Kima cha chini cha mshahara: Tsh 135,000/= | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kima cha chini cha mshahara: Tsh 135,000/=

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zemu, May 11, 2010.

 1. Zemu

  Zemu JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 517
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  WANA JF, JE KIMA CHA CHINI CHA MSHAHARA CHA TSH 135,000/= MNAKIONAJE? TAARIFA ZISIZO RASMI ZINASEMA SERIKALI IMEGOTEA HAPO HAITAKI KUPANDA HATA KUFIKIA 150,000/= NA KODI WAMESHUSHA KWA ASILIMIA 1 TU. KAZI KWELI KWELI:mad2:
   
 2. amanindoyella

  amanindoyella Senior Member

  #2
  May 11, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  135,000 ni kidogo mno ndo maana watumishi wanakula rushwa kupita kiasi! Kilekile cha 315,000/= angalau kinaweza kutusukuma! hebu fikiria unga wa ugali ni tshs 800/= kwa kilo, sukari ni 1600, mchele ni 1600/= je ukipewa 135,000 itakufikisha siku 30?
   
 3. N

  Nacho cha Ruwa Member

  #3
  May 11, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kubwaga manyanga tu
   
 4. masharubu

  masharubu Senior Member

  #4
  May 11, 2010
  Joined: May 5, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani mnataka muambiweje na mukulu kesha sema hata mkae miaka 8 mshahara huo mnao taka hamuupati ng'oooo. Sidhani kama anaweza kutafuna maneneo yake, tunashukuru kwa hicho pia, kwani asie shukuru kidogo hata kingi hawezi kushukuru
   
 5. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hulipwi ili utimize mahitaji yako,unalipwa kulingana na makubaliano yako na mwajiri na kulingana na uwezo wako kuanzia kielimu mpaka kiutendaji. Kama mtu anaona mshahara wa kima cha chini cha 135,000 kidogo basi aangalie utaratibu mwingine.

  Mahitaji ya mtu hayaishi,muhimu serikali iangalie kiwango cha mishahara inayolipwa na nchi nyingine zinalolingana na zetu kwa elimu kama za waajiriwa wake. Kwani kama matumizi ya mtu kwa mwezi ni Tshs 10,000, mtu alipwe kiasi hicho hicho ili kutimiza mahitaji yake? Mtu alipwe kutokana na utendaji na elimu yake.
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Ni uhuni tu yeye Hawa ghasia analipwa posho shs ngapi???
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu na wewe umepinda..... kaulizie mshahara wa PhD holder DRC alafu uniambie.... Mkuu wanasiasa na watawala wanajali zaidi matumbo yao na familia zao. Ukisema eti mtu analipwa kulingana na elimu na uwezo, sawa lakini kuna kitu kingine kinaigina hapo kwamba kama binadamu kuna vitu ni lazima uvipate kulingana na gharama za maisha zinavyo panda na kama mtu huyo havipati lazima atatafuta njia mbadala ya kuvipata na diyo rushwa inaingia hapo au wizi wa mali ya ofisi.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  May 11, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kiwe ni kwa ajili ya idara, taasisi na mashirika yote ya UMMA. Vinginevyo malalamiko yako palepale. Chunguzeni muone baadhi ya taasisi za serikali wanavyolipana kwa kufuru ya hali ya juu wakati hawazalishi chochote. Ulizeni TPDC, EWURA, REA, TCRA, DAWASA, DAWASCO, NSSF, PPF, TANESCO, SUMATRA, TRA, TANROADS,..... Ulizeni kima cha chini huko ni shilingi ngapi
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 711
  Trophy Points: 280
  ni mdogo sana
  sasa 135 ndio nini sasa wakati kwa wafanya kazi laki nne ukiwalipa 315,000 jumla ni trilion moja na usheee

  na si kama k alivyosema siku ile

  ni wezi tu dawa yao hawa ni kuingia barabani
   
 10. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  haya bwana let them suit themselves. Tutatafuta njia mbadala ya kuongeza kipata, be it dodging from work and concentrate on busines ama anything that comes around.
   
 11. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi ktk hili nashindwa kuelewa.
  Majibu naona yanawzekana ya kwamba kama mshahara hautoshi una uhuru wa kuacha kazi , ama kama unaona ajira hiyo ni haki yako ya msingi mwondoshe mwajiri wako, na kama unaona ni vigumu kumwondosha mwajiri wako gomeni wafanyakazi wote musi-andamane mnakaa tu majumbani mwenu kwani ffu watawatafuta majumbani?

  Mkifanya hilo hakika mwajiri wenu lazima atie adabu, lakini kuwaza kula rushwa eti kwa sababu ya mshahara mdogo wakati uwezo unao hii ni daganya toto labda mseme tu mmepata njia ya kuhararisha kuisema rushwa wazi wazi kwa sababu imo ndani ya damu.
   
 12. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Maisha bora kwa kila mtanzania ndo hayo,

  Hata tunapoteza muda kujadili keshasema habebembelezi kura zetu,

  hajui kuwa mimi nyuma yangu kuna ndugu zangu zaidi ya 10 wanategemea mshahara huo niwamegee japo kidogo,

  nikiwaambia msipige kura kwa huyo jamaa, atapata ngapi?
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mkuu nini maana ya minimum wage????????
   
 14. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndo ilitakiwa kufanyika
  Wafanyakazi wakiamuwa wanamtoa JK ktk uongozi maana wao wana access na wananchi hadi vijijini, mfano walimu. walimu wa shule za misingi ndo wanasikilizwa kule viviji kwetu. Sasa binafsi nashindwa kuelewa nguvu zinazotumika. Ni ukweli mtupu wafanyakazi ndo wanaoamuwa nani awe Rais na nani asiwe maana ndo hao hao wasimamizi wa kura ktk kila kituo cha kupiga kura na ndio hao hao wanaojumlisha kura. Kimantiki siwaelewi hasa baada ya JK kusema mshahara hautekelezeki na kama kura wamnyime, sasa wanalalamika nini bado??
   
 15. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Haki ya nani hii ID Ya Mponjoli huyu ni kapuya ndani ya JF. Sasa sikiliza Kapuya, sasa nisikilize kapuya nimekukamata tunajua elimu ipo pale na ndio maana sio wote wanaodai hiyo mishahara wanalipwa hiyo wapo wengine wanalipwa mpaka dola 6000 kwa mwezi ila wana uchungu na watu hawa wanaolipwa kima cha chini. Wewe kwa akili yako unadhani Mgaya analipwa laki laki moja na nini hiyo unayosema? ni uchungu wa nchi na wenzetu. Unajua Kapuya kusoma ni bahati tu kama bahati zingine na wewe ungeweza kujikuta hujasoma lakini sio kama huna akili. Hivyo elimu isiwanyanyase wananchi, au kaka maprofessor nao walikuwa wanadai laki tatu hiyo?
   
 16. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lazima uwe na uchungu wa nchi yako na watu pia.
   
 17. c

  chochamagesa New Member

  #17
  May 11, 2010
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  sijui kama mhe.alisoma na kuelewa kilichokuwa kimeandikwa kabla ya kutoa hotuba kwa hao aliodai ni wazee wa ccm na kama ndivyo akili ya hao na yeye aliyesoma itakuwa na walakini na haina tofauti na akili kwenye attachment hii:A S 100:
   
 18. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Matokeo ya empty promises wakati wa kampeni ni pamoja na haya ya mishahara, watu tunaweza kusema JK hakuahidi kuongeza mishahara lakini ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania ilibeba maana kubwa sana ikiwa pamoja na hili la mishahara, watu wanaweza kuwa wanapima maisha bora yaliyosemwa na rais in terms of mshahara wanaopata kwa mwezi na kujiona hawasongi mbele.

  Tuwe makini zaidi wakati tunatoa promises, unaweza kusababisha mtu asifanye kazi kusubiri ahadi iletwe mlangoni, promise ni mojawapo ya rewards, kama umeahidi mtoto wako utamnunulia baiskeli akifanya vizuri darasani usipofanya hivyo hatakuelewa hata kama kweli kwa wakati huo huna uwezo yeye atafikiri unafanya makusudi na inawezekana next time asifanye vizuri. Tuliposema maisha bora kwa kila mtanzania na sasa tunasema serikali haina uwezo kwa mtu wa kawaida hawezi kuelewa, therefore the government should take an extra care when making its promises to a desperate society like this.
   
 19. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  1 3 5 , 0 0 0
  | |
  3 1 5, 0 0 0

  Naona sirikali imeamua kuswap digit ya kwanza na ya pili, ie nafasi iliyokuwapo 1 wameweka 3 na nafasi iliyokuwapo 3 wameweka 1
   
 20. M

  Milindi JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,209
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 180
  Ndugu wana jamii kama JK alivyosema inatakiwa wafanyakazi wawe kama MBAYUWAYU,Maadam kima cha chini ndio hicho basi hiyo ni akili ya kuambiwa na SERIKALI,Kwa hiyo wafanyakazi wakichanganya na akili zao wenyewe(RUSHWA),Basi mwisho wa mwezi utapata zaidi ya laki tatu,ambazo TUCTA wamependekeza.Kumbuka Mkapa aliposifia kauli kuwa MTAJI WA MASKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE,Utekaji nyara na wizi uliongezeka huku waathirika wakivuliwa nguo na kulazimishwa kuimba wimbo huo wa mtaji wa maskini ni nguvu zake mwenyewe.
   
Loading...