Kimei asema kifo cha Mkapa ni pigo kubwa

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
375
1,000
Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Dkt Charles Stephen Kimei amesema kifo cha Rais mstaafu awamu ya tatu Mzee Benjamin William Mkapa ni pigo kubwa kwa familia, Tanzania na Afrika.

Akimuelezea alipofika kutoa pole kwa familia ya hayati Mzee Mkapa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam Dkt Kimei amesema

"Mzee Benjamin William Mkapa alikuwa kiongozi mwenye uzalendo wa hali ya juu kwa nchi yetu na Afrika. Alikuwa mwenye ndoto na maono makubwa ya Afrika kutumia utajiri wa rasilimali ilizonazo na idadi kubwa ya watu kujitegemea kiuchumi. Alihimiza umoja, amani na mshikamano kama msingi muhimu kwa maendeleo. Hakika tumempoteza kiongozi mahiri ambaye ushauri wake na uzoefu wake bado vilihitajika.

Natoa pole kwa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli, familia yake na watanzania wote kwa msiba huu. Tunauombea apumzike kwa amani."

Dkt Kimei amesema namna pekee ya kumuenzi Mzee Mkapa ni kuyaishi mazuri na maono yake kwa vitendo na kuendelea kumuombea apumzike kwa amani.

Pumzika Kwa Amani Mkapa, Buriani Mkapa, Tutaonana Baadae
IMG-20200725-WA0040.jpeg
 

Amazon Woman

JF-Expert Member
Aug 24, 2016
709
1,000
Hakuna ujanja kwenye kifo...Mkapa and his wealthy kaacha. Zile share za hisa Geita Gold Mine sijui zitamiminikia wapiiii
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,369
2,000
Pigo kwako, jisemee wewe usijumishe wengine. Kwa ambaye amepoteza ndugu yake katika mikono ya awamu ya tano, atakuona kama juha kusema ni pio.

Alisaidia nini kumkataza bwana yule kupoteza, kuua,kubambkia watu kesi etc etc, kwa aliyeathirika na hayo, atakuona kichaa! Jisemee wewe
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom