Kimbisa na Lukuvi; Mnasubiri Wafadhili na Wahisani au Amri Kutoka Ikulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kimbisa na Lukuvi; Mnasubiri Wafadhili na Wahisani au Amri Kutoka Ikulu?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Oct 22, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  [​IMG]Huu uchafu wa Dar, mnamsubiri nani awafanyie kazi na awasafishie jiji lenu?

  [​IMG]

  Ikiwa mna mamlaka na nyenzo, je mnahitaji nini?


  Kikitokea Kipindupindu, mtamlaumu nani?

  [​IMG]
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Samahani sana Hela tuliyonayo ni ya kununulia Benz za mameya na nissan za wakurugenzi usafi sio lazima kwa sasa, wewe unadhani tutaendaje airport kupokea wageni na magari wasiwasi. Ingawa tuna mapato makubwa tu yatokanayo na kodi nyingi, lakini POSHO za madiwani ni kipaumbele unajua kamati ziko nyingi sana na hukaa karibu kila siku hivyo Inabidi tuwalipe wao na suala la usafi wa Jiji ni Baadaye. Hata hivyo tunajitahidi sana kusafisha mji kwa kufagia mitaa na chelewa si unaona barabara zinavyong'ara. Ohoo nimesahau na takataka tunakusanya na magari ya takataka ambayo na yenyewe ni takataka si unajua dawa ya moto no moto???Mitaro kweli ni tatizo tunangoja Wajapani watusaidie sie hatuwezi kabisa na ndio maana namaliza kwa kukuomba kama mchungaji utuombee kipindupindu kisiingie kabla wajapani hawajafika.
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Mchungaji,

  Ungeongezea kuwauliza, wanasubiri nini taa za barabarani kuwaka? Barabara zote za Jiji ambalo linaonekana kubwa kuliko yote Tanzania ziko giza. Barabara kutoka uwanja wa ndege (Nyerere Rd) ikiwa giza kuanzia Vingunguti mpaka TAZARA (kwa sasa ni barabara zote Dar!), almost naambiwa kunaripotiwa vifo vya watu wanne kila wiki kwa kugongwa usiku wakati wakivuka kwani ni giza totoro! Ingekuwa ni sababu ya mgawo tungewaelewa, lakini hizi zinasubiri CCM wanunue nguzo hizo wakati wa kampeni nazo zikiwa zimebeba mabango mazito na kuelemewa ndo ziwake kwa kipindi cha miezi nane tu mpaka uchaguzi upite.

  Upuuzi mtupu, kama nchi haina mtu wa kumwajibisha mwingine, wanaangalia tu!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Oct 22, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Babu, sijawahi kukuona umekasirika hivi....yaelekea unakereka sana na hilo suala
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Julius,

  Hawa jamaa kama ukisikia kauli zao naamini hata wewe utakereka sana... Simply unaambiwa "Kwani wewe nani?"

  Upuuzi mtupu, washaigeuza nchi yao na wanapoenda kuomba kura kwa wananchi wanaenda kwa lugha za ulaghai mkubwa, nasikitika sana lakini ndiyo Tanzania yetu mkuu
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kinachoniudhi ni hawa watu wanaojiita watu wa mjini na kuwa misheni town, wakati wako short-changed karibia katika kila kitu kimaisha. Umeme hamna, kero mabarabarani, maji hayatoshi, uchafu kila pande, usafiri kero tupu, n.k. Tukitaka kujua nani mpenda mabadiliko hapa bongo ngojea tuone ni majimbo yepi ya uchaguzi bongo yatarudisha madarakani wabunge walewale walio fail ngwe hii inayopita. Halafu angalia wapi watabadilisha watu.

  Mabadiliko chanya ya uongozi na maendeleo yangeanzia Dar, nina imani mikoani ingelikuwa rahisi zaidi ku-assimilate. But as it stands, the opposite is the obvious truth.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Tatizo linaanzia kwa madiwani, watu wamefanya udiwani kama ajira, kwa nini isibadilshwe iwe kazi ya kujitolea na ikiwa hivyo watu watakuwa committed to the cause. Tatizo lingine ni priorities naona manispaa zina matumizi mengi ambayo si ya lazima sana. Mabenzi, landcruisers, sitting allowances badala ya magari ya taka, ambulance na magari ya maji machafu.

  Lakini mwisho tujiulize je hulka ya usafi imo miongoni mwa madiwani na watendaji, ni maoni yangu kuwa hawana hulka ya usafi. Inaelekea wahakerwi kabisa na uchafu vinginevyo wangeanza kuchukua hatua. Sijawahi hata siku moja kusikia jiji linaanzisha kampeni ya kuzuia watu wasitupe karatasi ovyo au jiji lina mpango wa kujenga public toilet etc kwao hizo sio agenda hata kidogo.

  Mwishoni kwa sababu inaelekea madiwani wameenda kuvuna pesa badala ya kufanya kazi na kwa sababu ni sisi tunaowaweka kwenye hizo nafasi basi tuchukulie kuwa wameshindwa, tunaambiwa kuwa wao wanafanya kazi kwa sera za chama chao basi tuchukulie kuwa sera ya chama chao ni uchafu mijini hivyo hatuna budi kuchagua madiwani prefarably wa chama kingine ambao wanaweza kuufanya mji wa Dar Es Salaam uwe wa kujivunia.
   
