilla. Pamoja na yote, viongozi kama hawa hawawasaidii watu kwani wana REACT baada ya kusikia au kusoma maneno kama ya akina Baraka 21 na wenzao kwenye mitandao. Viongozi hawa wanapaswa kuwa PRO - ACTIVE kama kweli ni wawajibikaji!
 
Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,277

Kama umewekeza huko nenda kwa RPC, hayo sio maneno yangu ni maneno ya DC.

Pole mkuu kwa yote. Kagera na Hai wanalima Vanilla miaka yote ila sio milioni moja kwa kilo.
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,734
2,000
Lawama zote kwa ITV!!! ITV kuna mkono wao kwenye hili saga maana ilifika wakati nikawa najiuliza kama "kijiji cha vanilla" ni habari au tangazo la biashara, kuna mtu hapa jf alikoleza zaidi kwa kusema eti Bi. Mhaville naye ana hisa mle!
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612
2,000
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Hata huko unakosema watu "wanapigwa" tu....kwa maoni yangu labda tuseme kuna nafuu tu. My point is wasiende au kuingia kichwakichwa kwa kuwa tu kuna usajili. Uwekezaji una risks nyingi sana. Tizama thamani ya hisa za voda, crdb, etc (linganisha na kipindi cha IPO zao). Hatari sana.
 
CHIEF MASALAKULANGWA

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
593
500
Usikubali kuwekeza popote kama fursa inayotangazwa kampuni haijasajiliwa soko la hisa

Waulize tu mumesajiliwa soko la hisa ili niwekeze hisa zangu?

Wengi wametapeliwa mara sijui wekeza kwenye kuku,vanilla sijui shamba umwaligiliaji rufiji nk usiwekeze kwenye kampuni inayojitangaza tu isiyokuwa soko la hisa .ukisikia wekeza shilingi hizi utavuna mara kumi uliza tu mumesajiliwa soko la hisa? wakisema hapana achana nao
Hili nalo siyo SAHIHI! Huu ni upotoshaji mwingine humu JF! Kampuni ikitangaza kuuza HISA ni kwamba iko tayari DSE, lakini suala la kukaribisha wawekezaji aidha kwenye kilimo cha vanilla au mahindi au chochote, ni suala la kibiashara zaidi na wewe unayetaka kuingia na kuwekeza humo, fanya utafiti wako na ujiridhishe vizuri ndipo ufanya UAMUZI bila kusikiliza wataalam wa kwenye keyboard humu JF yaani akili za kuambiwa ongeza na zako!
 
SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,612
2,000
Lwama zote kwa ITV!!! ITV kuna mkono wao kwenye hili saga maana ilifika wakati nikwa najiuliza kama "kijiji cha vanilla" ni habari au tangazo la biashara, kuna mtu hapa jf alikoleza zaidi kwa kusema eti Bi. Mhaville naye ana hisa mle!
Ingawa wazo (concept) kwa kweli ni zuri sana. Linafaa kuigwa au kukuzwa kwa scale kubwa zaidi na kwa mazao mengine. Serikali iangalie namna ya kuwezesha wazo hilo na namna ya kuhakikisha usalama wa mitaji upo vizuri/risk mitigation.
 
Opportunity Cost

JF-Expert Member
Dec 10, 2020
9,055
2,000
Ujumbe wa DC Njombe kissagwakisakasongwa kuhusu VanillaNjombe

📍Serikali bado inafanyia kazi maswali mengi yaliyopo katika jamii kutokana na matangazo kwamba Vanilla inalipa na bei ya manunuzi ya Vanilla kwa kilo zinazotajwa kuwa ni kubwa sana. Naomba wananchi tuwe watulivu wakati Serikali Inaendelea kufuatilia jambo hii kwa Kina. Aidha kwa wale ambao tayari wamewekeza waweze kufika kwa RPC wa Mkoa wa Njombe kama ambayo Mheshimiwa RC ameagiza ili kujihakiki majina yao.

