Kimenuka Ngorongoro, wananchi wamtaka Rais Samia kumtimua Dkt. Manongi

Kama hoja ndo hizo basi bado hazijitoshelezi kabisa kumtoa Fred Manongi.

Mlipohamishwa toka Serengeti mlipelekwa Ngorongoro kwa majaribio tu kama wanyama pori na binadamu wanaweza ishi pamoja ata mie nilikuwa shahidi wa hili huo mwaka 1959.

Kama mamlaka imeona imekuwa ngumu kwa binadamu na wanyama pori kuishi pamoja basi ondokeni tu kwanza kipindi mnahamishiwa Ngorongoro population yenu ilikuwa ni ndogo sana kulinganisha na sasa kwani mlizaliana sana pia mliita jamaa zenu kutoka nje ya hifadhi kuja kuishi nanyi.

Kutokana na idadi yenu kuongezeka mmekuwa chanzo cha kuenea kwa mimea vamizi (invasive spesies) kama vile Eleusine jaegeri na haya ma solanum incanum ambayo hata siyo malisho kwa viumbe wetu.

Alafu tuacheni tu uongo hivi kweli kuna binadamu anaweza acha kumla swala anaye ingia anga zake?

Mamlaka ya uhifadhi ya Ngorongoro imefanya makubwa sana dhidi yenu wakati mnaouwezo kabisa wa kujitafutia riziki. Nasikia mpaka NCAA ilikuwa ikiwalimia na kuwavunia mazao nje ya hifadhi ili tu mule bila kufanya kazi yoyote!

Hameni bhana na hiyo mifugo yenu maana najua fika hamuwez vumilia kuona ng'ombe wenu akiliwa na simba.
Kwamba mlipowahamishia huko 1959 mliwatoa kizazi ?
 
Wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutengua uteuzi wa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Dk.Freddy Manongi kwa kukiuka sheria ya uanzishwaji wa hifadhi hiyo na kunyanyasa wanachi wa eneo hilo.

Aidha wamemuonya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk.Damas Ndumbaro kuacha mara moja kushirikiana na mtandao wa Dk.Manongi uliodhamiria kuhamisha wananchi wa jamii ya kifugaji wanaoishi Tarafa hiyo ambao wamekuwa kivutio kikuu Cha watalii.

Pia wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kufanya ziara katika eneo lao ili kusikiliza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kuhamishwa kwenye makazi yao ya kudumu.

Akizungumza kwaniaba ya wananchi wa Tarafa hiyo mmoja wa wakazi hao na mzee wa mila (Laigwanani) Metui Ole Shaudo, alisema wamepewa notisi ya siku 30 inayoishia Mei 11 mwaka huu kuondoka kwenye makazi yao ya kudumu ndani ya hifadhi hiyo ili kupisha shughuli ya uhifadhi.

"Tunamuomba Rais wetu na mama yetu Samia Suluhu Hassan kumuondoa huyu Dk.Manongi hapa NCAA sababu anaendesha mamlaka hii kama familiya yake au boma yake na kutunyanyasa sisi kwa mambo mengi,"alisema.

Alisema kabla ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo mwaka 1959 wananchi hao walihamishwa toka Serengeti ili kupisha uanzishwaji wa hifadhi ya Serengeti na kuhamishiwa Ngorongoro, lakini wanashangaa tena wanafukuzwa.

"Sisi tumekuwa tukiishi vizuri na wanayama nabkuwalinda na hata sheria ya uanzishwaji hifadhi hii ya Ngorongoro inatambua kuishi kwetu na wanyama sasa leo wanataka kututoa watupeleke wapi,"alihoji.

Aidha wamemuomba Rais Samia kuwapa muda wa ziada wa kukaa na wataalamu toka ndani na nje ya nchi wanaohusika na usimamizi wa eneo hilo, pamoja na wizara ya Maliasili na Utalii,mifugo na ardhi ili kushauriana namna bora ya kumaliza suala hilo.

Alisema wanyama wamekuwa wakiuwawa pembezoni mwa hifadhi kama wilayani Karatu na sio ndani ya hifadhi hiyo.

Aidha alisema NCAA inawanyanyasa siku nyingi kwa kuwanyima eneo la malisho na maji kwa mifugo yao jambo linalotesa mifugo yao.

Alitahadharisha kwa Rais Samia kuwa makini kwa watu anaowateua ili wasichangie kuvunja katiba ya chi ikiwemo ya kunyima watu haki zao za kuishi,kuabudu na mengine.

