Kilosa: CCM na CHADEMA wazichapa toka saa tisa usiku, majeruhi wapelekwa hosp ya wilaya

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Usiku wa kuamkia leo kumetokea mapigano makali kati ya ccm na cdm katika kata ya Masanze katika kitongoji cha Mapekenya na kusababisha kuumizwa na kulazwa kwa wafuasi wa CHADEMA katika hospitali ya wilaya ya Kilosa.

Hali hiyo ilianza mara baada ya CDM kuwafumania wakigawa rushwa na kuchukua kadi za kupigia kura kwa kuzinunua na kuwatia ndani hao watuhumiwa. Ndipo simu zikapigwa mjini kilosa vijana wa green guard wasiopungua 20 na kuwamwaga eneo la tukio na kuwashambulia wafuasi hao wa chadema waliokuwa wamewakamata ccm kwa rushwa.

Hii imekuja ikiwa kuna tarajiwa kuwa na uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo hapo kesho
 
mmmmh tukizishinda mbinu hizi kesho ccm hawana chao, pole sana kwa makamanda wote waliojeruhiwa
 
Kazi ya Mwigulu na Kinana. Ipo siku

ndio mbinu mpya waliyogundua hiyo mkuu ya kudeal na wapinzani,matatizo ccm wanayoya create sasa hivi chini ya hii sekritarieti mpya ya kinana na mwigulu ni maafa makubwa kwa taifa letu hili changa.
 
Hii nchi itaingia machafukoni kwa gharama ndogo sana... Naamini gharama ya kuendesha hili jeshi la CCM ni ndogo sana, ila wanafaidika na umasikini wa vijana nchini...
 
Kamanda wa Green guard...
mw1.jpg


Hongera Mzee...
 
Kamanda wa Green guard...
mw1.jpg


Hongera Mzee...

Ndio maana ya hiyo nyota nyekundu kwenye kofia. Kwamba LAZIMA DAMU IMWAGIKE KUINUSURU CCM. Hii ndiyo ilikuwa maana ya hii rangi wakati Wachina wanapambana na Ubeberu wa Magharibi.

Hivyo tuliyategemea haya kutoka kwa Mwigulu. Ila siku yaja naye atakionja kikombe hiki.
 
Tutashinda tu. Poleni sana makamanda mliojeruhiwa na hao janjaweed.
Hayo ndio matokeo ya kambi ya green guard huko Mbeya.
 
mmmmh tukizishinda mbinu hizi kesho ccm hawana chao, pole sana kwa makamanda wote waliojeruhiwa

bila shaka hao waliojeruhiwa watakuwa si makamanda. ni vyura wa chadema. kamanda huwa hashambuliwi na kujeruhiwa kirahisi tena na greenguards
 
Hiyo green guard itawezaje kuitawala umma ya watanzania? Kwani serikali haijui kuwa watanzania walishafunguka macho? CCM acheni uharamia. Watanzania wameshachoka kupita kiasi.
 
Naona KINANA amehamishia mbinu zake za ujangili dhidi ya tembo kuikabili CHADEMA. Na huo ndo mtaji wa mwisho wa CCM.Baada ya hapa ni mazishi ya CCM.
 
Ndo maana wabunge wote wa CCM walichangishwa pesa kwa ajili ya kufadhili hawa wahalifu pia kugawa rushwa. Lakini iko siku Tanzania na Tanganyika iliyobora yaja.......tuvumilie mateso bado kitambo kidogo tu na muda ndo Hakimu mkubwa kuliko wote hapa duniani!
 
Tutashinda tu. Poleni sana makamanda mliojeruhiwa na hao janjaweed.
Hayo ndio matokeo ya kambi ya green guard huko Mbeya.

Ndugu mwita, Nachelea kusema kwa nini na vyama vya upinzani visianzishe Guards zao ili kupambana vizuri kivita kama kisiasa imeshindikana?. Naona Polisi wamekuwa wachache na wanatumiwa hivyo inaweza ikawa ni jukumu la kila mmoja kujilinda kwa kuchukua hatua mkononi.

Hata hivyo nikutakie maandalizi mema ya mapambano Hapo kesho katika sanduku la kura bila kusahau kuendelea kuwahamasisha wapiga kura wa hapo kata ya jijini.
 
Back
Top Bottom