Kimbunga CCM; Prof. Majimarefu, Nundu wapigwa mweleka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kimbunga CCM; Prof. Majimarefu, Nundu wapigwa mweleka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Oct 5, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  [h=2][/h]IJUMAA, OCTOBA 05, 2012 06:04 NA MWANDISHI WETU, KOROGWE

  *Prof. Majimarefu, Nundu wapigwa mweleka
  *Waziri Kigoda ang’ara, Mbunge Masele hoi
  ALIYEKUWA Waziri wa Uchukuzi na Mbunge wa Jimbo la Tanga, Omari Nundu, amebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC). Katika uchaguzi huo, Nundu aliambulia kura 127 kati ya kura 1,175 zilizopigwa.

  Nundu ameangushwa na mpinzani wake mkubwa wa siasa, ambaye aliwahi kuwa Meya wa Jiji la Tanga, Salim Kassim Kisauji, aliyeshinda kwa kupata kura 514. Kura hizo, zilipigwa mara mbili, baada ya awamu ya kwanza kukaribiana kwa karibu na Saumu Bendera, aliyepigiwa kura 446.

  Katika awamu ya kwanza, Kisauji aliongoza kwa kupata kura 556, akifuatiwa na Saumu Bendera (458), Nundu (127) na Salehe Bakari Masudi (37), ndipo awamu ya pili Kisauji akashinda kwa kura 514 na Saumu akipata kura 445.

  Nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga, imechukuliwa na Kassim Mbughuni, aliyeshinda kwa kupata kura 540 na kuwashinda Mwanshamba Pashua, ambaye alipata kura 372, huku Mkuu wa zamani wa Wilaya ya Tanga, Samuel Kamote akipata kura 200 na Salim Rashid Al-Mazurui, akiambulia kura 98.

  Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, ni Danny Mgaza aliyepata kura 485, Muzzamili Shemdoe (485), Mozza Mohamed (427) Mwanshamba Shekue (412) na Rukia Mapinda (413).

  Lipakisio Kapnade, alichaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Tanga, baada ya kupata kura 75, huku Bernard Goliama, akishinda nafasi ya Katibu wa Mipango, Uchumi na Fedha.

  KOROGWE VIJIJINI

  Habari kutoka Korogwe Vijijini, zinasema, Mbunge wa jimbo hilo, Stephen Ngonyani maarufu (Profesa Majimarefu), ameangukia pua, baada ya kushindwa na mpinzani wake, mchumi Dk. Edmund Mndolwa.

  Uchaguzi huo ulifanyika juzi na kusimamiwa na mbunge wa zamani wa Pangani, Mohamed Rished.

  Katika uchaguzi huo, nafasi ya NEC ilikuwa na wagombea watatu, lakini Dk. Mndolwa, aliibuka mshindi kwa kupata kura 962, akifuatiwa na Profesa Majimarefu aliyepata kura 310, huku Aweso Mandondo, akipata kura 112 na George Kinyasi akiibuka na kura 21.

  Katika nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Korogwe Vijijini, ilirudi kwa Nassor Malingumu, ambaye alipata kura 1,230, akifuatiwa na Majaliwa Tekero aliyeambulia kura 164.

  Waliofanikiwa kupata nafasi ya kuingia Mkutano Mkuu wa CCM Taifa, ni Halima Mussa, Mohamed Doadoa, Seif Bilal na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Sadick Kallaghe.

  HANDENI

  Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, ameibuka kidedea katika uchaguzi wa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupitia Wilaya ya Handeni.

  Akitangaza matokeo hayo, msimamizi huyo ambaye pia ni mbunge wa Mkinga, Dastan Kitandula alisema, Dk. Kigoda aliibuka mshindi, baada ya kupata kura 943 kati ya 1,112.

  Dk. kigoda alinyakua nafasi hiyo na kuwashinda wapinzani wake, Hadija Masudi aliyepata kura 27, Mhandisi Juma Nkondo aliyepata kura 75 na Agustino Mwengele aliibuka na kura 61.

  Pia alimtangaza Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Handeni, kuwa ni Athumani Malunde, aliyepata kura 534, dhidi ya Saidi Ngole, aliyepata kuta 356.

  Aliwataja wajumbe watakaowakilisha mkutano mkuu taifa kuwa ni, Salimu Mtelela, Riziki Msente, Dk. Mohamedi Muhina, Rehema Rashidi na Amina Omary Kigoda.

  Alisema, wajumbe watakaowakilisha Halmashauri Kuu ya Wilaya kupitia Jumuiya ya Wazazi, ni Jumanne Mzee na Joji Mwabela, wakati watakaowakilisha mkutano mkuu ni Zaina Mavumba na Riziki Msente.

  Pia aliwataja watakaowakilisha Halmashauri Kuu Wilaya kupitia kundi la UWT kuwa, ni Amina Kigoda, Josephine Mgaza, Hawa Sangali, pamoja na Riziki Said Mtenta.

  Alisema kwa upande wa kundi la vijana, waliochaguliwa kuwa ni Jabil Abdallah Mgaya, Mhandisi Nuru Marambo, Daudi Lukoya, pamoja na Abdallah Musa Bojo.

  WILAYA MBOGWE
  Habari kutoka wilaya mpya ya Mbogwe mkoani Geita, uchaguzi umefanyika kwa amani chini ya Katibu wa CCM Wilaya, Augustino Mbogo jana na kushuhudia vigogo wakitupwa nje ya ulingo.

  Katika mkutano huo, msimamizi wa uchaguzi, Pili Edwinsonje alimtangaza Deus Lyankando kuwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya, kwa kupata kura 483 na kumshinda aliyekuwa mbunge wa Bukombe, Robert Mashalla aliyepata kura 368.

  Alisema nafasi ya NEC, ilichukuliwa na Said Tangawizi, kuwa mshindi kwa kupata kura 473 na kuwashinda vigogo wawili akiwemo mbunge wa jimbo hilo, Augustino Masele aliyepata kura 354 akifuatiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri, Methew Kanela aliyeambulia kura 42.

  Nafasi ya Katibu Mwenezi, ilibaki kwa Johari Omari Juma, aliyepata kura 74 na kumshinda mpinzani wake, Andrew Bwire aliyepata kura 34, wakati nafasi ya Katibu wa Uchumi na Fedha, ilinyakuliwa na Diwani mkongwe Daud Mabenga, ambaye alipata kura 69 na kumshinda Kulwa Mashenji Ntoba aliyeambulia kura 37.

  Aliwataja waliochaguliwa kutoka kundi la UVCCM nafasi ya Halmashauri Kuu Wilaya, kuwa ni Nyanda Keyu, Masele Kanyala, Mahuma Masanja Yusuph na Mawaya Mawaya.

  Kundi la wazazi ni Mbaluku Salum Mseba, Yohana Malale, Kitambo Kishimb, Julius Maganga, Kazimili Ngodagula na Chenya Ngadule Manoni. Nafasi ya mkutano mkuu ni Ester Madungume na Ester Mihayo.

  Wakati nafasi ya mkutano mkuu Taifa, waliochaguliwa ni Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, Hasna Sudi Mwilima, Dabacha Simon, Salum Semba, Methew Kanela na Robert Mashala.  [h=4][/h]
   
 2. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,563
  Likes Received: 16,531
  Trophy Points: 280
  Hata ule U-profesa wake haukumsaidia?Ama kweli Mganga hajigangi!!!!!!!!!!!!:A S embarassed:
   
 3. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mambo ya siasa yanashangaza sana! Mtu anaye nisikitisha sana ni Mh.Nundu nafikili angejuwa kwamba mambo ya TAIFA letu wakati mwingine yamejaa unafiki na kuharibiana sifa!!! Kama angeli bahini hilo mapema hasingekubali kurudi nchini, ange endelea kubaki zake Ulaya wanako thamini taaluma yake na sio hapa BONGO. Mambo ya Kambarage kuhusu uzalendo na kufikili unakwenda kusaidia kujenga TAIFA lako naona siku hizi ni Viongozi wachache sana wanao jali hilo - na ili kwa bahati mbaya ndilo lilio mtokea Mh Nundu inasikitisha SANA.
   
 4. Mwakitobile

  Mwakitobile JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 453
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Prof maji marefu,kashindwa kufurukuta kwenye maji ya ugoko!dhambi ya kuibwaga mikoba ya uganga,inaanza kumla taratibu,mpaka atubu.
   
 5. LESIRIAMU

  LESIRIAMU JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 4,006
  Likes Received: 2,223
  Trophy Points: 280
  Kumbe kuna wakati tiba za jadi zinashindwa? Sasa wamemtema mganga wao kwenye huu uongozi usio na maslahi! Wakamwacha akagange ujinga bungeni kwenye maslahi ya jimbo na Taifa kwa ujumla? Yaani nawashangaa sana watu wa Korogwe
   
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  :biggrin1: alishindwa kulikoroga ashinde? Dah kweli waganga wa kienyeji ni uongo mtupu hakuna kitu pale
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Du!!! Hata Mzee wa Ndumba kashindwa
   
 8. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,797
  Likes Received: 36,826
  Trophy Points: 280
  Kumbe kimbola hakisaidii.

  Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
   
Loading...