"Maana katika hili wanatuondoa sisi kaya 178 zilizopo eneo la Tarafa hili hapa kuna nyumba za ibada za wakristo na waislamu,Zahanati,shule na vituo vya afya kitu ambacho sio sahihi kwa mustakabali wa nchi yetu,"alisema.

Naye mmoja wa wakazi wa eneo hilo Napokie Peshuti alisema notisi waliyopewa inakiuka haki za binadamu kwani haijazingatia kama hayo ni makazi ya kudumu.

"Notisi hii tuepewa kama vile sisi wakimbizi sio wazaliwa wa Tanzania, lakini wakati tunaanza kujenga nyumba zetu wao walikuwa wapi wasione na kutuachisha kumalizia ujenzi leo ndio wanakuja na amri zao hili sio haki tunaonewa wakati sisi ni binadamu kama walivyo binadamu wengine,"alisema kwa masikitiko.

Kuhusu madai na hoja zinazotolewa za kuhamishwa makazi hayo za kuwa wanazaliana sana Napokie, alisema siyo za kweli kwani sasa wanazaa watoto watatu au wanne tofauti na wazee wao walioa wanawake wengi na kuzaa watoto zaidi ya 100.

Benard James ambaye ni mkazi wa eneo hilo alisema wakati wanataka kuwafukuza eneo hilo vema wakakumbuka kuwa hata wao wamechangia hifadhi hiyo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kutangazwa kuwa ni urithi wa dunia.

Wananchi wa eneo hilo kwa miaka zaidi ya kumi sasa wamekuwa wakikumbana na sintofahamu ya kutakiwa kuhama kwa madai wanatishia uwepo wa ongeseko la idadi lubwa ya watu na kuhatarisha usalama wa hifadhi.

Hata hivyo jitihada za kumpata dk.Manongi kujibu malalamiko hayo hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa.

Ends.....

Walaji wa fedha kupitia MIGONGO ya wananchi.....
 
Tunataka dola za utalii kutoa huduma za afya, elimu na maji .Wapewe eneo lingine, mbona Tanzania ni kubwa sana
Si mtengeneze mbuga zenu muweke utalii wenu? Wale twiga waliopanda ndege...si walienda kuanzisha mbuga mpya? Ninyi kuswaga tu hao twiga kuelekea maeneo mengine mnapotaka kuwaamishia watanzania wenye asili ya kimasai mnashindwa?
 
Shida yenu moja tuu mmezaliana mnoo kwasababu mkajifanya nyie ndio malast born wa taifa..mnapewa vibunda bila kazi..

Sasa kale kaeneo mlikopewa hakawatoshi sasa mnabanana na wanyama pori.. mnamaliza malisho ya wanyama pori..sasa inatakiwa muwapishe wanyama nao Watanue..

Mkatafute pori lingine na mtakakoenda uko msijisahua mkizaliana kwa wingi itawalazimu kutoka tena.. angalizo ardhi yako ikihitajika na serikal inatakiwa uiachilie kwa mpango wa maendeleo.

Ndugu zangu wakazi wa tarafa ya ngorogoro msijione Bora kuliko Tanzania. Nawashauri ombeni mfidiwe mchape rapa..najua mnawaza mtaanzaje maisha mapya.
 
Dk Manongi hatimuliwi badala yake wao ndiyo watatimuliwa na kuondoshwa huko kwenye mbuga za wanyama.

Wamasai ondokeni Ngorongoro
Shida yao, wanadhani ngorongoro niya kwao, Hiyo hifadhi ni mali ya Watanzania. WAONDOKE BHANA, pia shida kubwa ya utaratibu wa ajira ndiyo unaomfanya Dr Manongi apate wapate wakati mgumu katika kutekeleza hili. Asilimia 80 ya waajira ni wazawa, sasa kila mpango au mikakati ya kiutawala inayopangwa kutekeleza azma hiyo, inavuja mapema. Hivyo akienda kufanya maamuzi jamaa wanakuwa tayari wameshajipanga.
Ili afanikiwe, hao waajiriwa wazawa wahamishiwe, MOYOWOSI GAME RESERVE, na wafanyakazi wa moyowoso wahamishiwe Ngorongoro, maana hapo hakuna hata mmoja mwenye familia ndani ya NCAA. Maamuzi yatatekelezeka. Hamisha wote hao. USHAURI WABURE KWENYE MENEJIMENTI
 
Back
Top Bottom