 8. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #8
  Oct 22, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Hawa si ndio wale wale waliokaidi hata maagizo ya Mkulu ya kutaka watu wawe na access na public places kama beaches na gardens..likiwemo la usafi? mbona hatujaona mabadiliko...au ndo yale ya kusema mkuu wa mkoa ndo bosi wa Rais?

  On the other hand kama tunataka mabadiliko kwa njia ya boksi la kura, je tuna watu mbadala ambao walau wanaonyesha matumaini? Au ndo tutaishia kuweka wapya ambao watatafuta mbinu mpya za 'kula'?


  yani ni presha tupu. by the way hivi barabara ya madela imeisha kujengwa wakulu au ndo bado longolongo? unajua kwa siye wa mikoani tufikirie pa kwenda kukwepa foleni
   
 9. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #9
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  KAIZER,Watu mbadala wapo wengi tuu, tatizo naloliona ni kuwa hatutaki kujiingiza kugombea udiwani tukidhani kuwa ni nafasi ya kisiasa. Nionavyo mimi udiwani uenyekiti wa mitaa na vitongoji hautakiwi kuwa nafasi ya kisiasa bali nafasi ya utendaji kabisa ili mkiingia kwenye vikao hamna siasa bali ni kazi ya kucontroll watendaji wa manispaa na miji katika mipango ambayo wananchi wamepanga. Tumechelewa kwenye uchaguzi wa vitongoji na mitaa kwenye udiwani tujitokeze kwa wingi sana proffessional na wasoni wengine ili manispaa zetu zitumike kwa kutuletea maendeleo na sio kuwafanya waganga njaa wawe madiwani.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Rev. Tuanzishe siku ya kuchapa viboko hawa viongozi wa mitaa... nao eti wanshinda maofisini tu!!! Hizi ndio kazi zao pia

  Lakini wa kuchapa zaidi viboko ni watu walio kwenye mitaa husika!!! Sie tulifanikiwa kutandika diwani makofi na mpaka leo heshima mbele hasa upande wa usafi na ulinzi

  It can be done
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Oct 22, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,785
  Trophy Points: 280
  Ndo hawa tunategemea watakuwa viongozi wa baadae wa ngazi za juu.Wanaubeba huu uzembe na kutowajibika mpaka kwenye ofisi nyeti kabisa. Ukisikia wanavyojisifu unashangaa. Ni kama miungu watu
   
 12. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #12
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Halafu uchaguzi wa serikali za mitaa tutawalipa mawakala wetu (wa CCM) posho. Ilitka pesa tutoe wapi? Na unadhani tukitumia gharama nyingi kufanya usafi wale FFU tunaowatuma kuwapiga mabomu waandamanaji tutawalipa na nini? Na mgambo wa jiji ambao wamekuwa vibaraka wetu je? Au mlitaka magari yetu yawekewe mafuta lita moja kama corrolla zenu? NA pesa za kwenda kuchukua majani ya ngombe chanika pamoja na posho ya dereva na vijana wa kupakia tutoe wapi?
   
 13. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #13
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mchungaji kuna jambo hujatuelewa 'sisi watu wa jiji" tupo very strategic. DAr ndio kituo cha wageni wote. Hata Bushi, na sasa tunamsubiri Obama, wanatua hapa. Unakumbuka hata Clinton alishukia hapa? Sasa hatufanyi usafi makusudi ili wakija waweze kutuoenea huruma halafu watupe misaada ya kupambana na Malaria na Kipindupindu ili tuanzia NGOs zetu na 'funds' tule!

  Hatusubiri ikulu, maana hawatasema. Kwani wao wanapita manzese au buguruni ili waone? Tukiweka wafagiaje wachache wakionekana wakati mkubwa anapita si baada tunaitwa ofisini kupewa pongezi? Na hata wakipita si vioo tinted na kwa sababu ya usalama hawashushi? Labda 2010 kwenye kampeni tutaanza.

  Halafu.. Kwa sasa, japo hata mitaro tumeshindwa kuchimba na iliopo kuzibua, japo tumeshindwa kuzoa taka, japo hospitali za jijini hazina dawa, japo tumeshindwa kupata madawati kwa shule zote za msingi, tunashughulikia mradi wa barabara za juu kuondoa foleni (japo magari yaendayo kasi bado hatujaleta).

  'Sasa najua tuu JF mtachonga CCM haijafanya kitu. Hayo yote hamuoni?'
   
 14. L

  Lingusenguse Member

  #14
  Oct 23, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 29
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huku Rwanda, Kagame usiku anawasha vogue lake(tena anaendesha mwenyewe) anazunguka mitaa ya Kigali.Ole wake meya akute kadhia ka hii ya Dar-es- Salaam,kesho yake mtu hana kazi. Mtamuita dikteta au vyovyote mtakavyo lakini watu wanjua bwana mkubwa hataki upuuzi.
  Matatizo hapo matatizo ni matatu:

  1)Wanaotakiwa kusimamia kampuni zinazo zoa uchafu ndo hao hao wenye kampuni hizo.
  2)Ukikuta ni kampuni ya mtu ambae kapata kazi kwa njia ya halali utakuta bei aliyoweka kufanya hiyo kazi ni 10% less of the budgeted price. Ngoma inakuwa inogile pale budgeted price inapokuwa ndogo ukilinganisha na ukubwa wa kazi.Hapo utakuwa ubabaishaji kwa kwenda mbele na kitu kidogo kitafanya kazi.
  3)Mwisho kabisa ni tabia za wana bandari salama.

  Kigali ukifika siku ya kwanza kwa jinsi mji unavyongaa utadhani huko Europe,ukweli ni mzuri japokuwa unauma. WANABANDARI SALAMA NI WACHAFU,TUNATEMA MATE HOVYO,TUNATUPA TAKATAKA HOVYO,TUNAJISAIDIA HOVYO KILA KITU ...............HOVYO HOVYO. Baadae tunamlaumu Kimbisa au Lukuvi, Wafanye nini?

  KUANZIA LEO UKIONA MTU ANATENGENEZA UCHAFU , kamata peleka polisi na kisha mpigie simu Lukuvi uone ka mji autapendeza. NIWAJIBU WETU KULIPENDA JIJI NA VIONGOZI WETU ITABIDI WATENDE KWA KUONA AIBU.

  TUWACHE KULALAMIKA NA KUPENDA KUFANYIWA KILA KITU.
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Almost 90% of CCM leaders are incompetent
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Oct 23, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Jaribuni kutembelea India muone uchafu......huo wa dar ni cha mtoto
   
 17. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #17
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135

  Very True...sasa swali ni what's next? Tatizo tumeliona...Je tunasubiri nini kifanyike? Nadhani tumefikia stage ya kujiuliza:....What i can i do for my country? Nadhani tukibadilisha muelekeo wa mawazo, hasa kuona hawa watu kama miungu midogo inayoziba maendeleo na badala yake kufanya kazi yao sisi huku tukijitangaza, tutachangia sana huo uwajibikaji. Au mnaonaje wakuu? It's time we put politics aside and have more action. Kila siku posts zimebeba ujumbe huo huo. Having knowledge is good, but the next question is what are we doing with it all? Maybe we shld look at how JF can play a part in bringing about a new movement....
   
 18. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #18
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kagame for EAC President
   
 19. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #19
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Magezi,

  Who cares about India? that is not our concern or our issue! Our issue is Dar, Tanzania.

  Yaani wewe umeongea kama Mkulo alipoulizwa kuhusu deni la Taifa kukua akadai mbona Zimbabwe deni lao ni kubwa kuliko letu!

  Damn it!
   
 20. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #20
  Oct 23, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  [quote
  Halafu.. Kwa sasa, japo hata mitaro tumeshindwa kuchimba na iliopo kuzibua, japo tumeshindwa kuzoa taka, japo hospitali za jijini hazina dawa, japo tumeshindwa kupata madawati kwa shule zote za msingi, tunashughulikia mradi wa barabara za juu kuondoa foleni (japo magari yaendayo kasi bado hatujaleta).

  'Sasa najua tuu JF mtachonga CCM haijafanya kitu. Hayo yote hamuoni?'
  [/quote]

  Tatizo wakazi wengi wa Dar hawaoni mafanikio tuliyoyafanya yatokanayo na mikakati yakinifu sambaba na mbinu endelevu na shirikishi za madiwani. Wengi wao kati yao wako JF ambapo ni mkusanyiko wa wasioipenda CCM na madiwani wake wanaoshinda kwa Tsunami. Lazima watu ndani ya JF mjue kuwa tunaondoa foleni sio kwa sababu watu wasipate msongamano na wawahi kazini la hasha, tabia yenu ya kuzomea viongozi imezidi, tumeona Ulanga juzi sasa tuna wasiwasi inasogea polepole kuja Dar, kuepuka hili barabara za juu zitakuwa maalumu kwa viongozi na wateule wachache walioonja pepo. Kwa kuanza tunafunga baadhi za Barabara kwa muda ili kurusu wateule wapite si mnaona feri hivi sasa na kwa hakika imeleta maendeleo.Hatuzoi takataka shauri ya kuimarisha utalii, unajua kunguru weusi ( wasio na Baka) ni ndege adimu, chakula chao ni takataka hivyo tukizoa takataka hapa mjini wale kunguru watakufa njaa na watatoweka duniani na watalii wataacha kuja kuwaangalia.Hatuna sababu ya kununua madawati, kwa jinsi hali ya maisha itakavyokuwa ngumu miaka kumi ijayo, watoto wetu na wajukuu lazima wameditate ili kuleta faraja kwenye maisha yao na huwezi kufanya hivyo ukiwa kwenye dawati lazima ukae chini, nyie wana JF mnaniudhi sana kwa nini hamuelewi vitu vidogo kama hivi. Kazi kuchonga tuuuu kwenye keyboard zenu mpaka vidole vinapata sugu, naomba mtuelewe.
   
Loading...