Kimeumana: January, Nape na Muhongo; long game yenu haitawasaidia. Legacy ya Magufuli ni kama mbuyu ndani ya chama mlichopo

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
10,074
2,000
January, Nape, Muhongo na wengine wa aina yenu fahamuni kwamba legacy ya Magufuli ndani ya chama imewafunika sana na hamtaweza kuizidi. Hamtaweza kuwashawishi wenzenu walio wengi kwamba Legacy ya Magufuli sio "special" tofauti na legacies za wenzake waliomtangulia.

Juzi na jana mmeongea kwa kuzunguka, uchungu na tahadahari sana katika mkutano wa bunge unaoendelea. Watoto wa mjini kama wanasema mmetanguliza mpira mkutane nao kwa mbele "long game" mkitaka kuwaaminisha wabunge wengine kwamba hizi ni zama za kitabu kipya na hakuna haja ya kung'ang'ana na yaliyopita. Haikuchukua muda mrefu mliyapata majibu yenu kutoka kwa Gwajima leo.

Ukiachana na Muhongo hahiitaji wachambuzi wa wabobevu mahiri wa siasa kufahamu nyinyi wengine ambao wakati fulani mlidukuliwa mkimsengenya mwendazake mnafanya hivyo kwa sababu mna malengo makubwa zaidi ya ubunge katika uongozi wa nchi siku za mbeleni.

Zaidi sana mlikuwa hamkubalini kwa kiasi kikubwa na sera za serikali iliyopita lakini mnafahamu jinsi gani serikali hiyo ilivyojizolea kundi kubwa la wananchi waliyoimani kupitiliza kiwango cha kuweza kuitwa 'cult'. Hivyo mnajaribu kuchanga karata zenu vizuri kwenda na makundi yote ndani ya chama.

Tanzania ya leo sio ile ya mwaka 2015 kurudi nyuma.Wakati fulani iliitwa ni Tanzania ya Magufuli, huenda sasa sio Tanzania ya Magufuli tena kwa sababu hayupo lakini hii ni Tanzania mpya na Magufuli 'footprints' au alama zake alizoacha ziko kila mahali.

Haitakuwa rahisi kwenu kufikia madaraka makubwa zaidi ya uwaziri kama mtafanikiwa kuendelea kuwa wabunge baada ya 2025, tena ikiwa ni kwa chama chenu.

Muda utazungumza.
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
33,451
2,000
Magufuli Magufuli,utadhani kuna la maana alifanya. Wabongo ujinga umewajaa sana,yaani mnamwabudu mtu kwa kutimiza wajibu wake. Jitu zima na kitambi chake anatumia rasilimali za nchi kutetea magufuli ambaye alijitakia mwenyewe kuharibu nchi
 

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
2,079
2,000
^Fanyeni yote. Paruaneni sana tu mkipenda; hata tumieni sime za Mmasai au bastola ya 'Mjirumani' Ila kumbukeni tu kutukamilishia miradi adimu & azizi alizoasisi kipenzi chetu JPM plus zileee ahadi za kurasa 303.^ ~ Alisikika Mzalendo mmoja
Siyo kukamilisha Bali waendeleze, hata akija rais mwingine ataimalizia

Hili ndilo kosa alilofanya magufuli, kuanzisha miradi mikubwa was wakati mmoja na kutaka kúimaliza kwa muda mfupi.

Hakujali maisha watu.
 

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
890
1,000
Magufuli Magufuli,utadhani kuna la maana alifanya. Wabongo ujinga umewajaa sana,yaani mnamwabudu mtu kwa kutimiza wajibu wake. Jitu zima na kitambi chake anatumia rasilimali za nchi kutetea magufuli ambaye alijitakia mwenyewe kuharibu nchi
Hilo jina utalisikia sana....!

JPM amekuwa SI unit kwa kipimo cha urais wa nchi hii. Kila Rais ajaye atapimwa kwa kigezo cha je ataweza kumfikia JPM, je ataweza kumpita JPM?
 

Nziiri

JF-Expert Member
Jul 23, 2020
367
500
Magufuli alifanya mengi mema, tuyaenzi.
Lakini personification ha hayo mema ni utaahira, maana kulikuwepo na watu wengine.

Kuna mengi vile vile alifanya ya ovyo na si ya kuuga.
Ukabila,,uprndeleo wa miradi, lugha chafu e.t.c
Yale mema aliyofanya alitimiza wajibu wake sawa na kila mtu anavotimiza wajibu wake. Yale ya ovyo ndio tutamkumbuka nayo kama rais wa ovyo kabisa kutokea tangu tupate uhuru.
 

nguvusimba

JF-Expert Member
Feb 17, 2020
340
1,000
Magufuli alifanya mengi mema, tuyaenzi.
Lakini personification ha hayo mema ni utaahira, maana kulikuwepo na watu wengine.

Kuna mengi vile vile alifanya ya ovyo na si ya kuuga.
Ukabila,,uprndeleo wa miradi, lugha chafu e.t.c
leo wasukuma wanajiona kama miungu watu, wanadhani wana haki na hii nchi kuliko makabila mengine
 

Jasmoni Tegga

JF-Expert Member
Oct 28, 2020
4,147
2,000
Siyo kukamilisha Bali waendeleze, hata akija rais mwingine ataimalizia
Hili ndilo kosa alilofanya magufuli, kuanzisha miradi mikubwa was wakati mmoja na kutaka kúimaliza kwa muda mfupi.

Hakujali maisha watu.


^Hakujali maisha ya watu^!??? Kwa kauli yako hii, naendelea kuthibitisha ukweli wa hoja ya Mbunge wa Mtera iwapo kweli elimu ya Tanzania inawasaidia wengine wa sampuli yako!?

Hivi hiyo miradi ilikuwa kwa ajili ya kuboresha maisha ya miti au watu!??? Umesahau ile mashine iliyokuwa mbovu Muhimbili NH for months, mgonjwa ambaye angefanyiwa check ups & oparesheni amelala miezi sakafuni akiingoja itengenezwe!??? JPM alipotia timu, just in a week mashine ikapona?

Naona unataka viongozi wanaopishana angani kwenda Dubai & Ulaya, siyo!??? Au waleee wasafirisha twiga!??? Nawaambiaga watu kila kukicha: pls heshimuni sana mvi za Mzee Mwinyi.

Kichwa chake ndiyo bayografi ya JPM kwa sasa -- ^Tulishindwa siye kwa miaka 40, yeye kayaweza, tena kwa muda mfupi!^ Niongeze volume, au!???
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom