Kimeumana: January, Nape na Muhongo; long game yenu haitawasaidia. Legacy ya Magufuli ni kama mbuyu ndani ya chama mlichopo

Kwa hiyo madawa ya kulevya yalizuiwa na Mwendazake? Kweli mnadanganywa Sana.

Drug lords wakubwa Shkuba ma Lwitiko walikamatwa mwaka 2014 kwa surveillance ya FBI/ CIA. Anayeamini kuwa Makonda aliwakamata wafanya biashara wa cocaine/ heroine siyo mwelewa. Makoknda alikamata drug pushers na 'punda'. Wengine aliwadhalilisha ili wampe pesa
Wewe usiyedanganywa,nieleweshe.kwa hapa tanzania mateja kwenye stand za mabasi walipungua au kuisha muda gani?
Naomba kwanza vua miwani ya mbao ili tujadili hoja tukiwa tunaona.
 
Report ya CAG imeonesha ufisadi mkubwa kwenye uongozi wa dicteta
Weka hapa report ya CAG yeyote ambayo haikuonyesha ubadhilifu serikalini?
Ndo maaana mimi nasema ni heri kuongozwa na serikali yenye ubadhilifu lakini inaleta maendeleo kwa wananchi.
kuliko serikali za watakatifu wasiowafanyia wananchi chochote,na huu ndo msimamo wangu.
Kama serikali zote nne tumeongozwa na wasiowabadhilifu lakini watoto wanakalia matofari darasani, kipindupindu kila kona
n.k alafu mnakataa katakata hamtaki kuitwa wanyonge,huku mnaishi kwenye nyumba za tembe????
 
Wewe usiyedanganywa,nieleweshe.kwa hapa tanzania mateja kwenye stand za mabasi walipungua au kuisha muda gani?
Naomba kwanza vua miwani ya mbao ili tujadili hoja tukiwa tunaona.
Mateja bado wapo vituoni, labda wewe unatumia usafiri binafsi. Njoo Mwenge uwaone
 
Yale mema aliyofanya alitimiza wajibu wake sawa na kila mtu anavotimiza wajibu wake. Yale ya ovyo ndio tutamkumbuka nayo kama rais wa ovyo kabisa kutokea tangu tupate uhuru.
Tukimtoa mama ambaye ndo kaanza kazi... Pombe ndiye Rais wa ajabu sana tuliyewahi kumpata. Rais wa hovyo aliyetumia media na wapambe kuaminisha wanyonge kwamba alikuwa mwema kama malaika....

Ila Mungu yu mwema na husikiliza maombi kwa namna anavyoona inafaa. Ningekuwa mimi ndio Mungu, Huyu fashisti ningemwacha ashuhudie yanayoendelea akiwa kalala kitandani akiwa hana mamlaka ya kuamuru nani auliwe kwakuwa tu kampinga ..
 
Back
Top Bottom