Kimenuka Kinondoni: Mbowe na wanachadema waliokuwa wanaandamana kwenda ofisi za NEC, watawanywa kwa mabomu

Nikukomaa hadi ccm na serikali yake wajue, upuuzi hautakiwi hata kidogo. Hii nchi itatuchuka miaka mingi kuwa na dira thabiti, kama serikali nzima na vyombo vya usalama vinaweza kushughulika na uchaguzi wa jimbo moja kwa takribani mwezi mmoja.
We wadanganye wenzio huku umejificha humu jf nenda naweye uwanja wa vita uone
 
Huyo DED Kagurumjuli amepoteza sifa za kuwa msimamizi wa uchaguzi Kinondoni, haiwezekani barua za mawakala zitolewe usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi, hata Mkurugenzi wa NEC naye kwa hili hawezi kukwepa, amepoteza sifa na credibility ya Tume kwa washiriki wa uchaguzi.

Lkn pili, hivi imefikia hatua watu hawatimizi wajibu mpaka watu waandamane kudai haki zao? Tumeona Mbeya, Sugu alinyimwa dhamana kwa wiki kadhaa hadi pale wafuasi wake walipoandamana na kusababisha biashara kusimama Mbeya. Hii ni aibu.

Vv
Hii Nchi Hii Acha Tuuuu

Yan Kuna Vitu Vinakera Hadi Karaaah
 
Cocochanel, damu isiyokuwa na hatia imemwagika chini, tayari inalia mbele za Mungu ikidai kulipiziwa kisasi. Watu wameapishwa Siku tano zilizopita mpaka Leo hawajapewa fomu zao za viapo, ni kosa la nani?.
Mungu hadhihakiwi , mtavuna mnachokipanda.
 

NDUGU,
mimi sijui mambo ya sheria,hivyo nmeona hiyo video watu wakipgwa na kuvutwa vutwa na hao polisi .
je ni halali polisi kufanya hivyo ?
je nikishtaki atachukuliwa hatua ?

ndugu zangu SIASA tuwaachie wenye SIASA...!!

POLENI WOTE MLIOPATA CHA MOTO KINONDONI
 
Awali nilipokea vibaya taarifa ya maandamano yakuwa chadema ndio wakorofi ila kwa habari hii nimeelewa mkorofi na mvuruga amani na maisha ya watanzania.
 
Mawakala lazima watoke Kinondoni sio Nje ya Mikoani, Kwanini mnaenda kuokota Watu toka Moshi?
Ina maana hamuwaamini wana Chadema wa Kinondoni kuanzia kwenye kugombea mpaka kwenye uwakala?

Hata kama unaongea upuuzi ngoja tu kuweke sawa, hao maofisa wa polisi na tume ya uchaguzi wote ni wazaliwa wa kinondoni? Sheria inasema mpiga kura sharti awe amejiandikisha kinondoni/ sehemu husika ya kupigia kura na sio kinyume na hapo.
 
Back
Top Bottom