Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Nimekuja na uzi mwingine, ukiona mtu kapost chassis namba ya gari na ile gari kaiagizia Befoward.. ichukue ile chassis number kama ilivyo igoogle, ilegari itakuja kama ilivokua listed na Befoward wakati inauzwa ikague zile picha nenda mpaka kwenye picha inayoonesha odometer reading utacheka ufe.. nakupa mfano gari hii apa chini naipost.. na nnaenda kuitafuta befoward ilivokua listed. Jaman tuache ukitonga na uvivu wa kutafta maarifa mapya, haya magari tuyaagize wenyewe tu hakuna mateso yoyote unayoweza kuya pata kwa kusubiri meli ifike mwezi mmoja mpaka miwili.View attachment 1890299
Gari inauzwa na dalali wa kibongo anaandika uongo uongo. Ukiichukua hiyo chassis namba ukaweka google ngoma zinakuja kama hivi chini cheki mileage halisi ya gari, jamaa kaamua kuficha hiyo laki kasema gari ina 51000kmView attachment 1890301
View attachment 1890302
View attachment 1890303
View attachment 1890304
Asipoweka Chassis namba unafanyaje?
 
Ni fraud mbaya sana hizi kufanyika kwa level ya kampuni. Nakumbuka kuna jamaa yangu alininua IST Befoward akijua ni low mileage kumbe ducuments za inspection zimeonesha paper mileage ni kms 106,000 ila kwenye odometer gari ina soma 6,000kms na gear lever imechakaa kinoma , kapeti ya miguu karibu na accelerator pedal imelika kwa kisigino
Kuna jamaa yangu Kanunua Premio kwa mtu yenye namba C lakini ODO inasoma 45,000km.

Sasa sijui huko Japan lilitoka likiwa na zero kilometa au vipi!
 
Kwa tanzania hii ukinunua gari kwa kuangalia km ilizotembea au plate namba mfano D, utakuwa umepigwa kidole..

Watanzania wanacheza na mileage za gari na kuzishusha...

Unaweza kukuta gari uhalisia wake ni Km 180000 lakini wahuni wanachokonoa na kushusha moaka km 40000....
Boya akijichanganya anapigwa, anaenda kushangaa mbona gari lake halina performance nzuri kama magari mengine..

Kumbe kauziwa mkweche
Hata zinazouzwa kwenye showrooms za kibongo nazo zinachezewa millage. Jamaa wananunua magari yenye 150,000km huko Japan kwa bei chee wanayaleta bongo na kuyashusha millage hadi 55,000 au 65,000km.
 
Sure nilisahau kutaja na steering, imechubuka imekwaruzwa na pete kila upande, kuna jamaa yangu aliwahi kupigwa tena aliagiza gari Befoward ni Ist ( BH427758) ukizigoogle hizi namba itakuja hiyo ist wame list kuwa ilikua na 6000 kms, angalia kwa umakini sana picha zake, speedometer inasoma buku 6, jamaa akashawishika akanunua.

Gari imefika bongo shoo ya kwanza ina miss za hatari ikiwashwa inatetemeka kama generator na imechoka kupita kiasi inatoa moshi mweupe .

NB. Gari ilinunuliwa mwaka jana (Kipindi gari zinakaguliwa Japani) .Sasa bas gari baada ya kuinunua zile document za Inspection report walivyo zi upload kwenye CAP, ndo zikatusanua kuwa gari ilikua na kilometer 106,000 km (paper mileage) ila kwenye actual mileage wakafuta 10 ikabaki 6000 ndo ina display ( wanasemaga ni ku cloack mileage).. ikabidi ni mueleweshe mshkaji gari kapigwa na wajapan ..angalia hiyo inspection report ya japan nime attach hapo chini..

Gari iko kwenye meli inakuja bongo tukaanza kuchapana email na beforward full kuchimbana mikwara ya kufunguliana kesi na kuikataa gari jamaa wana chomoa tu wana sema nao walinunua hivo hivo mnadani. Ikabidi jamaa aikubali tu kishingo upande baada ya kufika gari ndo alichoka zaidi na zile miss, plus pedal zimechoka, usukani umechoka, siti ya dereva kigodoro kimelala, gear lever imechubukaa ile silver .Ilikua ni balaa tu

Kwahiyo kupigwa hata nje unaweza pigwa piaa, lesson tujifunze ku pay attention to details sana , tuwe inquisitive na curious.

FOLLOW HII LINK kama itafunguka uone hiyo chuma

Mkuu hii gari ilikua ya 2003 yaani miaka 19 toka itengenezwe yenyewe ilikua wapj hadi sasa iwe na mileage ya chini ya laki moja?
 
Back
Top Bottom