Kim Jong Un atangaza kusitisha majaribio ya Nyuklia

Duh!! Sijui kiduku kadanganywa nini mpaka kakubali, ila yote kwa yote naimani ni uamuz sahihi kwa pande zote hasa hasa korea kaskazini, maana ni wakat muafaka kwa wao kukuza uchumi maana kama teknolojia ameshakuwa nayo, ila hapa mmarekani alipaswa ahakikishe kiduku kaharibu kila kitu ila kwa hiv naona kapuliziwa tu sababu km mabomu anayo, teknolojia pia anayo, akishakuwa na uchumi mzuri itakuwa tabu.
Aharibu nini...?
 
Ameokoka na kumpokea yesu kuwa bwana na mokozi wa maisha yake....

Nimepewa tu fununu
 
Japan not satisfied with N. Korea’s nuke test halt, wants ‘complete & irreversible’ denuclearization

‘US will say they saved the world’ while peaceful Russian approach on N. Korea won – Moscow
Kim kahakikishiwa ushirika na Moscow kuwa hataguswa...! Marekani analiwa timing tu. Kwa sababu zana zake sasa ni obsolete kwa teknolojia mpya ya Russia ya kijeshi. Kama tu S-300 inawapisha kelele...nyingine je?
=========
“If North Korea gets guarantees for its security and the threats to it from the West stop, then naturally the denuclearization of the region will happen,” Chepa told Inerfax. “That is what Russia and China have been always talking about, and today the program suggested by them is practically being implemented.”
 
Unaposema Kiduku anawalia Timing ina Maana
Marekani analiwa timing tu...haimaanishi Kim anawalia timing peke yake!
una Akili na Unamjua Sana Kim Kuliko Mike Pompeo
Haya si mambo ya akili tu ni pamoja na kuangalia 'facts' na kusoma mwenendo wa matukio yanavyotokea. Pia ni kuhakikisha unatafuta taarifa zisizo 'tango pori' na kuzichambua. Ingawa kwenye taarifa za tango pori unaweza kufanukiwa kugundua lengo la mleta tango pori. Na hiyo ikakupa mjumuishi wa kujua kinachojiri ama kitakacho jiri. Kwa kifupi hivyo ndiyo nifuatiliavyo masuala ya ulimwengu. Kuna uwezekano mkubwa na wewe unanjia zako zakujua ya ulimwengu huu.
Trump na Wenzake
Trump na wenzake wamechanganyikiwa....Russia kawachanganya (kuanzia kiteknolojia za kijeshi mpaka kwenye kujieleza mbele ya Ulimwengu). Kinachofanyika ni kutengeneza mbinu za kuongeza 'approval' rating za Trump na serikali yake kwa ajili ya domestic consumption. Hivi hujiulizi, US na washirika walienda kuwapiga IS huko Syria toka 2013(chini chini) na 2014(waziwazi). Mpaka 2016, IS ilikuwa imechukua eneo kubwa la syria. Russia alivyotia mguu ndani ya miezi karibu 7, IS ilikuwa imevunjwa uti wa mgongo. Cha ajabu, juzi kati Trump anaibuka na kusema amewamaliza IS, what a joke?!

Tukirudi Korea, na kwa hili siwezi kushangaa, Trump na wenzake wakiibuka kuwa vikwazo na maneno makali ndiyo yamemfanya Kim atuletee tamko hili. Hivi, Marekani unayoijua ingekuwa kweli na ubavu kwa kauli kali za Kim kuipiga US, zingeisha siku mbili hawajashmbulia Korea? Kutamka hadharani kuwa utaishambulia marekani ni sababu tosha ya Congress kuidhinisha fedha na vita dhidi yako. Kwa nini waligoma kumshambulia Korea? Kuna tatizo mahali.
Ukweli unabaki Pale pale hakuna Anayejua Kim aliongea nini na Xi Jin Ping
Hakuna anayejua Kim aliongea nini na Pompeo
Ya kukutana na Xi, naweza kukubalia mana kuna facts (ushahidi) lakini ya Pompeo bado nina wasi wasi kama jambo hili lilifanyika ana kwa ana!!!
Unaweza kuongea wee kumsifia kim At the end of the day ukashangaa Kim anakabidhi makombora Yaharibiwe Hadharani...
Au uje kushangaa kim anakubali US ajenge Airbase kule Pyong Yang...

Weka akiba ya Maneno uone nini kitatokea...Muda unakuja Tutaona na Kusikia
Jambo linalowaangusha waangusha analysts wengi wa masuala haya ni kutumia hisia kujenga hoja. Facts na ushahidi ndiyo habari ya 'mujini' kwenye kuelekea kuwa analyst anayeaminika. Kwa maelezo yako hapo juu ni hitaji facts na ushahidi usiotiliwa shaka kuyakubali kama yanaweza kujiri ama la!

Karibu, Mkuu.
 
Mkuu Umenifurahisha Sana Eti "Hamna mashoga Mule"

Nikifikiria North korea na Ubabe wote ule.....Kim Jong Un aliyekuwa anatukana Matusi mpaka ya Nguoni Viongozi wa USA leo amelainika kama Peanut Butter...

Tatizo watu wengi wakisikia USA wanadhani Ni ile Wanayoiona kwenye BBC swahili + VOA

Time will Tell lazima North Korea Aharibu. Au akabidhi Silaha za Nuclear Hadharani... Hicho ndicho USA wanataka na Mambo yameanza kwenda Spidi spidi baada ya China Kuanza kutikiswa Kibiashara...

Kwani we Ndugu hiyo habari umeielewa vipi???!!! Yaani kwa mawazo yake unafikiri KIM Jong Un ameogopa???!!!!
 
Hii situation ni kama kucheza chess, the more you make the right moves the more the chances of winning a game.

NK walisema watakaa wazungumze pale waki achieve mission yao, kitu walicho fanikisha.

Na mazungumzo wanayo yataka ni kutambulika kama taifa lenye nguvu ya nuclear.

Watu wanaliangalia hili swala kiushabiki baadala ya kujiuliza kwanini NK anataka mazungumzo sasa.
Na je majaribio yake yalikua success au failure!?!?
 
Kuna watu Wana Mawazo mgando masuala kama haya hayaitaji ushabiki kama wa Soka .
Leader Kim Jong Un anajua akifanyacho sababu Tabia za Hasimu wake Mkubwa U.S ana kariba gani We Unajua kilichokwenda kuzungumziwa China na Kabla ya Trump kukutana Kim jong un Huenda Xi jinping akatembelea Pyongyang Lakini miye nikionacho kuwa Tayari washatimiza Lengo la kwanza la Kuwa Neuclear state hii ikiwa na maana kuwa Hakuna tena haja ya Kuendelea kujitenga na wengine hasa kiuchumi Njia Rahisi ni kutofanya majaribio ambayo Yamekuwa yakipingwa ambayo yaliwafanya waonekane ni Taifa linalo leta hofu duniani ingawa Hawa wajiitao Jamii ya kimataifa ndiyo wamekuwa wakieneza uzushi huo
 
U.S.A bado yeye mwenyewe ni kunguru tuu ushabiki ulikua mkubwa sana walivyoshambulia Syria kuja kufatilia undani wa habari kumbe kabla ya kufanya shambulizi lenyewe walimpigia simu RUSIA baada ya RUSIA kutoa ridhaa ndio wakatekeleza shambulio. Achana na hiyo waangalizi wa kemikali wameenda RUSIA kazuia wazi wazi huyu mbabe vipi? Kwa nini asitumie tena ubabe wake kulazimisha kuingia? Kitendo cha North Korea kukubali kusitisha uzalishaji sio cha kufurahia cha kufurahia kilikua ni endapo North Korea angekua amekubali kuharibu maeneo ya uzalishaji wa makombora.
Syria kashambuliwa bila Russia kujulishwa.Lete source kama unayo
 
Syria kashambuliwa bila Russia kujulishwa.Lete source kama unayo
Kaangalie post Na.27 kuna link inayoonyesha uwepo wa mawasiliano kabla ya kufanyika kwa shambulizi husika na uwepo huo wa mawasiliano ndio kulikoifanya UK kukubali kujiunga kwenye shambulizi husika.
 
Siyo mimi niliyesema,ni USA ndiye alosema
Ila ukumbuke tuu kuwa pale kuna Red Line Zone ambayo U.S wala RUSIA hawezi fanya mashambulizi bila kumtaarifu mwenzake ili kujaribu kuondoa athari kwenye mali za jeshi la mwenzake. Ila fatilia pia mahojiano ya Al Jazeera na Sergey Lavrov waliyorusha leo-ameongelea suala hilo pia la kupewa taarifa kabla ya kufanyika kwa shambulizi.
 
Kim ana akili sana kwa faida ya raia wake ni bora aache malumbano na USA kwa ishu ambayo ataifanya hata miaka ijayo maana knowledge wanayo mwezi ujao anakutana na Trump kikao kitakua safi kwa wote na kuondolewa baadhi ya vikwazo kama sio vyote ili kukuza uchumi wao...
 
Back
Top Bottom