SautiYaMnyonge
JF-Expert Member
- May 13, 2018
- 439
- 742
Na Mwandishi Wetu,
VUNJO, Tarehe 28/07/2021.
Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mhe. Dkt. Charles Kimei leo amekabidhi mashuka kwenye vituo vya Afya vya Mwika na Himo.
Akikabidhi mashuka hayo aliwapongeza watoa huduma kwa nzuri ya kuhudumia wananchi:
"Niwapongeze kwa kazi nzuri mnayoifanya, tunajua changamoto zinazoikabili vituo vyetu vya Afya. Miongoni mwao ni pamoja na upungufu wa mashuka 100, hivyo nimekabidhi mashuka haya ili kuweza kupunguza changamoto hiyo."- Dkt. Kimei (Mb).
Mashuka hayo yalikabidhiwa kwenye vituo vya Afya Kata ya Mwika Kaskazini na Makuyuni.
Kwa upande wa madiwani kwa pamoja (Mhe. Samwel Shao- Mwika Kaskazini na Mhe. Dickson Tarimo- Makuyuni) walimpongeza Mhe. Mbunge kwa kuendelea kujitoa kwa ajili ya wananchi.
Uongozi wa kituo cha Afya cha Mwika na Himo wamempongeza Mhe. Dkt. Kimei Mbunge wa Jimbo la kwa msaada huo. Wamemuomba aendelee kuwasaidia pale penye uhitaji huo.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Vunjo.