Kimeeleweka Dulla Mbabe vs Twaha Kiduku 2

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,390
21,079
Ninaona uvivu kuandika.

Ila pointi ya msingi ni kwamba lile pambano ambalo tulikuwa tukilisubiria kwa hamu hatimaye kimeeleweka.

Hatimaye siku ya tarehe 28/8/2020 tutashuhudia tena kwa mara ya pili mpambano wa kukata na shoka kati ya bondia Dulla Mbabe na mpinzani wake Twaha Kiduku.

Kwenye pambano la kwanza kati ya Dulla Mbabe na Twaha Kiduku upinzani ulikuwa mkubwa sana na wengi wanaamini Twaha ndiye aliyeshinda pambano lile japo maamuzi ya majaji waliamua sare.

Sasa ubishi utaenda kumalizwa tarehe 28/8 hapo uwanja wa uhuru jijini dar es salaaam.

Twaha mara kwa mara amekuwa akilalamika kwamba Dulla amekuwa akimkimbia mara kwa mara kwa kuhofia kupokea kipigo kitakatifu kutoka kwake.

Sasa mbivu na mbichi zitajulikana siku hiyo , ngoja tuendelee kusubiri.

Screenshot_20200728-173134.jpg
 
Back
Top Bottom