Kimenuka P-Funky Majani na Jose Chameleon, kisa wimbo wa 'Bomboclat'

Fortunatus Buyobe

JF-Expert Member
Nov 9, 2011
463
1,127


Prodyuza mkongwe wa muziki nchini, P-Funky 'Majani' kakinukisha kwa Jose Chameleon kisa ni wimbo wake wa Bomboclat kutumika kama soundtrack kwenye movie ya Lupita Nyong'o iliyoshootiwa Marekani. Katika uchunguzi, 'Majani' kabaini Chameleon ndio kalipwa.

Majani akawasiliana na Chameleon akitaka maelezo jamaa akamdanganya eti kapewa dola 2000 kumbe kapewa zaidi ya dola 50,000. Majani kashtaki COSOTA wakafatilia Uganda bt jamaa hawakujibu chochote. Majani kawasiliana na Walt Disney watayarishaji wa movie wameomba wayamalize nje ya mahakama lakini nao watadili na joseee.

Credit Bongo5.com
 
Najiuliza tu; ina maana Walt Disney na ukubwa + plus ukongwe wao kwenye game, hawakuliona hilo toka mwanzo?

Tatizo Bongo huwezi jua zipi za vijiweni, zipi authentic. Watu wanachakachua hatari.
 
Ndio mimi jibu langu ni kuwa unahisi walt Disney hawwezi lulipa usd 50000 kwani watapata hasara. Kwa taarifa tu gharama za maandalizi tu ilikuwa zaidi ya dola millioni moja na nusu
Na vipi kuhusu matarajio ya mauzo baada ya filamu kuingia sokoni, au sio bongo muvi hiyo?(nimeliza ila sina jibu).
 
What is the logic behind your question? Kifalsa inaaminika kilamuuliza swali ana jibu. Sema huwa anauliza ili kuona kama jibu lake ni sahii
Kwel kabisa, pia mtu akikuuliza swali kabla ya kumjibu pia lazima ujue ni kwa nn ameuliza.
 
Najiuliza tu; ina maana Walt Disney na ukubwa + plus ukongwe wao kwenye game, hawakuliona hilo toka mwanzo?

Tatizo Bongo huwezi jua zipi za vijiweni, zipi authentic. Watu wanachakachua hatari.
yawezekana hawakujua, labda chameleone aliwaambia ni yake

yawezekana walijua wakachukulia rahisi
 
Na vipi kuhusu matarajio ya mauzo baada ya filamu kuingia sokoni, au sio bongo muvi hiyo?(nimeliza ila sina jibu).
Hiyo sio bongo muvi. Lupita nyongo ni wa kimataifa zaidi. Ameshashiriki filamu na wakongwe kina brad pit. Keshabeba tuzo za oscsar ambayo bado ni ndoto ya actors wengi wakubwa marekani. This is not a matter to underestimate. P funk anaongea hadi anataka kulia. Ametumia pesa nyingi kufatilia haki yake. Anasema lawyer kumlipa kwa saa tu anatumia dola 400. Chameleon ni tapeli. Watanzania tupige kelele juu ya ujangili huu.
 
Back
Top Bottom