Kimara, Dar: Mgombea wa CCM Udiwani, apita bila kupingwa

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam John Kayombo amemtangaza Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Pascal Manota kuwa mshindi katika uchaguzi mdogo ulioitishwa nchini katika Kata ya Kimara.


Kayombo amemtangaza Manota kuwa Diwani Mteule kutokana na madiwani wengine kutoka vyama upinzani kushindwa kujibu hoja za mapingamizi aliyowawekea kama mapungufu wakati wa ujazaji wa fomu.


“Vyama vilivyoweza kuchukua fomu ya kugombea Udiwani katika Kata ya Kimara ni , ACT-Wazalendo, Chadema, CUF na CCM lakini kutokana na mapungufu yaliyojitokeza katika ujazaji wa fomu Pascal Manota namtangaza kama Diwani Mteule aliyepita bila ya kupingwa,”amesema Kayombo.


Kwa Upande wake Manota ambaye ni Diwani Mteule katika Kata ya Kimara amewetaka wapinzani kuacha siasa za uongo za kuwasingizia watendaji kuwa ndio wanaharibu uchaguzi wakati wao ndio wa kwanza kuvunja taratibu za uchaguzi na sharia zilizowekwa.


Amesema wagombea wote walichukua fomu na zikajazwa na kubandikwa katika mbao ya matangazo katika Kata, hivyo baada ya kuona mapungufu ya wagombea wake aliamua kuwawekea mapingamizi.Kutokana na mapingamizi hayo wagombea wote wametupwa nje.


Amesema kuwa sasa anasubiri kuapishwa ili aendelee kuwatumikia wakazi wa Kimara na hatimaye wapate maendeleo ya kweli kupitia Serikali ya CCM inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli.
 
Mbona hata huku Tarime kata ta turwa mungombea Wa CCM Amelita bila kupinga inaama Chadema haikuwepo kweli? Au ndo mkakati Wa kufuta upinzani ndio umeeanza
 
Jiwe limejizatiti ndiyo maana limesema kwa kujiamini CCM itatawala milele. Hategemei kura zenu na ushindi wake utakuwa wa kishindo.
 
*Chama Cha Mapinduzi* (CCM) *imepita bila KUPINGWA* katika *kata* mbili za *KOLO* na *WANGI.* Dodoma kulikuwa na kata tatu za uchaguzi.
 
*Chama Cha Mapinduzi* (CCM) *imepita bila KUPINGWA* katika *kata* mbili za *KOLO* na *WANGI.* Dodoma kulikuwa na kata tatu za uchaguzi.
You should all be ashamed !!
Kama una akili timamu huwezi kutamba wala furahia upumbv huu unaofanyika !! Ipo siku, under this sun mtalipa dhambi hizi hapa hapa duniani, na tutahakikisha nyie ndo wafungwa mnaofanya ujenzi huku tukiwapiga mabuti..!!
 
Mmeshasema nyie ni wa milele!!! kaeni hivyo hivyo lakini siku zote Mwenyezi Mungu ajalibiwi!!!!!!
 
TAFSIRI YA KUPITA BILA KUPIGWA NNI....A. CCM INAKUBALIKA SANA,B. DEMOCRASIA NI FINYU KWA VYAMA VINGINE KUSHIRIKI UCHAGUZI C. NI SIFA TU ZA KIJINGA
 
Sawa ,na 2020 pia mtapita bila ya kupingwa hakuna Tatizo ila mkumbuke tu kila kinacho fanywa/kufanyika kina Matokeo yake ..
 
Kupita bila kupingwa ni sawa na mwanafunzi ajitungie mtihani then afanye bila usimamizi kisha asahihishe yeye uho mtihani
 
Yaani masisiemu bila aibu yanatangaza ymepita bila kupingwa aiseee,kweli ukiwa sisiemu lazima uwe na akili za KIBASHITE.
 
Hawana aibu hata kujisifia? Aibu kwa chama tulichotarajia kingesimamia haki kinaongoza dhuluma dhidi ya raia wake
 
Back
Top Bottom