Kilombero: Mwanamke ajifungua nje ya kituo cha Polisi baada ya kutolewa mahabusu

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
mama.JPG

Mwanamke mmoja Amina Rafael Mbunda (26) mkazi wa Kiswanya,kijiji cha Mgudeni,kata ya mwaya,Tarafa ya Mang'ula wilayani kilombero mkoani Morogoro,anadaiwa kujifungua nje ya kituo cha polisi baada ya kutolewa mahabusu alikokuwa akishikiliwa kwa tuhuma zilizomhusu mumewe aliyedaiwa kuhusika na ununuzi wa kitanda cha wizi.

Mwanamke huyo aliyelazwa kituo cha afya mang'ula alikopelekwa na kulazwa baada ya kujifungua,amedai alikamatwa Juni mosi na polisi,Mwenyekiti wa kitongoji na mwanaume mmoja waliofika nyumbani kwake,saa chache baada ya kuondoka mgambo waliokuwa wakimtafuta mumewe kwa tuhuma za ununuzi wa kitanda cha wizi,ambapo akiwa mahabusu licha ya kulalamika kuumwa uchungu,askari wa zamu alimpuuza hadi alipoona amezidiwa na kumtoa nje alipojifungulia kwenye nyasi bila msaada.

Mganga wa kituo cha afya Mang'ula,aliyetajwa kwa jina moja la Msomba ametafutwa kwa njia ya simu ili afafanue kuhusu afya ya mwanamke huyo na kichanga cha kike kilichozaliwa kikiwa na uzito wa kilo 3.5 kwa mujibu wa kadi yake ya kliniki iliyoonesha pia amejifungua kwa msaada wa ndugu,lakini simu yake iliita bila majibu.
Ulrich Matei.

Chanzo: ITV
 

MERCIFUL

JF-Expert Member
Oct 17, 2011
2,559
2,000
mbapo akiwa mahabusu licha ya kulalamika kuumwa uchungu,askari wa zamu alimpuuza hadi alipoona amezidiwa na kumtoa nje alipojifungulia kwenye nyasi bila msaada
Mwili unasisimka kwa hasira!! MOTO wa jehanamu utakamchoma huyo askari wa zamu, bado unachochewa:mad::mad:
 

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
8,557
2,000
Ungesema watanzania mkuu, Polisi ni cheo ndio maana ukivaa jezi watasema "Raia amejifanya Polisi"
Polisi sio cheo, ni wadhifa,
Pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, kuna baadhi ya mambo hawayafanyi sahihi, wanaonea sana RAIA wasio na hatia au kukuza mambo madogo, pia wanabambikia kesi watu.

Nb: polisi ni polisi tu hana urafiki ni wanaa sana.
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
42,695
2,000
AISEEEE "" ukitaka kujijua kuwa hauna dhambi ....basi fuatilia matendo ya police wa Tanzania....sasa angekufa hapo nje "" wange waambia nini watanzania ""....... Aiseee rasmi leo nimeona uzito wa ile kampeni ya kusaidia mama mjamzito inayofanywa na wizara ya AFYA ....."" police wa Tanzania "" ni wachawi "".....
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
60,002
2,000
AISEEEE "" ukitaka kujijua kuwa hauna dhambi ....basi fuatilia matendo ya police wa Tanzania....sasa angekufa hapo nje "" wange waambia nini watanzania ""....... Aiseee rasmi leo nimeona uzito wa ile kampeni ya kusaidia mama mjamzito inayofanywa na wizara ya AFYA ....."" police wa Tanzania "" ni wachawi "".....
Malaika Israel ana tawi lake kwa hawa jamaa
 

Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,534
2,000
Polisi sio cheo, ni wadhifa,
Pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, kuna baadhi ya mambo hawayafanyi sahihi, wanaonea sana RAIA wasio na hatia au kukuza mambo madogo, pia wanabambikia kesi watu.

Nb: polisi ni polisi tu hana urafiki ni wanaa sana.


Sijui kwenye course zao wanasoma mtaala wa wapi, ni kama wanafundishwa unyama dhidi ya binadamu na siyo usalama wa binadamu. mambo mengine hata wanyama pori hawawezi kuwafanyia binadamu, naona hii ni laana sasa!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom