Kim poulsen afukuzwe haraka kunusuru soka letu

lifeline

Member
Sep 10, 2013
63
9
Nimemfuatilia kocha wa timu yetu ya taifa kwa muda naona Hana jipya.Malinzi muondoe haraka sana.
 
Watu kama wewe nawashangaa sana! Afukuzwe Kwasababu tumefungwa na Kenya nusu fainali??
Au kuna sababu nyingine??
Afukuzwe halafu nani aajiriwe awe Kocha mpya??
 
Nimekutafutia tusi nimekosa kwani kocha ndiye alikuwa anapiga hizo penati timuimepiga mpaka penati saba halafu unalaumu kocha kwa nini usilaumu wachezaji waliokosa penati hasa ngasa na yondani kwenda zako.
 
Mi naona afadhali hata huyu wa sasa kuliko Maximo Maxime
 
Afukuzwe amekosa penati ya ngapi na afukuzwe kwa lipi,ebu tuambie mkuu?
 
Mi naona afadhali hata huyu wa sasa kuliko Maximo Maxime

Maximo alitufikisha hadi 84 kutoka kwenye 120 hivi katika viwango vya FIFA, huyu Paulsen katurudisha kulekule na sasa tupo 124--majanga! Hata kama Maximo hakuwa mzuri kivile, lakini huyu ni majanga zaidi. Takwimu hizo hapo!
 
Afukuzwe amekosa penati ya ngapi na afukuzwe kwa lipi,ebu tuambie mkuu?

Alipokuja alipewa jukumu la kutupeleka world cup, kashindwa! Yeye mwenyewe akaahidi atatupeleka AFCON, kashindwa! Akaahidi atatupeleka CHAN, kashindwa! Majuzi tu akaahidi atarejea na kombe la challenge, kashindwa! Kama huyaoni makosa, labda tutafute msaada wa miwani!!
 
Maximo alikuwa anapewa mechi za majaribio ambazo zilipangwa kufuata lkalenda ya FIFA.

Sasa hivi,kipindi cha Kim Paulsen TFF haitafuti mechi za majaribio za kutosha kwa ajili ya Timu ya Taifa.Tena TFF imekosa kuweka malengo kwa ajili ya timu ya TAIFA.

Wakati wa MAXIMO angalau kulikuwa na lengo la kuipeleka Taifa Stars kombe la Dunia.

Wakati wa Kim Paulsen malengo hayasimamiwi na TFF,kwa kuhamasisha washabiki wala kuiandaa timu kwa kupambana na timu zenye uwezo wa kuipima timu ya Taifa.

Sasa Jamal Malinzi, kipimo chake ni kusimamia malengo ya muda mfupi na muda mrefu,ili kuleta matokeo mazuri kwa Timu ya Taifa na soka kwa ujumla.

Tumeona wakati wa Maximo,TFF ikipanga,ikishirikisha wadau,wafadhili na kama nchi inawezekana.

Tuache,kauli zenye mwelekeo wa ushabiki wa timu kongwe ,eti mchezaji akikosa nidhamu,tunahoji ni kwanini kocha amemuacha.na washabiki kulazimisha fulani lazima acheze hata kama hana nidhamu.

Huwezi kuvuna kama haujapanda,lazima washabiki wavumilie na wafahamu udhaifu wa soka la Tanzania unachangiwa na vilbu vyetu kushindwa kuwa na mipango endelevu,kuwekeza vya kutosha, kukuza vipaji,miundo mbinu hata katika kuimarisha uongozi wa timu.
 
Hatuna talent. Period!
Hata Malinzi akimleta Arsene Wenger ni kazi ya bure tu sababu hatuna talent. Soccer imetushinda. Riadha zimetushinda. Labda tuanze mkakati wa kuimba ndio fani yetu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom