Kimeumana! Gambo amshukia kama mwewe mkurugenzi wa jiji la Arusha

nyamadoke75

Member
Apr 1, 2020
86
280
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amemchukia vikali Mkurugenzi wa jiji la Arusha, Dr John Pima kwa kumweleza wazi kwamba mkakati wake wa kumdhoofisha ili wananchi wa Jimbo hilo wamchukie hatafanikiwa kwani yeye ametokana na changuo la wananchi.

Akiongea katika mkutano wa hadhara katika zoezi la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri ya jiji la Arusha Kwa vikundi vya ujasiriamani lililofanyika katika viwanja vya Kilombero ,Gambo alikerwa na mpango wa mkurugenzi huyo wa kutaka Mbunge huyo asialikwe katika zoezi hilo.

Gambo aliibuka ghafla katika hafla hiyo na baadaye kupata fursa ya kuongea ambapo alimchana Bila kupepesa macho mkurugenzi Pima , yaakimwambia kwamba yeye amechaguliwa na mtu mmoja na kwamba muda wowote anaweza kung'olewa.

"Kati yetu sisi tuliopo hapa mimi nimechaguliwa na wananchi baada ya kuniona nafaaa kuwawakilisha wakifuatiwa na madiwani tofauti na hapo wewe mkurugenzi umeteuliwa tu na mtu mmoja, mkuu wa mkoa mshauri mkurugenzi awe mtulivu hawezi kumkataa mbunge"alisema Gambo na kuongeza kuwa.

Wakati nachaguliwa na wananchi Pima alikuwa amelala ofisini lazima.atambue kwamba tulipata kura Kwa shida kulizunguka jimbo la Arusha sio kazi rahisi mwambie amheshimu mbunge.

Gambo alikerwa na mkakati wa Pima kutomwalika kwenye shughuli hiyo ya utoaji wa mikopo Kwa vikundi vya ujasiriamani.

Hata hivyo Gambo alimwaibisha Mkurugenzi huyo baada ya kuamua kutoa fedha zake kuwakopesa bila riba baadhi ya wananchi waliotoswa kupokea mkopo wa jiji la Arusha na kuahidi kuanza kutoa mkopo wa sh, 200,000 Kwa kila mtu aliyeko kwenye kikundi chenye watu 100 kuanzia Sasa.

Hata hivyo RC John Mongela alisema kuwa nikiwapatanisha maendeleo hayatakuja Bora msipatane ili maendeleo yapatikane.

IMG-20211006-WA0007.jpg
IMG-20211006-WA0008.jpg

 
Laana ya kumdhalilisha Rais ,Magufuli ambaye alimpa ukuu wa mkoa na pia ubunge imeanza kuonekana. Huyu Gambo hatabaki salama .Ni mpuuzi Fulani.Nafikiri akapimwe akili.
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amemchukia vikali Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dr John Pima kwa kumweleza wazi kwamba mkakati wake wa kumdhoofisha ili wananchi wa Jimbo hilo wamchukie hatafanikiwa kwani yeye ametokana na changuo la wananchi
 
Watu wasiokua na haya wala akili ndio hawa taipu za Gambo, kajamaa kalivyokua RC kalihangaika sana na Lema na upinzani kwa ujumla sasa kanalalamika nini, atulie sindano iingie maisha haya ndivyo yalivyo ukiosha utaoshwa tu ndio ilivyo.
 
Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amemchukia vikali Mkurugenzi wa jiji la Arusha,Dr John Pima kwa kumweleza wazi kwamba mkakati wake wa kumdhoofisha ili wananchi wa Jimbo hilo wamchukie hatafanikiwa kwani yeye ametokana na changuo la wananchi
Wew gambo sijui gombe si ulizoea kuwatesa wapinzani gerezani? Sasa subiri dawa ikuingie. Kwanza hukuchaguliwa na mtu yeyote ni huyo mkurugenzi ndio aliye kutangaza kimizengwe na ndio maana anaona huna faida yeyote kwa wananchi ubunge wako ni wa viti maalumu dada wewe mrisho.
 
🤣🤣Huyo ndiye Komredi Mrisho Gambo.

Labda Dr.Pima hamjui vizuri El Comandante Gambo.

Aulizie nguvu zake kipindi kile cha CCM STAMINAZ ya kina Komredi James Ole Millya na komredi Ally Bananga Mwatiga.

Dr.Pima akaziulizie nguvu za Komredi Gambo kwa mama yetu Komredi Mary Chatanda.

My take:

MBUNGE ana haki ya kualikwa katika miradi ya MAENDELEO...Awe wa CCM ama upinzani....Wabunge ndio wanaotunga sheria zetu.

#SisiNiWamojaChiniYaChifuMkuuHangaya

#NchiKwanzaKablaYaMaslahiYetuNaNafsiZetu

SIEMPRE CCM
 
Laana ya kumdhalilisha Rais ,Magufuli ambaye alimpa ukuu wa mkoa na pia ubunge imeanza kuonekana. Huyu Gambo hatabaki salama .Ni mpuuzi Fulani.Nafikiri akapimwe akili.
Tumuache apumzike kipenzi chetu JPM.

Lini Gambo alimdharau mwenyekiti wake wa zamani?

Siasa HASIMU za vikundi hazikisaidii CHAMA.

#SiempreJMT
 
Wapiga kura.....

Kwani mkurugenzi anachaguliwa na wananchi?!!!

Hayo usemayo yatatokea ikiwa tu Gambo atakataliwa na kamati kuu ya CCM....si na mwingine yeyote awaye.......
 
Back
Top Bottom