na Charles Ndagulla, Moshi
MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro Simba wa Yuda, ametamba kuwa hadi sasa hajaona mpinzani wa dhati ndani na nje ya chama chake ambaye anaweza kumngoa kwenye kiti chake cha ubunge kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.
Akizungumza na Tanzania Daima mjini hapa jana, Kimaro alisema wote wanaotajwatajwa kuwa wanajiandaa kugombea jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wale wa vyama vya upinzani hawakubaliki hata kwa wapiga kura.
Miongoni mwa waliotangaza kuwania jimbo hilo ni Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustino Kabla ya mfumo wa vyama vingi vya siasa Mrema alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM wakati huo likiitwa Moshi Vijijini.
Wengine ni Mkurugenzi wa masuala ya Halmashauri na Bunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, Mwanasheria wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crispin Meela na Dk. Benny Moshi wote kupitia CCM.
Kimaro, mmoja wa wabunge wanaojipambanua kuwa ni makamanda wa vita dhidi ya ufisadi, alidai hata kama watatoa rushwa kwenye mchakato wa kuwania kuteuliwa na chama kugombea ubunge na hata wakiingia kwenye kura za maoni kwa kuhonga hawawezi kumshinda.
Alisema wanaodhani kuwa atashindwa kwenye kura za maoni ndani ya CCM na kwenye uchaguzi wenyewe, waende wakazungumze na wananchi na ukweli wataupata huko.
Kwangu ni salama kabisa na hao wanaokwambia kwamba mimi nitashindwa kwenye uchaguzi mkuu wanakudanganya. Kwa kifupi nakwambia hakuna mpinzani kwangu na hata wakitoa rushwa kwenye kura za maoni wataishia huko huko, alitamba.
Kauli ya Kimaro inatafsiriwa na wengi kama ni kujibu mapigo kutokana na kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Mrema kwamba jimbo la Vunjo ni mali ya TLP katika uchaguzi mkuu ujao na kujipa matumaini ya chama chake kuwa na angalau jimbo hilo moja kwenye uchaguzi huo.
Naye Mrema wa CHADEMA, amepuuza kauli hiyo ya Kimaro na kuiita kama ni ya kutapatapa kwa kile alichodai kuwa mbunge huyo hajatimiza ahadi zake kwa wapiga kura waliomwamini na kumpa ubunge mwaka 2005.
Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mrema alidai Kimaro atapimwa na wananchi kwenye uchaguzi huo kwani hivi sasa amegeuka kuwa mtetezi wa watu wenye uwezo na si wananchi waliomchagua.
Wanaoamua nani awe mbunge wao ni wananchi na Kimaro hawasaidii tena wananchi waliomchagua badala yake amekuwa mtetezi wa matajiri bungeni na kama unataka ushahidi tunao tutakupa, alisema. Alisema wananchi wanataka kupata taarifa kutoka kwa Kimaro jinsi yalivyotumika mamilioni ya fedha yaliyotolewa na wahisani mbalimbali kwa ajili ya kusaidia benki za kijamii vijijini maarufu kwa jina la VOCOBA. Mrema alisema hadi sasa mradi huo wa VOCOBA hauna maelezo ya kina na jinsi fedha hizo za wahisani zilivyotumika huku akidai kuwa kuna mchezo mchafu umetumika kwenye matumizi ya fedha hizo.
Source: Tanzania Daima.