Kimara: Dada wa kazi adaiwa kumnyonga mtoto wa miaka 8

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
15,091
16,125
Mtoto.JPG

Picha: Mtoto Erickson Kimaro enzi za uhai wake

Mtoto Erickson Kimaro mwenye umri wa miaka nane amedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na msichana wa kazi nyumbani kwao Kimara Temboni Dar es Salaam.

Inadaiwa Mfanyakazi huyo wa ndani alifika kwenye nyumba hiyo ya mwajiri wake siku ya Jumamosi 28 Mei, 2022. Ameshinda siku ya Jumapili nyumbani na Jumatatu Mtoto alivyorudi kutoka shule mfanyakazi huyo akamnyonga mpaka kufariki dunia.

Inadaiwa waajiri wa huyo binti walikuwa bado hawajamfahamu Vizuri binti huyo kwasababu ya kuwa busy tokea afike kwenye nyumba yao. Mama ni Daktari wa Moyo Hospitali ya Temeke, huku Baba akiwa ni Daktari wa Wanawake Hospitali ya Mloganzila.

Inadaiwa binti baada ya kumuua mtoto huyo, alimpigia simu mama mtoto mida saa 11:30 jioni na kumweleza kuwa mtoto anaumwa na anashindwa kupumua vizuri. Baada ya Mama kufika akakuta mtoto ashakuwa wa baridi kichwani ila kiwiliwili cha moto, baada ya mtoto kukimbizwa Hospitali ya Mloganzila ilithibitika ameshafariki dunia.

Shahidi anazidi kuelezea kuwa Binti wa kazi alichukuliwa na Jeshi la Polisi na bahati nzuri nyumba ilikuwa imefungwa Kamera za ulinzi na walipoangalia waliona kuwa Binti wa kazi ndiye aliyehusika na mauaji hayo kwa kumnyonga mtoto huyo asiye na hatia.
 
Mama ni Daktari wa Moyo Hospitali ya Temeke, huku Baba akiwa ni Daktari wa Wanawake Hospitali ya Mloganzila.
Watu wako busy na maisha huku jamii ama familia ama Taifa likipata malezi ya wadada wa kazi ambao wanalambishwa ama wananyonyeshwa nyuchi za wadada wa kazi JAMANI.

Kadi ya benki huwezi amini ukamuachia mdada wa kazi Ila mwanao unamuachia.

Yes, ni high social status kwa nje kuwa wote ni madaktari mko bize na hela ili watu waishi kifahari Ila Sasa malezi ya watt ni zaidi ya hela sema Sasa watu hatulewi.

Kila mtu Ana kipaumbele chake Cha maisha,eti baba akifa ama akisimama maisha ya mtt/watt yatakuwaje. He hujawahi jiuliza mkifa wote watt wataishi vipi.

Yaani Yale mayai ya kienyeji na maziwa ya ng'ombe wa kienyeji anywe mdada wa kazi halafu mwanangu akose lishe mbovu kisa hela.

Yaani ke anayafanya kazi huwezi kuwika ndani Mana anakuambia Niko bosi kata simu nitakucheki kumbe amekalia mfupa nyama.

Jamani maisha ni kuchagua.

Baada ya hapo poleni Sana madaktari kupoteza MTT mpendwa wa pekee kifo Cha MTT kimeniuma pia napata picha Kama mzazi namie Nina wanangu.😭😭😭😭😭😭😭😭
Hapo juu nu mtizamo wangu na usifanywe kuwa mtizamo wako na usitumiwe kama ushauri kwa mwingine kuchagua maisha yake. Kila mtu Ana maisha yake ambayo anayaota akiwa mdogo so please yaishi usiishi ya mwingine Kama huyu mjinga keisangora kwako Ila kwake ni mjanja.
 
Kweli kusoma sio kuwa na akili ngoja niishie hapo.
Wote harusi ya madaktari wenye bachelor hata kitanda kinalaliwa na madaktari wawili yaani kitanda tu ni sawa na doctorate mbili. Kumbuka md ya daktari ni sawa na PhD za kozi zingine.
So ni high status siku ya kufunga ndoa unaosha Sana mmeoana wasomi wote Tena madaktari wenye gpa first class.
Yaani mie na masters yangu mke wangu lasaba yaani nikinunua Sato hapa kamanga feri najua mwanangu lazima atapata supu ya kutosha na sio mdada wa kazi.yaani kulea familia nako ni Jambo la maana kuliko kuwa na kazi ya kulipwa mamilioni
 
Siku hizi utawasikia hawa Wadada wanatoa ushuhuda wa ajabu ajabu kwenye haya Makanisa holela.

Sijui kama Mamlaka wanajua madhara ya hayo. Unakuta Binti Mdogo anatoa ushuhuda wa mambo mazito ya kula nyama za Watu n.k...hivi leo ndio hao watakuja Majumbani watafanya hayo hayo wanayoyashuhudia huko.

Tuendekeze tu haya Makanisa yanayoeneza mambo ya kufikirika huku mnasahau kuwa mnatengeneza Ma Vampire....Kama kweli huyo Binti kamuua Mtoto kama huyo na bado akawa na guts za kusubiri hapo hapo basi ujue hata ukimuuliza atakwambia alijisikia tu kuua.
 
Back
Top Bottom