Kilio wafanyakazi Vodacom Huduma kwa wateja. ISON BPO ni Fyonzaji, Erolink Ltd cha mtoto

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,321
Naam
Wakuu, leo hii majira ya saa nane mchana, nilipita mlimani city ilipo HQ ya Vodacom Tanzania.

Safari yangu hii ilikua ni kwa ajili ya kuonana na marafiki zangu niliosoma nao chuo wanaofanya kazi pale na ndipi nilipoona ukweli wa ule usemi kuwa, "utaona umuhimu wa kitu pale tu utakapokipoteza".

Wengi tunajua kuwa erolink ilikua ni kampuni inayorun operations ktk call center ya Vodacom kwa ufyonzaji mkubwa. Well, mwezi wa tano mwaka huu, walishindwa bid ya kuendelea kuoperate call center ya Vodacom na kampuni ya ISON BPO (ambayo ilikuwa tigo call center) ikawin hiyo bid.

Wafanyakazi wa call center walitegemea mabadiliko chanya kutoka kwa ISON BPO but mambo yamekuwa hoi zaid ya yalivyokua kwa erolink. ISON wamecopy kila kitu kutoka kwa erolink na kuondoa baadhi mambo muhimu kama night allowance (ambayo ipo kisheria) kwa shift za usiku. Erolink walikuwa wakilipa night allowance but ison wameondoa.. Nimeona copy ya mkataba wao.

ISON wanawafanyisha kazi wafanyakazi wale kwa masaa 9 kwa siku but masaa yanayolipwa ni 8 tu. Yaani lisaa limoja hawalipi kwa madai kwamba, lisaa hilo mfanyakazi anakua amekwenda lunch na tea. Kwa utaratibu wao, lunch ni dk 40 na tea ni dk 20. Hizo hawalipi japo umezitumia ukiwa ndani ya masaa ya kazi. (hili sijui limekaaje kisheria - wataalamu wa sheria tusaidiane). Erolink walikua wakilipa muda wa tea na lunch.

Kwa mujibu wa ISON, unapewa break ya dk 40 za lunch na 20 za tea. Hupewi muda wa washroom. Wapo strict sana. Mfanyakazi anakaa kwenye system masaa hadi manne au matano kabanwa mkojo anaogopa kutoka kisa hana dk za washroom. Huu ni Unyanyasaji mkubwa.

Tena nilichokishangaa zaidi, ni pale ambapo, ule muda wa dk 40 na 20 za break, inabidi wafanyakazi waje wakaulipie kwa kufanya kazi siku ya sita kwa masaa matano. Kulipia yale masaa waliyoenda break ktk siku tano za kazi.. This is bulshit. Yaani wafanyakazi nimekuta wakilalamika na kusema bora erolink.

Makampuni kama haya ya kidalali yanayokuja nchini na kuwanunua wafanyakazi wa kitanzania kwa bei rahisi na kuwauza bei ghali, yanahitaji kupewa mwongozo chanya usiowatesa watanzania.

Yaani vodacom inatoa 800,000+ kwa kila call center agent but, hizi kampuni Fyonzaji, zinakata nusu ya mshahara huo na kuwalipa basic salary ya 400,000. Makato yakipita hapo, mshahara unakua 310000 hivi. Hapo bado kampuni husika inalipwa pesa za kurun operations. Serikali inabidi irekebishe ile sheria ya kazi ya 2004 inayosema minimum salary kwa wafanyakazi wa makampuni ya simu iwe 400,000 gharama za maisha zimepanda. Huo mshahara ni mdogo kwa life la sasa.

Anyways, nimewahasa vijana waendelee kupiga kazi huku wakicheki mishe zingine. Maana kazi ya call center ni ngumu mno.. Ila hiyo waliyoipata wasiiache kwanza hadi wapate kazi zingine. Mtaani pagumu.
 
Kwa maelezo haya ya undani kuhusu kampuni.. Bilashaka anayelalamika ni ww na usimsingizie rafiki yako.
Kuhusu masaa ya kazi angalia attachment ya sheria ya kazi..
2017-06-22 00.51.35.jpg
 
Kwa maelezo haya ya undani kuhusu kampuni.. Bilashaka anayelalamika ni ww na usimsingizie rafiki yako.
Kuhusu masaa ya kazi angalia attachment ya sheria ya kazi..
View attachment 528561

Mkuu,

hakuna mijitu mijinga kama hii mifanyakazi ya hizi kampuni. Unapohangaika kuwaletea hizo sheria maana yake waende wakashitaki mahakamani.

Ni mapumbavu haya mabwana kwa sababu hakuna hata mmoja atakayekwenda mahakamani, wanadhani mahakam yao ni huku Jamii Forum kama anavyofanya huyu mwehu.
 
We acha kazi au waambie waache kazi waende kwenye nafuu kwani nani kawalazimisha kufanya kazi hapo
 
Viongozi wenye dhamana na vyombo husika nadhani mnaona hili suala, kiuhalisia vijana wetu wanajua haki zao ila kutokana na ugumu wa maisha hawawezi dai haki zao kama wanafunzi wa elimu ya juu wanavyodai mikopo au vyama vya siasa, kwaiyo wasaidieni

Tukumbuke hawa ni vijana wa kitanzania wanaitaji mazingira bora zaidi ya kazi na hakuna wakuwasaidia zaidi ya nyie viongozi mliopewa dhamana ipo wazi wakisema wagome watafukuzwa kazi
 
Aisee.Minimum salary 400 000/=? Halafu mnasema ni ndogo, maisha magumu na.Mwalimu anaaeanza analipwa.Almost the same, yeye nadhani maisha yake hayana shida, kweli? Basi ajila ni uchaguzi wa ntu,
 
Aisee.Minimum salary 400 000/=? Halafu mnasema ni ndogo, maisha magumu na.Mwalimu anaaeanza analipwa.Almost the same, yeye nadhani maisha yake hayana shida, kweli? Basi ajila ni uchaguzi wa ntu,
mwalimu analipwa laki 4 lakini ana muda mwingi wa kupumzika na kufanya shughuli zake binafsi.
 
Muhindi hajawahi kuwa ndugu wa mwafrika hata siku moja.
Hawa jamaa wanachezea sana sheria na taratibu za Nchi yetu. Sijui kiburi hiki wanakitoa wapi? Kuna kampuni moja kubwa tu (jina kapuni) Mswahili na Muhindi wanaofanya kazi inayolingana unakuta Muhindi analipwa Tsh 2.5 mil (kwa mfano) kwa mwezi. Muhindi huyo amepewa apartment anakaa bure Kariakoo na wamepewa usafiri wa ofisi au pikipiki na chakula wanapikiwa na ofisi. Mtanzania anayefanya kazi hiyo hiyo ya muhindi unakuta analipwa laki 9 mpaka 1milion ....hapewi makazi wala usafiri. Inasikitisha mnoooo.
Wizara husika sijui iko wapi kuangalia Maslahi ya Watanzania halisi!?
 
ISON BPO(Zamani Spanco) ni wanyonyaji hasa waliotukuka.Pale Airtel walifukuza staff wote waliowakuta wanalipwa juu ya 800,000+ iwe na Call Center Agents,Team Leaders,Back Office hadi watu wa Quality. Baada ya hapo wakasusha mshahara gross hadi 422,000 ssaiz nasikia wameshusha tena hadi 300,000.

Ila ushauri wa bure tu ni kwamba Wahindi ni waoga sana Mahakamani ikitokea tu mmojawenu au kikundi kikaenda kufungua kesi basi mnashinda kirahisi.

Pale Airtel masupervisors waliofukuzwa kimakosa walienda CMA(Court of Mediation and Arbitration) wakashinda kesi na kulipwa mamilioni Wahindi ikala kwao ila naona bado tu hawajifunzi
 
Tatizo call center wafanyakazi wapo wa elimu tofauti tofauti.

Kuna wa degree, certificate, na diploma. Wote wanalipwa mshahara sawa.

Mtu wa degree anaeza tamani kuanzisha mgomo but haezi pata sapoti ya mtu wa certificate maana certificate wanaona mshahara ni unaridhisha kwao
 
Mbona unawa- undermine wenye certificates? Ulitakiwa kutoa ushauri kuwa watu waungane kupitia vyama vya wafanyakazi. Kwa sababu ndiyo chombo pekee kinachowawezesha wafanyakazi kudai haki zao. Na hapa hakuna mwenye degree, diploma, certificate etc.
 
Mbona unawa- undermine wenye certificates? Ulitakiwa kutoa ushauri kuwa watu waungane kupitia vyama vya wafanyakazi. Kwa sababu ndiyo chombo pekee kinachowawezesha wafanyakazi kudai haki zao. Na hapa hakuna mwenye degree, diploma, certificate etc.
Sija wa undermine, hiyo ni reality iliyopo.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom