Kimbilio la Watanzania ni CCM pekee, wapinzani wanachanganya wananchi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,052
28,242
Wasalaamu!

Nikiwa kama mzalendo wa kweli wa Kitanzania na tukiacha mbwembwe za kisiasa napenda kuja na waraka wa kipekee kwa maslahi ya umma.

Utangulizi
Tanzania ni nchi inayokuwa kimaendeleo kwa kutumia rasilimali zake na kwa vyovyote vile inahitaji uongozi imara katika hili. Uongozi huu unapaswa na kutarajiwa kuwa wa kidemokrasia na unaokubalika ndani na nje ya Tanzania.

KUHUSU VIONGOZI NA UONGOZI
Sina shaka na namna viongozi na uongozi unavyowekwa madarakani haswa katika nafasi nyeti za Urais,Urais wa Zanzibar,uwaziri mkuu na nafasi nyinginezo za juu.

KUHUSU DEMOKRASIA NA VYAMA VINGI
Ni ukweli usiopingika kuwa tumerithi na kulazimishwa na dunia ya leo kufuata the so called democracy hivyo kwa namna yoyote iliyo bora ni lazima kama Taifa chini ya mataifa lazima tuoneshe kuwa tunafuata mrengo huo ulioasisiwa na walami ili tuendelee kuwa sehemu ya mataifa.

Mwalimi Nyerere aliliona hili na kuamua tufuate mkondo huu. Tume ya Nyalali ilionesha kuwa hatuhitaji vyama vingi lakini busara za Mwalimu ziliamua tueandane na mrengo huu ili tuendelee kuwa salama.

Vyama vingi vya siasa vilianzishwa despite kwamba wananchi hawakutaka wala kukubali (Tume ya Jaji Nyalali)

Hivyo ni ukweli usio na shaka kwamba vyama vya upinzani havikuanza kwa matakwa ya wananchi bali busara za viongozi. White paper report imesema wazi

Uzoefu wa miaka mingi toka 1992 umeonesha bila shaka Watanzania hawajawahi kuuamini upinzani kushika hatamu za kiuongozi.

MAKOSA YA KUJIRUDIA KWA WAPINZANI
Toka mwaka 1995 Wapinzani wamekuwa wakifanya makosa ya kujirudia ikiwemo kushindwa kuhamasisha jamii, kushindwa kuboresha hali ya wananchi, kupinga na kuharibu utamaduni wa siasa za Tanzania. Kuendelea na propaganda mfu za 'katiba mpya, tume huru, unyanyasaji, badala ya kuja na sera mpya zenye mvuto kwa wananchi.

WAPINZANI KUKOSA SERA MBADALA
Wengi wa wapinzani hawajawahi kuja na sera mbadala dhidi ya CCM na mara nyingi huwa wanasubiria sera za CCM ndio watengeneze sera zao.

KUSHINDWA KUSIMAMIA MASLAHI YA UMMA
Bado kuna ombwe kubwa kwa wapinzani kusimamia maslahi ya umma na kuwekeza katika itikadi sahihi kwa maslahi ya umma, yaani wapinzani wamegeuka kuwa chaka la kifisadi demokrasia. Hawana dira na misimamo ya nini hasa wanachotaka kukisimimamia. Mwisho wa siku wanabakia kurukiarukia sera za CCM, Matamko ya walami na kelele za walaghai na wazee wa fursa.

MZAHA WA KUONGOZA
Wapinzani wapo kwenye mode ya kujaribu kuongoza na hawana strategic plan ya kuongoza nchi. Wapinzani wote wanajikita katika dhima ya kuangusha CCM tu huku wakikosa nini watafanya baada ya hapo.

RASILIMALI
waapinzani hawana na wameshindwa kumobilize resources ili waweze kuongoza.wanajichanganya katika fursa za kujenga uongozi bora unaojipanga kuchukua Serikali. Kinachoonekana ni uhuni wa wapinzani kulink na walami ili kutengeneza njia mpya za kutafuna kodi.

MWISHO
Upinzani uliotegemewa kuwa mbadala wa CCM umeishia kuwa sehemu ya corrupt system na bahati mbaya au nzuri CCM ikaamua kujivua gamba, hili limeifanya CCM kuwa kimbilio la wananchi.

Kwa upande wa wapinzani wameendelea kuwachanganya wananchi kwa kukosa msimamo wa nini haswa wanachosimamia.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Hapo zamani za kale CCM ilikuwa na itikadi na mwelekeo. Ilivipoteza vyote ilipolaaniwa na Kolimba.

Yawezekana humfahamu Kolimba kwa sababu ulikuwa mtoto. Usiogope kumuuliza Mwl Bashiru, anamfahamu.

Usimuulize Katibu Mkuu wa CCM, si ajabu hata yeye hamfahamu pia!
 
Hapo zamani za kale CCM ilikuwa na itikadi na mwelekeo. Ilivipoteza vyote ilipolaaniwa na Kolimba.

Yawezekana humfahamu Kolimba kwa sababu ulikuwa mtoto. Usiogope kumuuliza Mwl Bashiru, anamfahamu.

Usimuulize Katibu Mkuu wa CCM, si ajabu hata yeye hamfahamu pia!
yaani wewe umejiunga JF juzi halafu unataka kuongelea habari ya Horace Kolimba?
 
Maccm na ujinga wao
EjFv_zlX0AIYopC.jpg
 
yaani wewe umejounga JF juzi halafu unataka kuongelea habari ya Horace Kolimba?
Jf ndio nini? Jf hii inayotaka useme wanavyo taka watawala? Narudia katafute resources acha huu utopolo wa sasa wa Jf
 
Upinzani unazidi kuungwa mkono kadri siku zinavyosonga mbele!Hii inamaana tabaka la wajinga linapungua lakini wale wazee waliomuheshimu Nyerere na kuwa CCM damu nao wanapukutika!Kinakuja kizazi ambacho kimeshuhudia unyama wa CCM!
 
CCM ndio wanachananya wananchi hebu angalia wananchi walio wengi wanavyohangahika kutumia mitandao yao pendwa kisa imefungiwa na CCM
 
Back
Top Bottom