Nitoe wito kwa wananchi ambao wanakusudia kuwekeza kusubiri kwanza kuendelea na uwekezaji huu uliopo hadi pale serikali itakapojiridhisha ili kuepusha migogoro au sintofahamu ya aina yoyote inayoweza kujitokeza kwa wananchi.

📍Kazi inaendelea
Picha zinaelezea ziara ya leo nilipoongozana na Kamati ya Ulinzi na Usalama kwenda kufanya ukaguzi wa eneo maarufu lililowekezwa Vanilla wilayani Njombe.
Tzn ukianzisha fursa serikali inajifanya kuja , muwekezaji kawahakikishia watu soko na kununua Mazao afu serikali inaleta upuuzi wake,je yenyewe imewasaidiaje hao Wakulima? Stupid
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,734
2,000
Wewe ni mgeni labda vanilla inalipa Ina pesa ndefu hata kabla ya ujio wa hamasa hii.
Uliza kagera.
Madagascar mashamba ya vanilla yanalindwa na bunduki ndo ujue pesa ipo.
Ilikuwa ni jukumu la serikali kuwaunganisha wakulima na masoko.
Karagwe wameamua kuachana nayo kwasbabu waganda wanakuja na AK 47 na mabomu ya kurusha kwa mkono ili kuiba vanilla shambani kwa mkulima....ukiona mnyambo kanyoosha mikono (naturally jamii ya hawa watu huwa hawashindwi) ujue vanilla siyo!
 
CHIEF MASALAKULANGWA

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
593
500
N
Kama umewekeza huko nenda kwa RPC, hayo sio maneno yangu ni maneno ya DC.

Pole mkuu kwa yote. Kagera na Hai wanalima Vanilla miaka yote ila sio milioni moja kwa kilo.
Ni milioni ngapi kwa kilo!? Mbona hamsemi hiyo bei au hamuijui mnabaki kuandika HEARSAY TU!? RPC alisema watu waliowekeza waende WAKAHAKIKI narudia tena alisema waende WAKAHAKIKI mashamba au vitalu vyao PERIOD! Hakusema anything negative on uwekezaji huo ambao unatokana na watu binafsi walioikubali hiyo FURSA!

Kama wewe unaona siyo fursa au ni kupigwa basi andikaaaaa tu na sisi tuliowekeza wenye all LEGAL CONTRACTS tunaendelea na kutafuta fursa nyingine kama hizo. Halafu nadhani hapa tatizo jingine ni hako kamtaji ka kuanzia 2mi/= na kuendelea! Siyo pesa ndogo wala siyo pesa nyingi ni SUALA LA MTAZAMO NA UWEZO NA UTAYARI WA KUWEKEZA NA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO period!
 
ikigijo

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
1,443
2,000
Hapana Mkuu;
Kilo moja ni Tshs 850,000/= ?? sio Laki moja.!!!

Wewe unaleta Utani!
Ingia google search andika Vanila Industries Tanzania...
Utapata Kiwanda cha Vanila ambacho kipo Moshi,Wasiliana nao Uulize bei Utapata majibu,
Kinaitwa Natural extractive industries, just Google...
Nime google Vanila Industries Tanzania.
Ulixa wakulima pia
 
Ndebile

JF-Expert Member
Sep 14, 2011
6,734
2,000
Soko la Hisa sio Guarantee ya Kupigwa..., Na huko maumivu yaweza kuwa maradufu...

Cha Muhimu do your homework and use your common sense..., Na hapo sio guanrantee ya kutokupoteza sababu unaweza ukaliwa legally (after all there are risks involved)

Moral of my Statement; Do Your Homework
Yale ya kwenye Movie ya : The Wolf of Wall Street
 
CHIEF MASALAKULANGWA

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
593
500
Chini ya ccm utapeli unazidi kutamalaki
Na ndani CHADEMA au CHAGGA DEVELOPMENT ............ ujambazi unazidi kutamalaki tangu kuwaibia Wabunge vile vimilioni vyao kila mwezi hadi kutaka kutumia VILIPUZI kwa nia na lengo la kudhuru wananchi na viongozi wao. Bravo Gaidi Mwenyekigoda!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom