abubakar MT
Senior Member
- Jul 31, 2017
- 139
- 230
Zaidi ya tani laki mbili za Ufuta zenye thamani ya zaidi ya 570mil hazijulikani zilipo baada ya kuondolewa kwenye maghala mbali mbali ndani ya Wilaya ya Kilwa.
Thamani hiyo ni tofauti na mzigo uliokamatwa wiki hii ambapo jeshi limefanikiwa kukamata ufuta tani 32 wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80 ukiwa unatoroshwa kutoka chama cha Msingi cha ushirika Linali kata ya Likawage wilayaya Kilwa .Baada yataarifa hiyo Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mhe.Christopher Ngubiagai amwagiza Mkuu wa polisi Wilaya ya Kilwa(OCD) kuukamata mzigo huo na wahusika wote waliohusika kutengeneza nyaraka zisizo halali kukamatwa na kufikishwa mahamani.
Huu ni mchezo mpya tulio kwisha usahau masikioni mwetu ambapo kwasasa Maafisa msingi vya ushirika wakishirikiana na Wafanya biashara wasio waamifu kuanza tabia yenye lengo la kuwaibia wananchi ambapo mpaka sasa zaidi ya tani laki mbili zenye thamani ya zaidi ya 600 mil zimeripotiwa kuibiwa katika maghalambali mbali ndani ya Wilaya ya Kilwa.
Taarifa za Wizi na Ufisadi kwenye halmasauri zetu tulishaanza kuzisahau, lakini kwa taarifa hii ni doa chafu kwa serikali ya JPM huenda ni kwasababu yaonyesha Mh Raisi kaanza kuonyesha Upole katika kuwachukua Maamuzi magumu.
Source: